Nini kitatokea siku ya mwisho kama binadamu wengine watakua nje ya dunia?

Hadith za kwenye vitabu vya mapokeo zina matango pori ya kutosha,
Anyway hakuna kitu kinaitwa siku ya mwisho na blaa blaaa za jehanamu hizo ni hadith za kujifurahisha tu kama ilivyo sungura na fisi!

Povu rukhsaaaaa!
Unajidanganya na kiburi cha uzima baada ya kula na kushiba. Siku ile ipo, inakuja na inawaka kama tanuri. Siku ya wote wenye mwili kukusanyika mbele ya kiti cha hukumu ipo ndugu yangu. Mungu ni halisi, hukumu ni halisi na Jehanamu ya moto ni halisi. Acha kiburi cha uzima wewe mwanadamu uliye mavumbi.
 
Siku ya Mwisho inamaanisha ni mwisho wa Mambo yote. Kila Mwanadamu atasimama mbele ya kiti cha hukumu cha Mungu regardless alipo. Biblia katika Ufunuo wa Yohana 20:11 na Daniel 12:1-4, Mathayo 25: 32 vinaeleza watu wote wafu kwa walio hai watakusanyika na kuhukumiwa. Kwa hiyo hata hao watakaokuwa wapo Mars, Mwezini, Kuzimu, Baharini n.k watakusanyika mbele ya kiti cha enzi cha Mungu kwa ajili ya hukumu.
 
Unajidanganya na kiburi cha uzima baada ya kula na kushiba. Siku ile ipo, inakuja na inawaka kama tanuri. Siku ya wote wenye mwili kukusanyika mbele ya kiti cha hukumu ipo ndugu yangu. Mungu ni halisi, hukumu ni halisi na Jehanamu ya moto ni halisi. Acha kiburi cha uzima wewe mwanadamu uliye mavumbi.
amka wewe acha kuota hakuna kitu Kama hicho et Jehanamu hizo ni Hadith za kale za wayunani na wayahudi wa kale Kwanza unajua asili ya neno Jehanam?
Hizo Hadith za hio jehanum ilikua ni mifano ya vitisho kwa watoto ili wafuate njia njema Katika maisha yao
Jehanum lilikua ni dampo kubwa la takataka lililokua nje ya jiji la Jerusalem ya kale dampo Hilo lilikua linatumika kuchomea takataka za mji na lilikua likiwaka Moto kipindi chote Cha mwaka hivyo wayahudi ili kuwatisha watoto wafuate maadili na tamaduni zao wakawa wanaambiwa ukitenda mema utaenda kuishi bustani nzuri paradiso na ukiwa mwovu utaenda kuchomwa Moto mithili ya ule unaowaka katika dampo la Jehanam

Kwahiyo ndugu unavyoleta vitisho vya hiyo Jehanamu uwe unafuatilia historia Kwanza ndio maana nadiriki kusema hizo ni Hadith zilizopitwa na wakati hazina uhai katika zama hizi!

The terrible!
 
Habari zenu nyote,

Bila shaka wote mmesikia, mmeona juhudi za binadamu katika harakati za kutafuta sayari nyingine tofauti na dunia ambayo ina hali kama dunia yetu, chombo cha Marekani kishafika mars, swali langu kwa wajuzi wa masuala ya dini, siku ya mwisho itakuaje kama binadamu wengine watakua mars? Je Mungu ataangamiza sayari nyingine zaidi ya dunia? maana kwa mujibu wa mafundisho ya biblia, Mungu ataangamiza dunia(tu) na kila kilichomo maana dunia ndio sayari(pekee)iliyomkubali shetani

2 petro 3:10 "siku ya bwana itakuja kama mwizi siku hiyo, mbingu zitatoweka kwa kishindo kikuu, vitu vyake vya asili vitateketezwa kwa moto, nayo dunia itatoweka pamoja na kila kitu kilichomo ndani yake"
Wasalaam Forest Hill!

Yawezeka bibilia ikawa umesema zaidi ya hapo kwakuwa weye si mbobezi ukawa umebahatika kukutana na mstari huo pekee!

Katika uislamu Allah Subhanah hu wataala anasema yeye husema "KUN FAYA KUN" maana "KUWA NA HUWA" hivyo sioni kama itakuwa ni issue kubwa kwake hata kama ungekua umejifukia katika tumbo la ardhi
 
Wao hawaamini kama kuna hiyo 'siku ya mwisho'. Usipoteze nguvu kwa kuwaza mambo yasiyo na faida
 
Wanadamu tuna limit ya kufikiri i think kama wote sisi tunaamini katika dini there is nothing nje ya vitabu vya mungu na ukitaka kupata jawabu lolote rejea maandiko au nenda kwa wasomi wa dini, never judge anything without being full informed about it. kama unataka Kufikiri sana katika baadhi ya mambo especially ya kiimani jaribu kumshirikisha mungu possibly utapata mwanga wa kweli but ukijifanya man alone lazma utaenda wrong na utamkosea mungu but kama kuna mwanasayansi hapa aendelee kuamini katika sayansi yake cse hawaamini mungu.
 
Habari zenu nyote,

Bila shaka wote mmesikia, mmeona juhudi za binadamu katika harakati za kutafuta sayari nyingine tofauti na dunia ambayo ina hali kama dunia yetu, chombo cha Marekani kishafika mars, swali langu kwa wajuzi wa masuala ya dini, siku ya mwisho itakuaje kama binadamu wengine watakua mars? Je Mungu ataangamiza sayari nyingine zaidi ya dunia? maana kwa mujibu wa mafundisho ya biblia, Mungu ataangamiza dunia(tu) na kila kilichomo maana dunia ndio sayari(pekee)iliyomkubali shetani

2 petro 3:10 "siku ya bwana itakuja kama mwizi siku hiyo, mbingu zitatoweka kwa kishindo kikuu, vitu vyake vya asili vitateketezwa kwa moto, nayo dunia itatoweka pamoja na kila kitu kilichomo ndani yake"

“...siku hiyo, mbingu zitatoweka kwa kishindo kikuu...”

Nadhani hapo kwenye “mbingu” pana kila kitu kingine ikiwemo hiyo sayari ya Mars.
 
Vitabu vingi vinataja ulimwengu

YESU alikuja kuukomboa ulimwengu ....
.
.
.
.
Yesu atakuja kuhukumu ULIMWENGU NA SIO DUNIA
 
amka wewe acha kuota hakuna kitu Kama hicho et Jehanamu hizo ni Hadith za kale za wayunani na wayahudi wa kale Kwanza unajua asili ya neno Jehanam...
Hii kitu hata mapadre wanafaham, maana kuna padre mmoja, alishawahi kutuhutubia hii kwa kirefu zaidi.. Na mwisho, alimalizia kwa kusema, adhab kubwa kiumbe chochote ni kutokuona ufalme wa mungu.. Ila maswala ya moto ni story tu
 
Back
Top Bottom