JamiiTalks

JF Advocacy Team
Aug 7, 2018
626
938
1687207671409.png

Dunia kwa sasa inapitia mapindizu makubwa ya kidijitali, watoto limekuwa miongoni mwa kundi muhimu ambalo linastahili kulindwa na kuongozwa katika suala zima la matumizi ya kidijitali.

Zaidi ya wadau mbalimbali kusisitiza umuhimu wa kuwalinda watoto katika wakati huu wa mapinduzi ya kidijitali, bado kuna changamotokubwa sana kwa kundi la watoto wenye ulemavu. Watoto hawa wanaonekana kuhitaji uangalizi maalumu ili kuwalinda na dunia ya kidijitali.

Je, unafikiri nini kifanyike kuwalinda Watoto wenye ulemavu katika dunia ya kidigitali?

Karibu katika Twitter Spaces ya JamiiForums siku ya tarehe 20 Juni, 2023 kuanzia saa 12:00 jioni mpaka saa 01:00 Jioni ili upate kuwasikiliza Wataalamu nawe upate wasaa wa kutoa maoni yako.

Kujiunga gusa linki hii hapa chini:


DKT. ISAAC MARO
Katika kazi tunazofanya tumekuwa tukiona Watoto wenye Ulemavu wakipata shida kuishi kwasababu nyingi ikiwa ni pamoja na dunia ya Kidigitali kutokuwa rafiki kwao Hivyo kwasasa tunaka kupata njia za kuweka mazingira yatakayokuwa rafiki kwa Watoto wenye Ulemavu

GODFREY KIMATY
Watoto wenye Ulemavu kwenye jamii yetu inachukuliwa kama Walemavu wa Viungo lakini Ulemavu unabebwa na nyanja pana. Kuna Ulemavu unaoonekana na usioonekaUlemavu unaoonekana ni pamoja na Ulemavu wa Viungo, lakini kimaana Ulemavu ni hali ya mwili kushindwa kutenda sawa

Tunapozungumzia Ulemavu kwa Watoto unaweza kutokana na vichocheo mbalimbali kama vile changamoto za Ujauzito ikiwemo kukosa virutubisho au madini joto ambayo husababisha mtoto kuzaliwa na ulemavu wa viungo.

Kuna ulemavu ambao unasababishwa na mazingira ikiwemo kupata shida wakati mzazi anajifungua ikiwemo kubanwa au kudondoka wakati wa kuzaliwa au wakati wa ukuaji wake

Aina nyingine ya Ulemavu inaweza kusababishwa na Magonjwa kama vile Malaria au kupata tatizo kwenye Mfumo wa Fahamu (Ubongo) ambapo aina hii huathiri moja kwa moja tabia za Mtoto

NOELAH MSUYA, Mkurugenzi Child Support
Watoto wenye ulemavu moja kwa moja wako hatarini kwa kuwa wao wanakuwa waathirika, inahitajika Watu wanaowazunguka Watoto hao kuhakikisha wanawalinda. Mfano, jinsi ambavyo tunatumia picha za Watoto wenye Ulemavu kutangaza shughuli zetu, wakati mwingine tunaweka picha ambayo inamuonesha Mtoto akiwa kwenye hali mbaya

Licha ya kutumia picha za Watoto wenye Matatizo ya Kiafya kwa nia njema, zile picha zinaweza kuja kutumika vibaya mbeleni.Yule mtoto akija kuwa mkubwa picha zinakuja kumuathiri au kuharibu maisha yake kabisa. Na hii ni hatari zaidi kwa Watoto ambao wana Ulemavu

DKT. ROMANA MALIKUSEMA (AFYA CHECK)
Tuko katika wakati ambao Wazazi tunadhani kumpa mtoto Simu ni kuonesha unamjali.Kuna vitu vingi ambavyo Watoto wanakuwa kwenye mazingira hatari, unakuwa na mtoto unampa simu bila kujua anaangalia nini

Sasa hivi kuna mitandao kama Tiktok inafanya 'Challenges' ambazo kama mzazi haufatilii hautajua mtoto anajifunza nini kulePia, kuna picha ambazo anakutana nazo nyingine zinakuwa si rafiki. Kuna wengine wakutana na unyanyasaji mtandaoni bila Wazazi kujua.

MHANDISI SHANGWE MGAYA (Living Together Autistic )
Mimi nimekuwa nikikutana na changamoto ninapotoka na mwanangu, kwasababu Watoto wenye Usonji hawaonekani kama wana UlemavuNatumia picha za mwanangu kwaajili ya kusaidia uelewa kwa Watu wasiojua. Wengine wanauliza mbona mtoto anaonekana yuko sawa, wapo wengi wana changamoto ya Usonji lakini wanaficha

GODFREY KIMATY
Katika kutoa taarifa za Watoto wenye Ulemavu inabidi kujikita katika kufanya tafiti na kuwa na taarifa sahihi pamoja na kuzingatia matumizi ya picha za za Watoto wenye Ulemavu. Kuna Watu wamekuwa wakifanya uchangishaji wa hisani katika kutafuta misaada ya Watoto na kutumia picha ambazo zina sura za wenye changamoto za ulemavu, hapo ndio kuna changamoto

Katika kuwalinda Watoto wenye Ulemavu, ni kuanzia pale Mtu mmoja mmoja jinsi anavyofikisha taarifa kuhusu Mtoto mwenye Ulemavu. Kama kuna Mtu anafikisha taarifa zinazohusu hali za Ulemavu kwa njia ya unyanyapaa hapo kunakuwa na tatizo la kutomlinda Mtoto mwenye hali hiyo

