GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 56,742
- 109,177
Binafsi zaidi ya mara Tano ( 5 ) au Saba ( 7 ) nilimsikia na kumuona mara kwa mara alipokuwa akihojiwa akisema kuwa hatokuja Kuvaa Viatu kamwe na kwamba sehemu zote atakazokuwa anaenda au anatembea atakuwa na ile ile ' Identity ' yake ya ' Pekua Peku Daima ' ila nimeshtushwa na taarifa yake mpya.
Ni kwamba Msanii Mrisho Mpoto katika hali isiyokuwa ya kawaida amemua Kulamba ' Matapishi ' yake ya ' Kinadhiri ' rasmi kwa kusema kuwa Kuanzia sasa atakuwa anavaa Viatu na kwamba hatotembea tena ' Peku Peku ' kama ilivyozoeleka na alivyokuwa ' amejibrandi ' hivyo mwenyewe.
Sababu alizotoa ama hakika zimenifanya nibaki Kushangaa na kuwa na Maswali mengi ya Kumuuliza ila pia kupitia tu hayo Majibu au hizo sababu zake kadhaa alizozitoa juu ya haya Maamuzi yake mapya Mrisho Mpoto amenifanya nizidi Kuamini kuwa ama hakika Bange / Bangi ni mbaya mno kwa Matumizi ya Mwanadamu / Binadamu na kwamba kila Mzazi nashauri ahakikishe Mwanae asitumie huu ' Mmea ' kwani unaharibu sana mfumo mzima wa ' Medulla Oblangata ' ya Mwanadamu.
Je na Wewe mwana JamiiForums unadhani ni kwanini Msanii Mrisho Mpoto ameamua Kulamba Matapishi yake mwenyewe na kwenda Kinyume kabisa na ' Nadhiri ' yake aliyoiweka na aliyotuaminisha nayo kwa miaka mingi tu tokea alipoanza rasmi Kujulikana na kuwa Msanii mkubwa hivi? Hivi Binadamu / Wanadamu wanajua madhara ya kwenda Kinyume na ' Nadhiri ' zao ambazo walijiwekea wenyewe tena mbele za Watu?
Nawasilisha.