Iziwari
Member
- Jun 5, 2021
- 76
- 56
Kumekuwa na ongezeko kubwa sana la wanawake wanao lea Watoto wenyewe katika jamii zetu. Sio kwamba ni sifa mbaya lahasha, bali ni moja ya mfumo unaoanza kuzoeleka na kufanywa kuwa kama ndio mfumo wa Maisha. Na nikisema wanalea wenyewe namaanisha bila kuwa na baba kama msimamizi.
Lengo kuu la kuandika kuhusu hili, ni kwa sababu tunahitaji suluhisho. Na suluhisho hili lina lengo la kama kupunguza au kuwezesha jambo hili kufanyika kwa njia ambayo haileti madhara katika jamii zetu.
Lakini kwanini tupunguze wanawake wanao lea Watoto wenyewe katika jamii zetu? au jambo hili ni kweli linaweza kuleta madhara kwa kipindi kijacho?
Na tunawezaje kupunguza swala hili au nini kifanyike?
Pia naweza kuuliza ni namna gani tunaweza kuinua mfumo wa kipato katika jamii zetu. Tukizingatia kuwa wakina dada hawa wanahitaji namna nzuri ya kujipatia kipato?
Maswali haya ndio ntajaribu kuyajibu kwa wale watakao endelea kusoma. Na hii ni kwasababu haya yote yana suluhisho rahisi sana kulinganisha na vile jinsi ulivokuwa unafikiria.
Kwa maana, wanawake wanao lea Watoto bila msaidizi katika jamii zetu ni wanawake wenye upendo na kujali Watoto wao sana.
Nimeshuhudia kwa wengi wakiwa wanapambana kujitengenezea kipato na wakiwa wanasomesha Watoto wao. Na kuhakikisha Watoto wanapata huduma na matibabu pale wanapopata tatizo lolote.
Wanawake hawa wakiwa katika hali ya kutafuta na kupambana Maisha. wamekutana na changamoto nyingi lakini wamekuwa wakitanguliza upendo kwa Watoto wao na kuzivuka changamoto.
Cha kwanza wanastahili pongezi na kwa kweli wanastahili sifa ya kuitwa Mama Afrika.
Umaskini umekuwa bado ni tatizo kubwa katika jamii zetu. Na tunakumbuka kuna Umaskini, ujinga, na maradhi. Kama maadui wakubwa watatu tunaopambana nao kwenye jamii zetu(J.k Nyerere).
Tukirudi kwenye mada kuu kwamba ni nini kifanyike ili kumkomboa mwanamke, mwenye jukumu la kulea Watoto wake bila msaidizi?
Tukianza na wanaume wanaoacha Watoto wao bila ya kujali wanaishije, na wanakuwa katika hali gani. Hili ni swala ambalo halimpendezi kabisa Mwenyezi Mungu. Na tukirudi kwenye swala la maadili hii ni picha kuu ya kuporomoka kwa maadili katika jamii zetu.
Na hii inapelekea hata Watoto wanaokuwa katika hali ya kumkosa baba, kuwa wapweke na kutaka kulipiza kisasi. Kitu ambacho kinaendelea kujenga jamii mbovu na yenye sifa mbaya.
Nini kifanyike kwanza kwa wakina baba?
Cha kwanza cha kufanya ni maandalizi. Maandalizi ya kuyapokea majukumu ambayo tayari yamesha kufikia.
Kumbuka Maisha hayapo ili kukimbia majumkumu. Bali Maisha yana mpa amani yule tu, ambae anajituma kuyatimiza majukumu yake.
Hakuna kinacho jificha apa, maana hata ulimwengu ukikupa nini cha kukufurahisha, kitaishia kuwa ni jukumu lingine lililoongezeka maishani mwako.
Mfano kuna mtu labla kafrahi sana kununua gari zuri kuliko mwenzake. Bila ya kujua kuwa gari linapoongezeka uzuri ndio pia na jukumu la kulitunza linaongezeka.
Kila kinachotokea maishani mwa mtu kama ni kitu kizuri sana. Iwe amepata udhamini wa Kwenda kusoma nje ya nchi au amepata safari ya Kwenda mbali. Yote haya ni majukumu na kama haupo tayari kuyafanya atayashindwa.
Hakuna jukumu baya au zuri.
