Stories of Change - 2021 Competition

Hamid abdul

New Member
Aug 4, 2021
3
2
Maendeleo ni chachu ya kila mtanzania hapa nchini ikiwemo maendeleo kwenye nyanja mbalimbali za kiuchumi, biashara, utawala Bora, uwajibikaji, afya, haki za binaadamu, demokrasia na kadhalika.

UCHUMI NA BIASHARA TANZANIA.
Ni wazi kua uchumi wetu Tanzania ni uchumi wa kati kwa mujibu wa takwimu zilizofanyika mwaka 2020 , lakini kufikia hatua hio, sio kikomo cha watanzania kukuza uchumi wao ,kutokana na kwamba kuna mikakati mingi ikifanyika itapelekea kukua zaidi ya hapa tulipo sasa.

Awali ya hayo ni utekelezaji wa miradi mikubwa nchini mwetu , mfano mzuri ni mradi wa umeme katika bwawa la rufiji ambao ulibainika kutengeneza ajira za watanzania takribani 3500 ambao umeweza kuwaokoa kimaisha kwa kiasi flani, hivyo bas kupitia mradi huo na mengine Kama ya reli ya mwendo kasi basi Tanzania itafkia mahala pazuri kiuchumi na biashara.

Pili: Uboreshwaji wa miundombinu ya nchi ikiwemo barabara pamoja na majengo,kukiwa na barabara nzuri hapa nchini basi itapelekea urahisi na unafuu kwenye usafirishaji wa bidhaa kutoka nchini mwetu kwenda nchi jirani kwaajili ya biashara ,na kwa kupitia hivyo pato la taifa litaongezeka .

Tatu: Matumizi mazuri ya rasilimali za nchi pamoja na usmamizi katika rasilimali hizo, endapo rasilimali zitasmamiwa vizuri basi maendeleo ya nchi yataonekana kupitia rasilimali hizo.
Kwakufanya hayo na mengineyo mengi basi sekta ya uchumi na biashara itakua na kuleta maendeleo mazuri kwenye nchi yetu.

SEKTA YA AFYA TANZANIA.
Kwa kipindi hiki abacho Tanzania inakabiliwa na janga la UVIKO19 ambapo ni janga lililo gusa sehemu kubwa ya dunia ,lakini serikali imejitahidi kupambana na ugonjwa huo kwa njia mbalimbali ili kuboresha afya za wananchi wake.Hatua zilizo tumika ni pamoja na kuletwa kwa chanjo ya kuzuia ugonjwa huo na pia utoaji wa elimu kwa wananchi wake . Serikali kupitia viongozi wake wanachukua hatua mbalimbali kupambana ili kuboresha afya za watanzania walio wengi hapa nchini. (1) Utoaji wa elimu ya mara kwa mara juu ya kujikinga na maradhi mbalimbali Kama vile Ukimwi , malaria,kifua kikuu na magonjwa mengi ambayo yanasumbua afya za wananchi watanzania, kwa kupitia elimu hizo afya za watu wengi nchini zimeweza kuimarika kwa kiasi flani.

(2) Uboreshwaji na uwepo wa vituo vingi vya afya nchini,kwenye mikusanyiko ya watu wengi lazma serikali iweze kuweka vituo vya afya ambavyo vitakua vikisaidia kutatua maradhi hata yale madogo madogo , kwa kufanya hivyo wananchi wengi wataweza kuokoa maisha yao kwa kupata huduma nzuri kupitia vituo hivyo vya afya.

MAENDELEO YA JAMII TANZANIA.
Maendeleo katika jamii ni jukumu la kila mtanzania hapa nchini, uwepo wa huduma Bora za afya ,elimu , maji nakadhalika yote hayo ni maendeleo katika jamii . Katika maeneo mengi nchini jamii zake zimeendlea , hii ni kwa sababu kua huduma nyingi za maisha ya watanzania zinapatikana . Serikali imebaki kujikita zaidi kwenye kuboresha huduma hizo haswa kwenye huduma zenye uhitaji na watu wengi, hivyo basi serikali inatakiwa kutumia njia mbalimbali ambazo zitaweza kuongeza maendeleo katika jamii zetu .
Moja : Uwepo wa uangalizi na usimamizi katika utoaji huduma za kijamii , kupitia uongozi uliopo matatizo Kama ya utoaji rushwa na Matumizi mabaya ya madaraka yote yanatakiwa kuchukuliwa hatua na serikali.

