saidoo25
JF-Expert Member
- Jul 4, 2022
- 602
- 1,407
Bunge limeridhia kuipa mamlaka Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Madawa ya Kulevya (DCEA), uwezo wa kuanzisha mahabusu zake na masharti ya kumuweka mtu kizuizini kwa kuzingatia taratibu za kisheria kabla ya mtuhumiwa kufikishwa mahakamani.
Wachambuzi hebu tuitazameni hii Sheria iliyopitishwa na Bunge letu jana Septemba 14, 2022 ili tuone nini kimejificha kwenye sheria hii.
Je, ni kweli Mahabusu zilizopo sasa za Polisi na Magereza hazina uwezo wa kuwatunza hao mahabusu wa Dawa za kulevya hadi Mamlaka ya Dawa za kulevya ianzishe Mahabusu zake maalum na je miaka yote mapambano ya dawa za kulevya yalifanyikaje?
Au kuna nini kinataka kufichwa nyuma ya pazia la kuanzisha Mahabusu maalum za Mamlaka ya Dawa za kulevya na Kwanini hoja hii Ridhiwani Kikwete aliishikia bango sana bungeni wakati ni jambo ambalo haliko kwenye Wizara ya Ardhi anayoingoza.
Wazuoni na wajuzi tulijadili ili tumuombe Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan asiweke sahihi sheria hii ili irudi bungeni ichakatwe upya kwa kuwashirikisha wadau wote ikiwemo wananchi na Jeshi la Polisi.
Chanzo: Mwananchi Septemba 15, 2022