Nini kimewakumba Halotel?

Nini kimewakumba Halotel?

Zamani ht LIVESTREAM nilikuwa nacheki fresh lakini siku hizi haiwezekani inakwamakwama...sema kwa bongo sijaona mtandao mwingine wa kukimbilia maana nina experience na majanga ya Tigo ,voda ,Aittel zote ziliniboa
mina nazani watu wameshaongezeka sasa ndo inaleta shida ila mida ya asubuhi inakuwa fresh ata hivyo halotel bado tunawaamini ni wepesi kusikiliza mwanzo kulikuwa kuna tatizo la mb kwenda haraka ila sasa naona wameboresha ilo kama una mb 600 kwa matumizi ya kawaida utatumia wiki nzima bila kuisha
 
Mdau wa ndani kabisa alinijuza wanalaunch kifaa kipya kwa ajili ya 4G LTE itachukua miezi miwili kurudi kwenye ubora wao au zaidi

Miezi miwili yote hiyo ya nini - kufanya majaribio? Huo mbona muda mrefu sana.
Mtandao wao umekuwa hovyo kwa kiwango cha kutisha. Ikichukua miezi miwili kwa speed hii ya kukatika-katika, hakuna mteja atabaki kwao.
 
Nyie mtakuwa watu wa tigo yaani sisi tunavyotesa na Halotel bye mnalalamika!
tofauti ipo tena kubwa sana kipindi wanaanza na walivyo sasa hili hata wenyewe wanajua kwa namna watu wanavyo walalamikia cha ajabu sijui ni kwa nini hawana ufumbuzi
 
U
tatizo mb zinaliwa fasta mno

Ukiona mb zinaliwa faster ujue mtandao uko poa sana( faster) sio kama wale wengine wanakupa mbS kibao wanauhakika huwezi kuzitumia zote sababu speed wanayotoa ni ndogo"
 
Hamna kitu mkuu, speed imepungua sio kama mwanzo
Inategemea ni saa ngapi na ni maeneo gani. Maeneo ya vyuo mlipo jazana lazima sipidi ipungue.

Lakini ukitaka kuwatambua halotel ni kina nani NENDA PORINI PASIPO NA MAKAZI KISHA TUMIA KIFAA CHAKO. NI KASI YA AJABU.

Vijijini Halotel hawana mbadala. Wengine woote mitandao yao huko mashambani ni 2G hasa Voda na Tigo. Halotel ni 3G nchi nzima.

Kuna maeneo kasi huwa ni kubwa hadi nahisi nimejiunga peke yangu kwenye mnara.
 
Kurudi Airtel ni sawa na kushuka kwenye basi na kupanda mkokoteni
Ni kweli. Airtel wamekuwa ghali sana. Voda wana nafuu kidogo ya bei na mijini internet yao iko vizuri.

Kwa walioko Dar internet ya kasi na bei poa inapatikana TTCL. kitu cha 4G LTE ya ukweli.
 
Ni kweli. Airtel wamekuwa ghali sana. Voda wana nafuu kidogo ya bei na mijini internet yao iko vizuri.

Kwa walioko Dar internet ya kasi na bei poa inapatikana TTCL. kitu cha 4G LTE ya ukweli.
TTCL iko posta na Kariakoo pekee hata ubungo haishiki!
 
Wikiend Imefika Nimebadilisha Line ya Halotel sasa Natumia Voda nianze Ku stream Game ya Man City na Southampton na Chelsea Vs Manchester United. For just 1024MB
 
Sikuizi speed imepungua saaana
 
Back
Top Bottom