Nimejua kwa nini roho yangu huburudishwa sana na nyimbo zenye maudhui ya Neno la Mungu

FaithClass

Member
Jul 16, 2023
14
114
Ilishanitokea mara nyingi, japo sikujua sababu hasa. Nilijua roho yangu huitikia vizuri sana nyimbo zenye jumbe za Neno la Mungu.

Hata kama nilikuwa nikitembea njiani huku nafsini najisika kukaukiwa au hali ya utupu, nikipita sehemu wanakopiga wimbo mzuri unaokubaliana na Maandiko Matakatifu, kuna namna moyo wangu huchangamka na hali ya kububujika huamshwa ndani yangu. Hali hiyo hunifanya "nihisi" hali ya "upako" wakati hapo kabla ya kuusikia huo wimbo, ingelitokea nikaambiwa "nihubiri" au hata niombee chakula, ningefanya hivyo kwa vile imenilazimu tu. Upako wa kufanya hivyo unakuwa upo chini sana au haupo kabisa. Hiyo ni kutokana na hali ya ukame ninayoihisi nafsni muda huo.

Ndivyo ilivyo pia kwa maneno niyasikiayo. Kama ni ya Imani, au maneno chanya, huniacha nikiwa na hisia za ushindi moyoni. Lakini kama ni ya kukatisha tamaa, huenda nikajikuta ninajuta kuyasikiliza.

Maneno yana nguvu sana, kuliko watu wengi wanavyofikiria. Laiti wengi wangefahamu hilo, na wakachagua kuyatumia kwa faida, wangekuwa na mazuri mengi ya kusimulia kuzidi waliyo nayo kwa sasa. Kila mmoja angekuwa nayo bila kujali dini yake, umri wake, rangi yake, kabila lake, na itikadi yake ya kisiasa.

Baada ya kugundua kuwa maneno niyasikilizayo huniathiri hali yangu ya ndani, nimekuwa na tabia ya kuwa "mbaguzi" sana juu ya yale niyasikiayo na niyasemayo. Ninakuwa makini sana kuchagua cha kusikiliza na cha kuongea.

Hata ninaposikiliza mahubiri, nimekuwa nikifanya kile wengine wanachosema KUMEZA WALI NA KUTEMA MAWE. Ikitokea kimesemwa kilicho sahihi kinachokubaliana na Neno la Mungu, nitakipokea bila kujali nani kakisema. Lakini, kama kinapingana na Neno la Mungu, sitakichukua. Nitaamini kile kilicho sahihi kwa mujibu wa Neno la Mungu na kile kilicho kinyume na Neno, nitakiacha papo hapo kilipotamkwa hata kama kilitamkwa na mtu anayeaminika sana na watu wote ulimwenguni. Sitaruhusu kiingie moyoni mwangu.

Kwa muktha wa mfano nilioutumia hapo juu, WALI ni maneno mazuri na MAWE ni maneno yenye kujenga mitazamo isiyo na tija yaliyovaa "suti" ya dini.

Hata nyimbo pia, ziwe ni "secular" au za Kwaya, zikiwa zinapingana na Maandiko Matakatifu, nitajizuia kuzisikiliza. Nyimbo nyingi za "kidunia", ikitokea zimesikika masikioni mwangu kwa muda mrefu, hunifanya nihisi hali ya upako/utayari wa kuomba, kuhubiri, n.k. kupungua au hata kuisha kabisa moyoni mwangu. Lakini nikienda penye utulivu na kuanza kusoma Biblia, hali ya "kuhisi" uwepo wa Mungu hurejea.

Siku za nyuma nilikua nikifikiri nina aleji ya nyimbo za kidunia, lakini sasa nimeshaujua ukweli. Ni kwa sababu ya asili ya moyo wangu, kwamba, una asili ile ile aliyo nayo Mungu. Kwa hiyo, Neno Lake linaposikika masikioni mwangu, huichochea Hiyo asili ndani yangu, kama vile kuiamsha tayari kwa utendaaji wa yale yanayoendana na Neno la Mungu .

Nimekaribia kumaliza kukisoma kitabu kidogo kinachoitwa "GENETICS OF WORDS". Nimekipata kupitia "group" la "WhatsApp" liitwalo "CHRISTIAN LIBRARY". Ni kupitia hicho kitabu nimeweza kubaini kinachopelekea niwe na aleji na nyimbo nyingi za "kisecular" huku nikivutiwa sana na nyimbo za "Gospel".

Simfahamu sana mwandishi wa kitabu husika. Na pia bado sijakimaliza kukisoma, lakini ninakubaliana naye kwa asilimia zote juu ya kile nilichokwishakukisoma kwenye hicho kitabu.

Moja ya hayo mambo ni kuwa mtu anapomwamini Kristo, asili ya Mungu huingia rohoni mwake. Roho yake inakuwa imezaliwa na Mungu. Kama vile mtu anavyokuwa na vinasaba kamili vya wazazi wake, kadhalika, na roho ya mtu aliyemwamini Yesu nayo inakuwa na vinasaba halisi vya Mungu; YAKOBO 1:18, 1YOHANA 4:17, YOHANA 1:12, 13, YOHANA 3:6.