Pili:Kushirikisha taasisi zisizo za kiserikali katika kutoa huduma hizi za kijamii ili tu kuleta maendeleo katika jamii, mfano mzuri utoaji wa elimu kupitia shule za binafsi ,pia utoaji wa huduma za kiafya kwa vituo binafsi, pia kwenye sekta ya usafiri magari mengi ni ya makampuni yasiyo ya serikali.Kwankufanya hivyo jamii zetu zitaendelea.

Tatu: Kupunguza vikwazo kwa taasisi binafsi ili Utoaji wa huduma za kijamii ziwe kwa wingi bila unyanyasaji. Serikali ikiweka mazingira mazuri kwa wawekezaji basi maendeleo katika jamii yatakua kwa wingi na pia itapunguza gharama ya serikali katika kutoa huduma hizo.

TANZANIA NA DEMOKRASIA.
Tanzania ni miongoni mwa nchi zinazo endeshwa kwa mfumo wa kidemokrasia , ambapo asilimia 90 ya demokrasia inatumika nchini katika shughuli mbalimbali za kiserikali.Uongozi wa nchi ukiongozwa na mheshmiwa raisi upo vyema kutekeleza na kusimamia demokrasia katika nchi. Hivyo basi serikali hiyo inapita kwenye mbalimbali ili kuhakikisha utekelezwaji wa demokrasia katika shughuli za kiseikali kwa kufwata misingi ifuatayo,
Moja: Kusmamia haki na usawa kwa kila mtanzania hususana usawa katika jinsia ,dini na kabila.Kwa kusimamia haki basi watanzania watafikia maendeleo yao bila unyanyasaji wala ubaguzi wa Aina yoyote.

Pili: Serikali inatakiwa ismamie uwazi na uwajibikaji wa viongozi katika madaraka yao ,uwepo wa uwazi katika shughuli za uongozi kutaimarsha demokrasia ya nchi yetu pamoja kuleta maendeleo kwa wananchi kwa ujumlaa.

Tatu: Serikali ismamie uhuru na usawa katika nyanja mbalimbali za kidini ,uchumi ma kisiasa . Uwepo wa uhuru kwa wananchi hususani vyombo vya habari kutapelekea uwazi kwa viongozi na maendeleo. Pia usawa kwa viongozi uwepo hasa kwenye siasa ,chama tawala na visivyo tawala vipewe usawa kulingana na nafasi zao.

Kwakufanya hayo serikali itakua imeboresha demokrasia yake na pia maendeleo yatakua yamesogea mbele kwa kiasi kikubwa.

SEKTA YA KILIMO TANZANIA.
Tanzania kupitia kilimo imeweza kujiinua kwa kiasi kubwa sana katika uchumi wake, hii inatokana na kwamba nusu ya pato la taifa linatokana na sekta ya kilimo. Ukiangalia pia bidhaa zinazotoka Tanzania robo tatu ya bidhaa hizo ni kutoka kwenye kilimo. Serikali kupitia sera ya kilimo kwanza iliweza kuboresha na kuinua maisha ya watanzania walio wengi Sana kwa kujipatia ajira na pia kuwaajiri wengineo, hivyo basi, serikali imekua ikichukua hatua mbalimbali ili kuwezesha sekta hii ya kilimo kufikia maendeleo ya nchi. Kwanza kabisa , serikali imejikita katika kutoa elimu juu ya mbinu Bora na mbadala kwa wakulima ili kuwawezesha waweze kutoa mazao yalio Bora kwa Matumizi ya wananchi wake na biashara .
Pili, serikali imejikita katika kuweka sawa miundombinu yake hususani barabara ambapo usafirishaji wa bidhaa za mazao kutoka mashambani kwenda kwa wanunuzi itakua rahisi na salama zaidi.
Tatu: Serikali imeweza kuruhusu taasisi binafsi kushiriki katika kutoa mchango wao kwenye maendeleo ya kilimo hapa nchini ikiwemo utoaji wa elimu na vifaa vya kufanyia kazi mashambani.
Hivyo basi serikali kupitia viongozi wake imeweza kufanyikisha yote hayo ili kuleta maendeleo katika jamii zetu za watanzania.