Wakina baba naombeni mnisikilize hapa. Hakuna jukumu baya au zuri. Kila jukumu limewekwa mbele yako kwa sababu Mungu anajua unaliweza.
Sa nyingine majukumu tunajitakia wenyewe. Na hapa wengi wetu ndio wanaanza kukasirika na akati ni kweli.Mfano, kuna watu wawili, mmoja alienda kununua mbuzi na mwingine akaenda kununua kuku. Alienunua mbuzi alijua kila siku ni kuhakikisha mbuzi anatoka nje kula majani. Na alie nunua kuku alijua ni kuwafungulia watoke nje wajitaftie. Wote walikuwa sawa lakini tunajifunza , walikuwa na maamuzi tofauti ya kuchagua mifugo kulinganisha na kile walichokiona kinawafaa.
Na tukirudi kwenye mada, mfano huu unatufundisha kufanya maamuzi ndani ya uwezo wetu. Kila mmoja anaruhusiwa kufanya maamuzi. Lakini maamuzi yeyote yalio nje ya uwezo wetu yanafananishwa na kujitoa muhanga.
Ni kama Kwenda benki kukopa milioni mia moja bila ya kujua jinsi utakavoirudisha. Ni maamuzi mazuri lakini pia utakuwa umefanya kujitoa muhanga bila ya kupiga mahesabu.
Tukianza kujifunza kwa namna yeyote ile. Inabidi tujifunze namna ya kufanya maamuzi. Na sana sana wakina baba ndio nawazungumzia hapa.
Kumbuka kuna umaskini, ujinga na maradhi.
Ujinga ni chanzo kikuu cha umaskini. Tukubali au tukatae hii ndio kweli.
Tukirudi kwenye mada ya maamuzi, chochote kinachotokana na maamuzi yako, kinatakiwa kuwa na elimu ndani yake. Narudia tena, mfululizo wa maamuzi yako yanatakiwa kutokana na elimu ulionayo kuhusu kile unachotaka kukifanyia maamuzi.Mfano Mtu mwenye uwezo wa kufuga kuku na kufanikiwa, ni yule mwenye elimu yote na uzoefu wa kutosha kuhusu ufugaji wa kuku.
Tumeshaondoka kwenye karne ya kufanya maamuzi bila ya kufikiria. Na neno fikiri kabla ya kutenda ndio neno la karne hii ya 21 ishirini na moja.
Elimu ndio chanzo pekee cha kupambana na ujinga.
Sio kwamba nasema watu wasio na elimu wote ni wajinga, lahasha. Namanisha kuwa, kuna njia nyingi za kujifunza vitu sasahivi.
Mfano unataka kujua kuhusu elimu ya uzazi utaipata haraka sana. Iwe ni Hospitali au kiliniki iliopo karibu na wewe. Au mtandaoni.
Tusijitoe ufahamu, maana kuitafuta elimu kuhusu kitu chochote unachotaka. Utaipata mtandaoni. Hii ndio karne pekee ambayo kila mtu ni msomi.
Kwaio usifikiri nazungumzia wasomi wengine Zaidi yako. Kama unajua kusoma basi jifunze kusikiliza na kufanya maamuzi sahihi.
Wakina baba wanahitajika kujua moja kwa moja jukumu walilo nalo; kabla hawajafanya maamuzi ya kupata Watoto bila maandalizi sahihi.
Na wale wababa ambao tayari wapo kwenye majukumu ya Watoto bila elimu sahihi. Basi ni vizuri wakaanza kujifunza jinsi gani ya kupambana na hayo majukumu.
Lakini pia, sababu za wanawake kuwa single mother zipo nyingi. Tofauti na hii sababu ya wanaume kukimbia majukumu.
Na sababu zingine zote za ziada sintazitaja hapa.
Basi tuanze na njia ya kwanza.
Tunajua kuwa umaskini ni adui wa kwanza wa haki. Na umaskini ni adui mkorofi sana, ukitaka kupigana nae hadi kumshinda inahitaji nguvu ya ziada(Elimu).
Nikisema nguvu, Tukumbuke kuwa umoja ni nguvu.
