Song of Solomon
JF-Expert Member
- Aug 5, 2021
- 2,733
- 5,490
Kelele ni nyingi na shahuku ni kubwa lakini maneno yangu ni machache;
Makonda hatakuwa na wakati mzuri wakati huu ambapo kundi la Msoga lina nguvu ndani ya CCM na Serikali. Kundi la Msoga ni kundi la Wazee wakongwe, wenye nguvu ndani ya CCM, na pia wenye majeraha waliyopatiwa wakati wa Magufuli.
Pia ni kundi lenye vijana wenye ndoto za kushika madaraka makubwa kuliko waliyonayo sasa, kupata/kupora fedha nyingi zaidi ya walizonazo sasa, na zaidi wanadharau kubwa kwa watu wanaowaona si wa kundi lao. Makonda atapaswa kurudia enzi zake za kulamba viatu vya kina Ridhiwani Kikwete, au awe mpole na kutojihusisha sana na mambo ya watu.
Ubabe, Kiburi na Jeuri zake hataweza kuziishi kwa sasa kwa kuwa yeye si kijana wa kundi hilo. Na zaidi hana mahusiano mazuri na kundi hilo lenye nguvu.
Rekodi yake ya kupora mali kwa wafanyabiashra, kuwadharau na kuwakandamiza watu wa chini yake - ambao hawakuwa na nguvu hata ya kulalamika enzi za Magufuli, inamuweka kwenye nafasi ya kuwa mtu wa kujitafakari sana kwa kila atua anayopiga.
Makonda aliwahi kumuonesha dharau hadharani Bw. Daniel Chongolo wakati yeye Makonda akiwa RC wa Dar es Salaam na Chongolo akiwa Mkuu wa Wilaya wa Kinondoni.
Makonda ni mtoto wa kundi lililotengwa kisiasa wakati huu. Amerudishwa ili kupunguza uwezekano wa uasi ndani ya CCM lakini je, tasaidia kitu? Kundi maarufu la Wendazao, ambalo nguvu yake kubwa ni wingi wa kura za Mkutano Mkuu wa CCM, limekosa nguvu za kisiasa ndani ya CCM baada ya kundi la Msoga kushika hatamu.
Mabadiliko ya mara kwa mara kwenye baraza la Mawaziri yamezingatia makundi haya mawili; Msoga na Wendazao. Mara nyingi kundi la Msoga limeibuka kidedea, kwa kupewa wizara nyingi na nyeti.
Kwahiyo Makonda atakuwa akifanya kazi kama mwakilishi wa kundi la Wendazao, wakiongozwa na kundi hasimu la Msoga.
Hatatakiwa kwenda kinyume na Msoga ili aendelee kubaki kwenye hiyo nafasi, na hapo itampasa kufanya kazi kwa upole na adabu - kinyume na haiba yake ya kiburi na dharau.
Sisi kazi yetu ni kuchambua!
Nawasilisha
Dr. Chris Cyrilo.