Inapotokea akalisikia Neno la Mungu au maneno yanayokubaliana na Neno la Mungu, ile asili ya Mungu iliyo ndani yake huamshwa au kuchochewa. Inakuwa kama vile inawekwa tayari kwa ajili ya kutenda kulingana na maelekezo yatakayotolewa na Neno la Mungu.

Kama hiyo haitoshi, mwili wa mwanadamu, DNA zake zinaweza kung'amua maneno mazuri na mabaya , nazo huitikia kulingana na maelekezo ya hayo maneno.

Namshukuru Mungu kwa ajili ya hicho kitabu cha GENETIS OF WORDS. Naweza nisiwe nimeshajua kila kitu, na inawezekana hata hicho kitabu hakijaandika kila kitu kuhusiana na hilo, lakini sasa, alau, nimepata mwanga. Nimejua kuwa ni asili ya Mungu ndani yangu ndiyo inayoitikia Maneno ya Kimungu yanayosikiwa na masikio yangu.

Mtu akilifahamu hilo, kutamsaidia sana katika maisha yake ya kila siku. Atajua kuwa anachokihitaji sana maishani mwake si watumishi wa kumwombea, bali Neno la Mungu. Akiwa na ufahamu wa Neno la Mungu, akilitamka kwa Imani, atapata matokeo anayoyatamani, iwe ni uponyaji, ulinzi, mafanikio ya kiuchumi, kimasomo, ndoa, n.k.

Kama alikuwa mgonjwa na amekata tamaa ya kupona, akiyasikia mafundisho sahihi juu ya uponyaji wa Mungu, Imani yake huweza kuhuika na kuwa tayari kwa utendaji. Akijua jinsi ya kuiachilia imani yake, uponyaji hautaweza kumpiga chenga. Na, njia mojawapo ya kuiweka imani yake katika utendaji ni kwa kulikiri Neno la Mungu kana kwamba limeshatendeka kwake, na ndivyo ilivyo katika ulimwengu wa roho.

Kwa upande wa Mungu, tayari ameshafanya kila kitu mwanadamu anachokihitaji. Ameshamalia kazi Yake. Wajibu alio nao mwanadamu ni kufahamu kile ambacho Mungu kafanya kwa ajili yake kupitia kufa na kufufuka kwa Yesu kristo, na kupokea kwa IMANI.

Kama ni uponyaji, tayari ameshaulipia. ImeandIkwa, KWA KUPIGWA KWAKE, SISI TUMEPONA; 1Petro 2:24, Isaya 53:5, Mathayo 8:17.

Si uponyaji tu, bali ni kila kitu. Kwa kadiri mtu aanavyojifunza Neno la Mungu na kuchukua hatua ya Imani, ndivyo na matokeo yatakavyozidi kuonekana kwake.

Ninajua inafanya kazi. Mimi binafsi nimeshafanya hivyo na nikapata matokeo ya amani.

Nilishafaulu mtihani wa chuo Kikuu kimuujiza, katika mazingira ambayo ilikuwa nifeli.

Nilishaponywa kwa imani madhaifu tofauti tofauti kwa nyakati tofauti: mafua, kikohozi, maumivu ya kichwa, typhoid, amoeba, majipu, vidonda vya tumbo, n.k., kwa njia ya kuliamini NENO LA MUNGU PEKE YAKE. Sikutumia dawa yo yote, isipokuwa NENO Peke Yake, nikapona kabisa. (Kutumia dawa au kwenda hospitalini si kosa).

Tena, miaka ya nyuma, ilikuwa ni kawaida kusumbuliwa na mafua nyakati za baridi, au nikiwa penye vumbi. Lakini baada ya kujua jinsi ya kulitumia Neno la Mungu kwa afya, mafua yalipoteza anuani ya kunifikia. Hata nikikaa katikati ya watu wenye mafua, hayanisogelei. Virusi vya mafua vimeshajua kuwa vikinigusa tu vinaishia kufa. Haviruhusiwi kabisa kukaa kwenye mwili wangu.

Nilishapata muujiza wa kifedha zaidi ya mara moja katika nyakati ambazo nilikuwa nikikabiliwa na changamoto ya kifedha.

Na mengine mengi.

Ingawa mimi nimekiona kitabu husika kuwa ni kizuri, kinaweza kisiwe kizuri kwa mwingine. Lakini nimeamua kukiambatanisha ili kama kuna atakayekipenda, naye aweze kukisoma. Nilikipata bila kulipia hata shilingi, isipokuwa bundle la Internet pekee, hivyo na mimi nimekitoa bila kutoza hata senti. Atakayekihitaji atagharamikia bundle la Internet tu.

Na kama utakiona ni kizuri, na wewe ukampatie mtu mwingne unayefikiri anakihitji.

Nilipewa bure, nimekitoa bure! Na wewe, ikikupendeza, ukakitoe bure, lakini baada ya kuijridhisha kuwa ni kizuri.

Karibu!
 
Attachments

  • Genetics of Words Recreating your World through the Supernatural Power behind your Words by Ue...pdf
    336.5 KB · Views: 17

Iweke hapa link ya group la Vitabu.
 
Hiyo ni HYPNOTIC INDUCTION hakuna cha UPAKO wala KUBARIKIWA na Wimbo.. Mziki una-create TRANCE STATE kwenye Ubongo wako....
 
Back
Top Bottom