Nini kilikwamisha Meli kubwa kutia nanga bandari Mtwara?

Ikija meli ya magari kutoka Japan, ina magari 300, kati ya hayo 250 yanakuwa ya wamiliki wa Dar yaliyobaki 50 ndio nchi jirani na mikoani.
Ikija meli ya makontena 500, 400 yanakuwa ya watu wa Dar,100 yaliyobaki nchi jirani na mikoani. Sasa meli kama hizi zitashusha Mtwara au Tanga?
 
Ikae Dar es Salaam kwa muda mrefu au ishushiwe Bandari ya Mtwara kwa muda mfupi, uongeze gharama ya mafuta lak2 au 3,kipi ni bora?
 
Bandari ya Dar ina kina cha kuchimbwa, hujaa matope, eneo dogo hivyo meli kubwa haina uwezo wa kuingia na pia kugeuza wakati wa kutoka,
Bandari ya mtwara ina kinakirefu cha asili.
 
Hoja ya msingi kulikopelekea bandari ya Mtwara kutotumika kikamilifu ni kukosekana na miundombinu ya kuunganisha pwani ya Mtwara na Miji na nchi za ndani kama vile Malawi na Zambia.Kwa sasa barabara ya kusini ya Tanzania Mtwara corridor itafunguka kwani barabara ya kutoka Mtwara hadi mbambabay itakuwa ya lami.Aidha,mipango ya ujenzi wa reli kutoka kwenye makaa ya mawe na chuma ipo mbioni hivyo bidhaa hizo zitatumia bandarini ya Mtwara kwa kusafirishwa nje ya nchi.Kwa kipindi kirefu bandari ya Mtwara imekuwa ya msimu tu kwa kutegemea kusafirisha korosho kati ya octoba na januari na hivi karibuni kumekuwepo na ongezeko la ujaji wa meli zinazohudumia makampuni ya utafiti wa mafuta na Kiwanda cha Dangote.
 
Kuna umbali sana bora kushushia bandari ya dar

Hivi mizigo ya congo inapitia kule kaskazini Rusumo au inazunguka kusini chini ya Ziwa Tanganyika? Kule kwenye mto wanakovuka kwa pantoni?( River Kabesi nadhani,niko tayari kusahihishwa)

Na nina uhakika umbali kutoka Dar mpk Kabesi ni mrefu kuliko umbali toka Mtwara. Tatizo ni miundombinu ya barabara pia
 
Hoja ya msingi kulikopelekea bandari ya Mtwara kutotumika kikamilifu ni kukosekana na miundombinu ya kuunganisha pwani ya Mtwara na Miji na nchi za ndani kama vile Malawi na Zambia.Kwa sasa barabara ya kusini ya Tanzania Mtwara corridor itafunguka kwani barabara ya kutoka Mtwara hadi mbambabay itakuwa ya lami.Aidha,mipango ya ujenzi wa reli kutoka kwenye makaa ya mawe na chuma ipo mbioni hivyo bidhaa hizo zitatumia bandarini ya Mtwara kwa kusafirishwa nje ya nchi.Kwa kipindi kirefu bandari ya Mtwara imekuwa ya msimu tu kwa kutegemea kusafirisha korosho kati ya octoba na januari na hivi karibuni kumekuwepo na ongezeko la ujaji wa meli zinazohudumia makampuni ya utafiti wa mafuta na Kiwanda cha Dangote.
Umesema kweli tupu mkuu, ingawa kwa sasa barabara ya Mtwara-Masasi-Tunduru-Namtumbo-Songea(Njombe-Makambako) ina lami kwa 98%. Hivyo visingizio hakuna tena. Hata hiyo 2% ambayo imebaki wakandarasi wanamalizia,wako site.

Kipande pekee ambacho kinahitaji Bajeti ni ile lami ya zamani kutoka Mtwara-Mnazi Mmoja-Masasi(km201),hiyo lami yake imechoka. Design Life ya miaka 20 imeshapita. Hivyo haiwezi kuhimili magari mazito, na hasa kipande cha Mnazi Mmoja hadi Masasi(km121)!
 
Sijajua gharama ya mafuta inayoongezeka ni ya nini.
Mkuu gharama za mafuta si umesema Dar ndiyo matajiri huleta magari mengi, sasa kama wako Dar, ukishushia Mtwara ili gari lifike Dar si lazima uliwekee mafuta kutoka Mtwara hadi Dar(km 565)
 
~~~>>>>Mtwara ndio Bandari yenye kina kirefu Afrika Mashariki....

~~>>>Nafikiri Sababu kuu ya kutokutumia zaidi Bandari ya Mtwara ni Sababu ya kijeographia....

Wateja wetu wa kuu ni Congo, Rwanda, Burundi na Zambia....

Ni gharama nafuu kusafirisha mizigo yao kutoka Dar kuliko Mtwara....

Naruhusu masahihisho.
 
Tatizo unaangalia gari moja. Angalia gharama ya kusafirisha magari mia mbili au tatu. Mafuta,mazingira etc. Demand si ndio inapeleka huduma sehemu? Au....
 
~~~>>>>Mtwara ndio Bandari yenye kina kirefu Afrika Mashariki....

~~>>>Nafikiri Sababu kuu ya kutokutumia zaidi Bandari ya Mtwara ni Sababu ya kijeographia....

Wateja wetu wa kuu ni Congo, Rwanda, Burundi na Zambia....

Ni gharama nafuu kusafirisha mizigo yao kutoka Dar kuliko Mtwara....

Naruhusu masahihisho.
Au wewe fikiria meli iliojaa magari 300, 200 ya dar,50 transit,48 mikoa mingine na 2 ya mtwara. Kiuchumi ikoje hio?
 
Meli kubwa iliyobeba magari ya Dangote imetia nanga bandari ya mtwara,kiasi kwamba imeshangaza Dunia kuona kwamba,kumbe mbali ya bandari ya Dar, Tanzania tuna bandari nyingine yenye uwezo wa kuingiza meli kubwa zaidi.

Nini kimefanya bandari hii kutotumiwa na meli kubwa kwa miaka yote hii?
Elewa bandari ya mtwara ndiyo yenye kina kirefu kuliko bandari za Dar na Tanga.tatizo lilikuwa logistic hasa barabara
 
Sasa utaziona nyingi Mtwara, hiyo bandari iliboreshwa na Kikwete.

Na kwa jitihada za Kikwete alizozifanya bila kuchoka kutuletea watafuta gesi na mafuta tutashuhudia mengi mapya kwa Mtwara na Tanzania nzima kwa ujumla.

Kikwete tutakukumbuka daima.
FaizaFoxy Kikwete
 
Umesema kweli tupu mkuu, ingawa kwa sasa barabara ya Mtwara-Masasi-Tunduru-Namtumbo-Songea(Njombe-Makambako) ina lami kwa 98%. Hivyo visingizio hakuna tena. Hata hiyo 2% ambayo imebaki wakandarasi wanamalizia,wako site.

Kipande pekee ambacho kinahitaji Bajeti ni ile lami ya zamani kutoka Mtwara-Mnazi Mmoja-Masasi(km201),hiyo lami yake imechoka. Design Life ya miaka 20 imeshapita. Hivyo haiwezi kuhimili magari mazito, na hasa kipande cha Mnazi Mmoja hadi Masasi(km121)!
Kweli kabisa na madhara wanaomekana kwa kipande cha Mtwara hadi Lindi mle yanamopita malori yenye shehena ya saruji kutoka Dangote..kuna haja ya kuwa na lami yenye tabaka Nene kama Ile ya Namtumbo Songea.
 
Back
Top Bottom