The Farmer
JF-Expert Member
- Jan 7, 2009
- 1,658
- 559
Vile vile sii vibaya kama tutaorodhesha pia mambo muhimu ambayo tunapenda kuona mabadiliko ktk chama tawala yaani CCM ikiwa bado wanataka kupata support ya wananchi kwa sababu hadi leo hii inaonyesha wazi vyama vyote nchini - They don't get it!...Wanafikiria wananchi watahadaika vipi kuliko nini mahitaji yao kiasi kwamba Siasa nchi Tanzania zimekuwa ni Utapeli... Mwongo na mwenye kutoa ahadi kubwa kubwa ndiye huchukua mwali nyumbani..Sasa ni wakati wa wananchi kusema TUMECHOKA na ahadi, tumechoka na sura, tumechoka na mapambo ya vyeti..TUMECHOKA...
Enough is Enough!
Mkandara, SISIEMU imeoza! Tusitegemee mabadiliko ya aina yoyote ile ndani ya SISIEMU. Swala la UFISADI liko wazi na MAFISADI wanafahamika, kuna chochote kile kilichofanywa na Serikali ya SISIMU?? Swala la DOWANS, RICHMOND nk, linajulikana na walioisababishia nchi hasara kubwa kutokana na kampuni hizi wanajulikana lakini kuna yeyote yule aliyeshughulikiwa kikamilifu???
Ukija kwenye swala la IPTL nchi imekula hasara ya kutosha kabisa, nini kiliendelea au kinaendelea kwenye mchakato mzima wa kuwawajibisha waliosababisha hasara hii kubwa kwa Taifa?
Kwa kifupi tusitegemee mabadiliko yoyote yale ndani ya SISIEMU. Wakati wa mabadiliko umefika. "TANZANIA BILA YA CCM INAWEZEKANA"
- Hivi Zitto ni Chadema au CCM-Mtandao?
FMES!
Naona ishu kubwa inayotawala discussion humu ndani ni huu ufisadi. Kitu tunachokisahau ni watumishi wa umma (public servants) walivyooza Tz. Kwa mfano polisi, wizarani, nk.
Swali: Je hata kama CCM itaondolewa madarakani, upinzani utaweza kuboresha nchi na muozo uliopo ndani?
Labda tunasahau kuwa tatizo letu ni zaidi ya chama kinachoongoza. Maana upinzani hautaweza kuanza na timu mpya katika kila sekta. Na hivyo, watu hawa tutapambanaje nao?
Na kuipeleka serikali mahakamani ndo ujue utakufa ukisubiri haki yako.
Naona ishu kubwa inayotawala discussion humu ndani ni huu ufisadi. Kitu tunachokisahau ni watumishi wa umma (public servants) walivyooza Tz. Kwa mfano polisi, wizarani, nk.
Swali: Je hata kama CCM itaondolewa madarakani, upinzani utaweza kuboresha nchi na muozo uliopo ndani?
Labda tunasahau kuwa tatizo letu ni zaidi ya chama kinachoongoza. Maana upinzani hautaweza kuanza na timu mpya katika kila sekta. Na hivyo, watu hawa tutapambanaje nao?
Na kuipeleka serikali mahakamani ndo ujue utakufa ukisubiri haki yako.
Na unategemea itachukua muda gani kwa upinzani kubadilisha utendaji ndani ya serikali?
Sina uhakika serikali ina-employ watu wangapi, lakini nadhani inaweza ikawa karibia asilimia hamsini ya wafanyakazi wote nchini.
Njia moja ya kuboresha utendani ni kupunguza wafanyakazi. Na itapelekea kuwagusa hiyo asilimia 50 ya total work force. Upenzi (popularism) kwa upinzani kweli utaendelea hapo?
Tatizo la utendaji bora nadhani lilianza kwanzia enzi za ujamaa, ambapo sera ya serikali ilikuwa kutoa employment kwa watu wote. Na hivyo kutoa job security hata kama unaboronga kazini. Sasa kurekebisha hapo sio kitu cha siku moja.
Kurudisha integrity katika system nzima itachukua zaidi ya miaka mitano na hata kumi. Walimu kurudi mashuleni, Ma-profesa kufundisha kikweli, polisi kuwatii wananchi na sio kuwaonea, nk...
Pia ukumbuke, power is corruptive. Mpinzani na yeye anaweza kugoma kuondoka - eg: Kenya. Sasa hapo si tutakuwa tunazunguka mbuyu?
Mmmhhhhh!!! una uhakika na hilo? Mwalimu unashindwa kufundisha utasingizia uongozi? Lecturer unatoa marks za chupi kweli utasingizia uongozi? Wewe unachukua pesa kwa mafisadi ili wasilipe kodi TRA, kweli matatizo ni uongozi?Uzoefu unaonyesha kuwa watanzania ni wachapa kazi wazuri sana wakipata uongozi bora.
Sasa tuna uhakika gani kama wapinzani watakaokuja watakuwa viongozi bora?Uzoefu unaonyesha kuwa watanzania ni wachapa kazi wazuri sana wakipata uongozi bora.