SAYANSI NA TEKNOLOJIA YA TANZANIA.
Tanzania katika sayansi na teknolojia bado tupo nyuma ,na hii inatokana na sababu mbalimbali ambazo serikali ipo mbioni kuzitatua changamoto hizo. Wizara ya sayansi na teknolojia nchini inatakiwa kuweka mikakati mbalimbali ambayo itainua sayansi na teknolojia ya Tanzania. Kwa kufuata yafuatayo serikali itaikwamua Tanzania kutoka kwenye Hali ya chini ya sayansi na teknoloji.
Moja: Serikali inatakiwa kuboresha mfumo wake wa elimu amabapo utaweza kutoa wahitimu wenye uwezo mzuri zaidi wa kugundua na kuboresha Hali ya sayansi na teknolojia hapa nchini.

Pili; serikali kupitia wizara ya sayansi na teknolojia itoe hamasa na elimu kwa wananchi juu ya umuhimu wa teknolojia na sayansi katika nyanja mbalimbali za kimaendeleo hapa nchini.

Tatu: serikali inatakiwa kutoa fursa mbalimbali kwa wananchi wake bila kujali jinsia wala ubaguzi wa Aina yoyote ule , kupitia hivyo tutaweza kukuza sayansi na teknolojia yetu hapa nchini.
Kwakufata hayo na mengne mengi tutaweza kujikwamua kisayansi na teknolojia na kupelekea maendeleo ya nchi.

HAKI ZA BINAADAMU.
Haki za binaadamu ni misingi ya maadili inayotakiwa kutumika kwa manufaa ya binaadamu wote duniani na kwa usawa.
Kuna mashirka mengi duniani yanayo jihusisha na ufuatiliaji na utetezi wa haki za kibinaadamu, hivyo basi serikali ya Tanzania nayo imechukua hatua mbalimbali katika kupambana na kutetea haki za binaadamu.
(1) Uwepo wa mashirika mbalimbali yanayo jihusisha na utetezi wa haki za binaadamu, miongoni mwa mashirika hayo ni LHRC ( legal and human right center) kituo cha sheria na haki za binaadamu. Kupitia taasisi kama hizi , haki za binaadamu zitakua salama kwa kila mtu.
(2) Serikali inatakiwa kutoa elimu juu ya haki za binaadamu, faida zake pamoja na utekelezaji wake kwa wananchi. Wananchi wanatakiwa kujua umuhimu na kupata elimu ya haki za binaadamu.
(3) Serikali inatakiwa kuweka adhabu kali na sheria kwa watu wote watakao kwenda kinyume na haki hizo za binaadamu. Hatua kali zichukuliwe ili iwe funzo na kwa wengne wenye kuenda kinyume na haki za binaadamu.
Kwa kufuata hayo na mengne mengi kutapelekea kulinda haki za binaadamu na pia kupelekea maendeleo ya nchi.

UTAWALA BORA NA UWAJIBIKAJI.
Utawala Bora ni Matumizi ya mamlaka ambayo yanakuwa na uwazi, uwajibikaji, ushirikishaji wa watu , ufanisi ,tija ,uadilifu, usawa na kufuata utawala wa sheria . Kukosekana kwa utawala Bora nchini ndio chanzo kikuu cha migogoro katika nchi , kunakua na migogoro ya kikatiba ,vita ya wenyew kwa wenyewe na migogoro mengine tofauti tofauti. Hivyo basi, uongozi wa nchi unatakiwa kuchukua hatua mbalimbali ili kuwezesha utawala Bora na uwajibikaji katika nchi kwa kufata misingi ifuatayo.
Moja; Serikali inatakiwa kuweka usmamizi makini sana kwenye kufuatilia Matumizi mazuri ya madaraka , vyombo vya dola na rasilimali kwa faida ya watu walio wengi.
Pili; Viongozi wanatakiwa kujua madaraka yao , Matumizi yake pamoja na mipaka iliyowekwa na katiba pamoja na sheria.

Kwa kufuata misingi hiyo na mingine kutakua nautawala Bora nchini na pia maendeleo endelevu ,utokomezaji wa umasikini , maradhi pamoja na ujinga .

AHSANTE KWA KUSOMA ANDIKO HILI , NAAMINI UMELIPENDA NA KULIELEWA ,BASI USISITE KUWEKA KURA YAKO HAPO CHINI.
 
Back
Top Bottom