Nini kinaendelea kati ya spika na John Mnyika?

Nini kinaendelea kati ya spika na John Mnyika?

Kama utakua unafwatilia bunge basi utakubariana na mimi kua. Kwa siku za hivi karibuni spika ameonyesha chuki za wazi dhidi ya mnyika. Hali inayo pelekea spika kushindwa kuzuia hisia zake nakujikuta anasahau kua yeye ni spika na kuanza kumshambulia Mnyika inpersonal.

Mkuu nimemfuatilia huyu mama tokea juzi, Jana na Leo asubuhi, kwa kweli nimeshindwa kumwelewa. Chuki zake kwa Mnyika na Tindu Lissu yamekuwa dhahiri Sana. Kimsingi naona hata wakati mwingine anaamua kuvunja kanuni za bunge kwa makusudi Ili tu kulinda au kutetea serikali.
 
Mnyika akirudi hapa ubungo nahama nchi,huyu jamaa ni kichwa Nazi hajafanya lolote hapa jimboni ni kelele tu bungeni

....we ni boga kabisa tena limeoza, Kai anayofanya mnyika imevuka mioaka ya ubungo na inatambulika kwa taifa na nje ya Tanzania .Mmekaa miaka 50 mijitu imekula taifa mlikuwa kimya, leo mnyika and team wameonyesha mini maana ya kazi ya mmbunge unajifanya eti nahama nchi. wakati hata Kigamboni huwezi kumudu...
 
Mnyika kashindwa kuleta maendeleo ubungo kabaki kupayuka tu maendeleo hayaletwi kwa maneno matupu.
 
ulimsikiliza jana Simba chawene ITV?

Issue imetokea Bungeni na sio ITV, kama kweli walikubaliana mswaada uletwe kwa nini mama Makinda hakuongea pale Bungeni?

Kwanini akae kimya na kukimbia ukumbi wa bunge kama kulikua na makubaliano?

Simbachawene wakati anaongea alijua hakuna mtu wa kumchallenge.
 
11000053_1790682141157892_6120419612937126814_n.jpg
 
Mnyika akirudi hapa ubungo nahama nchi,huyu jamaa ni kichwa Nazi hajafanya lolote hapa jimboni ni kelele tu bungeni

Nadhani hujui mchango wa Mnyika kwenye bunge hili la 10.
Ubungo na Taifa zima wananufaika na hoja zake. Haijalishi amefanya nini kwenye jimbo lake lakini kama mi ningekuwa napiga kura jimbo la Ubungo definitely ningempigia arudi jimboni kwa ajili ya hoja zake.
Suala la amefanya nini bungeni ni suala lenye mapana sana. Serikali ndio iliyoshika mpini na inaweza ika sabotage sana mipango yako kwenye jimbo kwa sababu yenyewe ndio inayotoa hela.
Hujaona barabara ya Goba - Mbezi Kiamara imejengwa kipindi hiki chake, hauoni maji yameboreshwa kwa namna moja jimboni mwake.
Hiyo barabara ya Strabag mradi wa mwendo kasi uko kwenye jimbo gani?
Unataka akuletee mkate na mayai mezani kwako kila siku asubuhi?
 
Mnyika akirudi hapa ubungo nahama nchi,huyu jamaa ni kichwa Nazi hajafanya lolote hapa jimboni ni kelele tu bungeni
Tuwe wakweli na waungwana ili kutendea haki nafasi tuliyoipata ya kuishi.
Mh. Mnyika sio kafanya kazi kwa Ubungo tu bali amelitumikia taifa zima. Ninavyoona kazi ya Mnyika kwa miaka mitano aliyojaaliwa kuwemo Bungeni ni kubwa kuzidi kazi za wabunge wengi ambao wengine wamekaa zaidi ya miaka 15 bungeni akiwemo spika mwenyewe! Huu ni ukweli unaouma kwa wenye kinyongo kama wewe na ccm wengi na historia itasema ukweli.

Kama utakua unafwatilia bunge basi utakubariana na mimi kua. Kwa siku za hivi karibuni spika ameonyesha chuki za wazi dhidi ya mnyika. Hali inayo pelekea spika kushindwa kuzuia hisia zake nakujikuta anasahau kua yeye ni spika na kuanza kumshambulia Mnyika inpersonal.

Kinachoendelea kati ya bibi kiroboto na mnyika ni UNDAVA , Yaani UNYAMA UNYAMANI.
 
Nadhani hujui mchango wa Mnyika kwenye bunge hili la 10.
Ubungo na Taifa zima wananufaika na hoja zake. Haijalishi amefanya nini kwenye jimbo lake lakini kama mi ningekuwa napiga kura jimbo la Ubungo definitely ningempigia arudi jimboni kwa ajili ya hoja zake.
Suala la amefanya nini bungeni ni suala lenye mapana sana. Serikali ndio iliyoshika mpini na inaweza ika sabotage sana mipango yako kwenye jimbo kwa sababu yenyewe ndio inayotoa hela.
Hujaona barabara ya Goba - Mbezi Kiamara imejengwa kipindi hiki chake, hauoni maji yameboreshwa kwa namna moja jimboni mwake.
Hiyo barabara ya Strabag mradi wa mwendo kasi uko kwenye jimbo gani?
Unataka akuletee mkate na mayai mezani kwako kila siku asubuhi?
Naona hata 'like' haikutoshi mkuu. Kumbe tunaoelewa tupo japo nilikuwa naelekea kukata tamaa!
 
Naona hata 'like' haikutoshi mkuu. Kumbe tunaoelewa tupo japo nilikuwa naelekea kukata tamaa!

Kaka ukiingia kwenye jukwaa hili kuna kibarua kikubwa sana cha ku deal na watu wenye akili ndogo sana ambao wamejazana sana humu. Aidha inawezekana akili zao zimekamatwa sehemu, au wanalipwa kufikiria hivyo wanavyofikiria au wanazi wa vyama fulani fulani ambavyo vimeshakufa kwenye medani za siasa hapa Tanzania.
Kibarua hiki si kidogo kaka. Mi na wewe wote tumekichukua pindi tulipojiunga na jukwaa hili.
Usichoke
Ndo maisha kaka.
Zigo zito mpe mnyamwezi. Na we na mimi ndo wanyamwezi wenyewe.
 
Bahati Mbaya Mnyika ni miongoni mwa wabunge kumi bora kabisa Tanzania, kwahiyo ana uhakika wa kushinda kuliko wakati uliopita. Na hata akishindwa kwa goli la mkono rekodi yake inatosha.

Amesema akirudi , sasa atahamje wakati hayajatimia.
 
Muacheni Mnyika apambane anajua watu wote wanamuangalia kwenye tv, ubungo maji hamna lazima atafute cha kuongea kwenye kampeni.

Naona Ubungo hawakuahidiwa maisha bora kwa kila mtanzania au mnajitoa ufahamu?
 
Kipindi kile wanaelewana sana mpaka Anne alipokuwa anamlalamikia kwa kusema

"Hivi mnyika mbona ni mkorofi hivi nimekukosea nini Mimi, nikupe nini utulie. Mbowe nisaidieni jamani"

Silivuma habari kwamba wanamahusiano.

Sasa kama sikuhizi wanagombana labda wametengana.
 
Back
Top Bottom