Mmmhhhhh!!! una uhakika na hilo? Mwalimu unashindwa kufundisha utasingizia uongozi? Lecturer unatoa marks za chupi kweli utasingizia uongozi? Wewe unachukua pesa kwa mafisadi ili wasilipe kodi TRA, kweli matatizo ni uongozi?
Uongozi nakubali ni tatizo lakini pia sisi wote kama Watanzania tuna matatizo makubwa sana.
Unakuta watu mpaka kwenye nyumba zao ambako wao ni viongozi bado ni maguvu tu, kwenda kujichana nje huku familia inaumia na ujinga mwingine.
Sawa CCM ni tatizo lakini wanafanikiwa kuafanya hivyo kwasababu sisi pia wananchi tuna matatizo mengi sana kwenye utendaji na kuwajibika.
Uzoefu unaonyesha kuwa watanzania ni wachapa kazi wazuri sana wakipata uongozi bora.
Unajichanganya sana...... weka wazi point yako
My point is....IT'S NOT AS SIMPLE AS ABC. Kubadilisha utendaji nchini sio rahisi hata kidogo. Blame kubwa imewekwa juu ya CCM, lakini pia lazima ujiulize, CCM inamgusaje profesa wa chuo kikuu katika kuwafundisha wanafunzi?...and so forth....
Umeelewa? I suggest u shld re-read my post slowly.
Uzoefu unaonyesha kuwa watanzania ni wachapa kazi wazuri sana wakipata uongozi bora. Mfano mzuri mdogo ni makampuni/institution za serikali zinazo/zilizo binafsishwa. Ukiangalia utakuta sana sana wafanyakazi wapya wanaoletwa mle hawazidi kumi, na wengi wao ni kwenye management level. Pia wanaokuwa retrenched ni wachache sana (wezi na wazembe). Vivyo hivyo kwenye serikali kama chama chenye viongozi bora kikichukua nchi, ni wachache sana watakaoachishwa kazi (hiyo lazima maana kuna mizigo isiyobebeka), ila cha msingi ni kuhakikisha kila sekta inapata uongozi wenye discipline kutokea juu. Kukishakuwa na dira na ground rules, hii nchi hutaiamini ndio ile ilikuwa ikiteswa na CCM kivile.
Matatizo ya watanzania yanasababishwa na CCM. Nasita kumlaumu mwingine yeyote kwa uzembe na kutowajibika wakati pale juu pameoza. Watu wanaongozwa kwa mifano bwana. Usifikiri hawa dada dala tunaowalaumu kila siku kusimama ovyo barabarani na kuvunja sheria watakavyo bila kujali kwamba ni bahati mbaya. Mtu gari linamharibikia barabarani hajali kulisukuma pembeni anatengenezea hapo hapo tena bila hata ya kuwa na triangular reflector wala nini. Mama wajawazito kutukanwa na manesi hospitalini hadi watoto kufa kabla ya kuzaliwa, Au pale ardhi uko ofisini kwa mtu badala ya kukusikiliza anapiga soga kwenye simu unangoja saa nzima kisha anakuambia nenda urudi kesho. Wafanyakazi kufika ofisini saa 1 lakini wanaacha koti kwenye kiti siku nzima na mambo kama hayo. Yote ni mazao ya CCM. Watu wanajijali wao tu, hawana hata chembe ya kuwajali wenzao. Ndicho kikubwa CCM ilichojengea watu wake.
Ni kwa sababu pale juu hakuna mtu anayejali wenzake. Aliye pale juu yuko bize kwenye dili na Rostam. Na hawa watu wa chini wanalijua hilo, kwamba jamaa yuko bize anaiba. Mtu wa chini yake akimpelekea ishu ya wizi, yeye ndio eti ashupae nayo, ataanzia wapi? Na huku anajua akiipeleka popote anajishtaki mwenyewe, maana alipokuwa anasuka dili na Rostam aliwahusisha baadhi ya watendaji wake ambao sasa akitaka kumshughulikia huyu mwizi lazima pia awahusishe. Anaona haina tija hivyo anakaa kimya. Kesho huyu jamaa akiletewa kesi ingine kama hiyo wala hahangaiki tena kuipeleka mbele. Finally wezi wote wanashtukia kwamba kumbe hata ukiiba hakuna wa kukufanya lolote maana wote wezi. Basi kila mmoja kazi kuiba tu. Kuiba si lazima uwe ofisini. Hata kusimamisha gari liliokufa katikati ya barabara na kuwasimamisha wenye haraka zao bila sababu ni wizi. Nchi haiwezi kuendelea kama watu hawathamini muda wa wenzao. Watathamini je kama wanajua hata wasipofanya hivyo hakuna wa kuwachukulia hatua?
CCM imeondoa dhana ya uwajibikaji. Watu hawajali tena wenzao wala mambo ya umma. Ukiondoa CCM na kurestore hiyo hali mambo yatabadilika by far by fast.