Nini kitatokea ikiwa marehemu aliombwa akifa azikwe sehemu fulani lakini akazikiwa sehemu nyingine?

Mr Nyau

JF-Expert Member
Oct 18, 2018
1,128
2,337
Nini kitatokea ikiwa marehemu aliomba/alitaka akifa azikwe sehemu fulani lakini akazuiwa sehemu nyingine?

Naomba kufahamishwa wajuzi wenye historia waliowahi shuhudia matukio haya ikiwa marehemu wakati wa Uhai wake aliomba/alitaka akifa azikwe sehemu fulani lakini baada ya kifo Ndugu/jamaa wakiandika eneo tofauti na aliposema nini hutokea?

Share experience

Naomba uzi huu usiunganishwe ama kufutwa iwe sehemu ya mafundisho kwa wasomaji wote.

Tupate elimu kwakuwa sote tuna ndugu/jamaa na sote tutarudi mavumbini.
 
Bibi yake baba tulipotaka kumzika sehemu tofauti na aliyotaka yeye tulishindwa kuchimba kaburi ardhi aikufunguka kwa kitu chochote unachokijua wewe hadi pale alipombwa kuwa baadae watahamisha kaburi.kwakuwa wakati huo kulikuwa hakuna mtu ambaye alikuwa na uwezo wa kuusafisha mwili huo.ambaye alikuwa na uwezo huo kwa wakati huo alikuwa Dar.
 
Hakuna kitakachotokea bali watu watasema watachoka
Kwa sisi baadhi tunaamini unaweza kufa popote pale na kuzikwa ulipofia mradi kuna binadamu wa kuzika

Sasa unasisitiza kuzikwa kwenu au karibu na makaburi ya wazazi halafu unaliwa na fisi
Yaani mimi naomba mwisho mwema tu haya ya kufa na kuzikwa wapi yakae pembeni hayanisaidii chochote

Kuna ndugu mliowazika karibu lakini mliwasahau hata kwenda kusafisha makaburi

Hata humu wamejaa waliowazika wapendwa wao ila wakaendelea na maisha yao wala hawakumbuki jamaa zao walizikwa mstari upi
It's a shame
 
Maisha ni yako ila msiba ni wetu , ishi maisha yako mambo ya msiba wako waachie ndugu jamaa na marafiki.
 
Wachagga walipata changamoto sana kumsafirisha marehemu walipokinzana na kile alichosema kuhusu mahali pa kuzikwa (mfano ajali kutokea wakati wa safari, viiini macho etc)

Nadhani kuna namna ya kufuta kauli yake isilete madhara --- @ Mshana
 
Nini kitatokea ikiwa marehemu aliomba/alitaka akifa azikwe sehemu fulani lakini akazuiwa sehemu nyingine?...
Naomba kufahamishwa wajuzi wenye historia waliowahi shuhudia matukio haya.. ikiwa marehemu wakati wa Uhai wake aliomba/alitaka akifa azikwe sehemu fulani lakini baada ya kifo Ndugu/jamaa wakiandika eneo tofauti na aliposema nini hutokea?

Share experience

Naomba uzi huu usiunganishwe ama kufutwa iwe sehemu ya mafundisho kwa wasomaji wote...

Tupate elimu kwakuwa sote tuna ndugu/jamaa na sote tutarudi mavumbini
Hakuna chochote linaweza tokea mtu akisha kufa basi it's no more walio hai ndiyo wenye maamuzi ya azikweje
 
Ni imani tu, ila mwanadamu akishakufa kumbukumbu lake linatoweka hawezi jua kinachoendelea duniani....soma Ayubu hapa chini.

AYUBU: MLANGO 14.

10 Lakini mwanadamu hufa, huifariki dunia; Naam, mwanadamu hutoa roho, naye yupo wapi?

11 Kama vile maji kupwa katika bahari, Na mto kupunguka na kukatika;

12 Ni vivyo mwanadamu hulala chini, asiinuke; Hata wakati wa mbingu kutokuwako tena, hawataamka, Wala kuamshwa usingizini.

21 Wanawe hufikilia heshima, wala yeye hajui; Kisha wao huaibishwa, lakini yeye hana habari zao.

Kwa hiyo utaona kwamba waabudu mizimu, wakiwemo wale watambikaji huwa wanaishia kuabudu mapepo tu, maana marehemu hawajui lolote linaloendelea katika nchi ya walio hai.
 
Back
Top Bottom