Unapompa mtoto kifaa cha kidigitali kinaweza kumuongezea mtoto hali ya hatari au kumpunguziaMfano mtoto mwenye 'Down Syndrome' anaweza kutumia vifaa vya kidigitali katika kuongeza ari ya kujifunza vitu lakini pia vitu anavyokutana navyo mtandaoni vinaweza kumsababishia unyanyasaji wa hali aliyonayo

NOELAH MSUYA (Mkurugenzi Child Support)
Vifaa vya Kidigitali havijampa nafasi Mtoto mwenye Ulemavu kujifunza vitu vingi. Mfano, vifaa vingi vimeundwa kwaajili ya watoto wasio na ulemavu na hata vile vichache vilivyoundwa kwaajili yao bado sio rafiki sana

Kwenye maisha ya kujifunza inabidi wanaotengeneza vifaa vya Kidigitali waunde vifaa ambavyo vinakuwa jumuishi ikiwemo kuwa na Kompyuta ambazo zina mfumo wa nukta nundu. Mfano, Watoto wenye Ulemavu wa 'Dyscalculia' kama ukimpa 'Calculator' anaweza kufanya hesabu na kuonesha uwezo. Mifumo yetu ya Elimu inaweka mkwamo kwa Watoto wenye Ulemavu.

'Dyscalculia' ni aina ya Ulemavu ambao huonekani, inaweza kuwa pamoja na kutokuwa na uwezo kufanya vizuri Hesabu. Mtoto mwenye tatizo hili akipewa Vifaa vya Kidigitali anaweza kufaulu vizuri hesabu.

KIMMITO A.K:
Tunapojaribu kuangalia masuala ya Kidigitali lazima kuwe na misingiHauwezi ukawazungumzia Watoto wenye Ulemavu kwa kuwaweka katika kundi moja. Bahati mbaya hapa nchini hakuna mtu ambaye ametengeneza 'App' ambayo ni ya kundi hili la Watoto wenye Ulemavu

Hizi Taasisi za Teknolojia ziambiwe vitu vinavyohitaji kwaajili ya Watoto wenye Ulemavu kwasababu wana uwezo wa kufanya hivyo

Ukweli ni kwamba kwa kiasi kikubwa hatuwazungumzii sana Watoto wenye Ulemavu na sijajua kwanini Watanzania wengi tunaamini ukiwa Mlemavu ndio mwisho wa maisha.

DKT. ROMANA MALIKUSEMA (AFYA CHECK)
Tuhakikishe Vifaa vya Kidigitali vinakuwa salama kwasababu unapotumia muda mwingi kwenye vifaa vya kidigitali unaweza kupata matatizo ya kiafyaKitaalamu inaelezwa kuwa Mtoto anatakiwa kutumia saa 2 tu katika siku akiwa anatazama 'Screen' ya kifaa cha kidigitali ili usijekupata matatizo kama vile Matatizo ya Afya ya Akili.

MHANDISI SHANGWE MGAYA (Living Together Autistic )
Mimi nashauri hawa Watoto wenye Ulemavu watengenezewe vifaa vya kumfuatilia (GPS Tracker). Mfano, mtoto wasioweza kuzungumza anakuwa hatariniTunaweza pia kuanza kutumia Vishkwambi (Tablets) kwaajili ya kuongeza ari ya kujifunza.

Kwenye hizi 'Tablets' mzazi anaweza kuweka mipaka ya matumizi na aina ya vitu ambavyo ataangalia pamoja na kujua vitu gani atajifunzaMimi njia nzuri ya kuanza kusaidia watoto wenye ulemavu ili waweze kujifunza na kushiriki katika dunia ya kidigitali, tunaweza kutumia 'tablets'.

SHEILA MCHAMBA
Jamii isitumie Watoto wenye Ulemavu kama chanzo cha kujipatia kipato, pia wazazi wasiwafiche Watoto kuhusu masuala ya kidigitali. Ni vema kuanza kuwafundisha katika ngazi ya familia kuliko kusubiri Mtoto akajifunze mambo mengi kwa njia ya mtandao.

GEOFFREY NKAMBI
Nimefanya kazi Marekani kulikuwa na Tablets ambazo zina vitu na picha ambazo zinamsaidia mtoto mwenye ulemavu kuweza kuwasiliana. Mfano, mtoto akitaka kula anaonesha picha ya chakulaKwa muda ambao nimefanya kazi katika mazingira ya Watoto wenye Ulemavu, nimegundua kwa Tanzania mfumo bado unawatambua zaidi wenye ulemavu wa kuonekana zaidi kuliko wenye ulemavu usionekana.

MICHAEL SALALI (DISABILITIES HOPE)

Ipo changamoto ya uelewa kuhusu matumizi ya Digitali, ukifanya utafiti utagundua kuna kundi dogo lililoingia kwenye Uwanja wa digitaliMfano kwa mwenye Ulemavu wa Macho, nikitaka kupima VVU nitapataje majibu, Kwanini kusiwe na vipimo ambavyo vinaweza kutoa sauti kwaajili ya kusaidia wenye shida hiyo?
 
Mada muhimu sana kwetu wazazi na walezi, nipo nanyi nimeshajiuna nafatilia ili npate vitu
 
Kutoa Elimu zaidi kupitia Social Media ili watumiaji wa Digitali wapate uelewa Mpana hii itasaidia kupunguza Mabezo/Attack za mtandaoni na watu wakielewa basi watawathamini na kuwaepusha na attack za mtandaoni
 
Mada Nzuri nasubiri Kujifunza zaidi ya kile ninachokielewa kwa upande wangu
 
Back
Top Bottom