Cha kwanza cha kufanya ni kutengeneza mifumo mingi na mizuri kwa ajili ya kusaidia Watoto. Kuwapa chakula, elimu, makazi na malazi. Tunafahamu vituo vya kulelea Watoto. Vimekuwepo kwa muda mrefu sana. Lakini vimekuwa kama sehemu ambazo za kujiuliza sana kabla ya mtu kumpeleka mtoto wake.Hasa kwa vijana wakike na wakiume wa miaka hii.
Na kwanini iwe ivo; Ni kutokana na jinsi ambavyo tumejitengenezea akilini mwetu. Hatuna elimu ya kutosha kuhusu vituo hivi. Sawa unaweza ukasema, Watoto wapo wengi, watatosha kwenye hivi vituo vilivyopo.
Au ukasema sintapenda mtoto wangu awepo kwenye vituo kama hivi. Na bado tutarudi kwenye swala zima la kutambua kitu kwa undani sio kwa hisia. Kwa sababu vituo hivi havipo kukusimanga kwamba wewe ni maskini. Bali vipo kukupunguzia jukumu kwa muda Fulani mpaka utakapo pata mwelekeo mzuri katika mapambano yako.
Ndio tunajua vituo hivi vya watoto, havipo vingi na pia vingine havina muonekano mzuri. Lakini izi ndio sehemu ambazo zikiboreshwa zitawasaidia sana wamama. Uboreshwaji wake uje na kauli mbiu mpya kwamba. Muhifadhi mtoto wako kwa kipindi Fulani mpaka utakapopata uwezo wa kumuendeleza mwenyewe.
Waliopo tayari kuanzisha hii wangewasaidia sana Watoto. Na wanaweza wakachangia mada hapo chini.
Kingine cha kufanya ili kuwakomboa wamama hawa.
Kutengeneza vituo vingi sana vya ujasiria mali. Mwanamke wa kiafrika anapata mafanikio yake pale ambapo anakuwa mjasiriamali. Kuna vikundi vingi vinajulikana vya kutengeneza sabuni, na vya ufugaji.
Lakini bado havijawa na mwendelezo mzuri kwa sababu watu bado hawafikirii kuviendeleza. Nikimaanisha sa nyingine vimekuwa vikundi vya kichoyo sana. Wamekuwa wakibania hela na kuchagua watu wao.
Kwaio kinachohitajika apa ni kuwa na vikundi vinavyoanzishwa na mashirika makubwa yenye pesa za kutosha. Maana watu ndio chanzo kikuu cha pesa, basi watu wapewe elimu ya kutumia wingi wao na umoja wao kama chanzo cha kujiongezea kipato.
Wazo linalohusu kupata mtaji ni wazo linalosumbua wajasiriamali wengi.Na ni Baada ya kupata elimu au wazo ndio unakuwa tayari kutafuta huo mtaji. Na Mtaji ni kweli unahitajika, maana lazima ,vifaa ,nauli , chakula mawasiliano, na mavazi vyote ni gharama hata kabla haujaanza kuchapa io kazi. Hii inapelekea watu kukata tamaa na kushindwa kuendelea katika mapambano yao ya kila siku. Vikundi vya kutoa mikopo vipo na tutaunga group moja la telegram kwa ajili ya wale wenye vituo vya Watoto na wale wenye vikundi vya kutoa mikopo. Yawezekana kila kitu kikawa kilishafanyiwa ufumbuzi sema watu wenyewe ndio hawana taarifa sahihi.Lakini nimekuja na taarifa sahihi kwamba unaweza ukaanza Maisha yako kwa upya tena kwa kupitia izo njia mbili nlizo shauri hapo.
Wengine mtaendelea kuchangia mawazo yenu baada ya haya yakwangu.
Angalizo.
hakikisha unatoa wazo la kusaidia.Maana Mungu amekupa akili kama zawadi na haujui imetoka wapi. Amekupa nguvu na uwezo wa kuiona leo kwa kusudi lake, ili na wewe uwe msaada kwa watu wote. Kwaio andika kitu chenye kuleta tija na kitakachofanya wakinamama hawa wapate suluhisho.
"you must forgive and forget for the sake of life".

Jinsi gani ya kumkomboa single mother.
Nikisema single mother namaanisha mwanamke mwenye jukumu la baba na mama katika familia.Basi tuanze na njia ya kwanza.

Kila mtu ana Wazo la kupata mtaji, nini kifanyike.