Fisadi Mtoto
JF-Expert Member
- Jan 7, 2008
- 639
- 82
SIKATAI WALA SIKUBALI KUWA SYSTEM NDIO ILIVIANZISHA KWA KUWA USHAHIDI NI WA MAREHEMU AMBAYE SIJUI KAMA ALIMPA KAMA SEHEMU YA WOSIA AU ALIMWAMBIA KAMA MWANDANI WAKE.LAKINI SIJAONA MAHALI WALIITWA VIONGOZI WENGI WA UPINZANI IKULU NA MZEE MAGUTO KUITWA KWAKE HAKUMAANISHI KUWA VIONGOZI WOTE WALIITWA NA WALA HAKUMAANISHI KUWA KUITWA NI ZOEZI ENDELEVU ATA WALIOZALIWA JUZIJUZI MRADI NI UPINZANI WATAITWA KUPEWA MAELEKEZO.NA WALA HAIMAANISHI KUWA KAMA WALIWAANZISHA BADO WANAWENZA KUWACONTROL MPAKA SASA,NI KAMA VILE WALIANZISHA JAMBO WASILOWEZA KULICONTROL ANYMORE......HOWEVER,TATIZO KUBWA LA VYAMA VYA UPINZANI NI KUONGOZWA NA REJECTED MATERIALS YA CCM,GANDA LA MUA LA JANA CHUNGU KAONA KIVUNO.Mie sielewi point yako ipo wapi?Unamaanisha wananchi wasiviunge mkono vyama vya upinzani kwa sababu vyote vipo kwenye system?Je njia mbadala ni ipi?Kwa nini usianzishe chama chako kisicho kwenye system ili utuonyeshe mfano?
Wewe unachoongea ni utumbo mtupu, soma hoja vizuri. Au unaogopa ukweli? au unaona doooh, "kupigia debe kote kule upinzani lakini leo naambiwa ni system, haiwezekani!".Kuna watu wana mawazo ya kizandiki kuliko SISIEMU yenyewe.Watu hawa ni hatari kuliko systemu tupambanayo kwa sababu ni watu wa kujikomba kwa kila hali, hata kama faida yao ni kuchakaza soli za viatu na kukausha sauti za makoo yao kwa kushangilia upuuzi wenye kuwadharirisha utu wao wenyewe.
Kingine kibaya zaidi ni ving'ang'anizi wa hoja zisizo weza simama kwa miguu yake mpaka ziwe juu ya hoja nyingine za kufikirika.
Kuthibitisha jambo kutokana na source moja tena ya mtu ambaye ndoto yake ilikufa kabla haijaotwa ni Uzandiki na Uhabithi mkubwa na pengine ni kujikana utu wako mwenyewe.
Kuna watu wanajipendekeza kwenye System kana kwamba mwisho wa Uhuni wao wa kisiasa uko sambamba na kiama.Katika maana kwamba maovu ya SISIEMU ni kama Natural Principle( Gravitation Force, Magnetism and Density) ambazo ni ujuha kutaka kwenda kinyume nazo.
Wakati ni kweli kwamba kuna maofisa kibao Usalama wa SISIEMU ndani ya vyama vya upinzani;pia kwamba SISIEMU wanatumia fedha walizo iba BOT kununua na wapinzani na kudhoofisha juhudi zao, si kweli kwamba vyama hivi vimeundwa na SISIEMU au serikali ya SISIEMU. Sisi wengine tulikuwapo toka enzi za akina James Mapalala wakieneza propaganda za mageuzi kinyume na sheria za serikali ya SISIEMU tunajua kianachoendelea.
Ukiona mtu ambaye kalelewa ndani ya Thermos( Uniform Tempeture and Pressure) anasimama na kudhihaki mapambano ya halisi ya kujikomboa Kiuchumi na kifikra ili tu joto la Thermos inamuhifadhi lisibadirike, ujue ni dalili moja kubwa kwamba ameng'amua kwamba joto la maji ndani ya Thermos linapungua na maji yameanza geuka barafu. Hakuna Shwari, sasa anatapatapa.
Sishangai, utamaduni wa kusema uongo na kujidanganya ni hulka ya SISIEMU na wanachama wake wengi. Ndani ya miezi 12 iliyo pita SISIEMU na Vikaragosi wake wamejidanganya zaidi ya mara 1000 katika masuala kibao ambayo sasa hivi wanajaribu kujitoa kimaso maso kwa kupaka rangi Upumbavu wa makanusho yao kwa mafanikio haba au bila mafanikio kabisa.
Madai haya kwamba Upinzani Tanzania ni uongo mtupu yanaweza tolewa na mtu ambaye yuko kwenye kada ya juu ya SISIEMU, ni mtoto wa kiongozi wa SISIEMU, ni mke wa kiongozi wa SISIEMU au Kimada ambaye anafaidika moja kwa moja na Uharamia wa $133 Bill.
Lakini maneno haya kama yanasemwa na mwanachama mtiifu wa SISIEMU ambaye anaiona SISIEMU kwenye Fremu ya 1977, mwanachama huyu inabidi azinduliwe kutoka kwenye usingizi ulo mzito mithili ya ule wa pono na kuambiwa:
" Hi Mr Pono mkia wako umeshika moto unateketea, tena unateketezwa kwa moto wa hila za pono wenzako."
Ahsante kwa wazo lako zuri, ushahidi wa mwanzo:Mheshimiwa Ndugu Zomba, Nimesoma wakala wako si chini ya mara moja. Pia nimesoma mawazo ya wengine katika mada hii, Kadhalika nimepata kiasi cha muda wa kutafakari yote katika pande mbili za mjadala yaani upande wako na ule unaopingana nawe. Yangu ni machache tu kwako.
Siwezi kuyakubali wala kuyakataa yako kwa kuwa sina ushahidi. Na katika uliyoyazungumza sioni popote unapoyatolea ushahidi. Hali kadhalika siuoni ushahidi unaotoka kwao pia. Ili mradi, mtaniwia,
mnabishana kama wototo wadogo.
Mimi nafikiri, ungetoa maelezo yako, kisha ukayatolea ushahidi na kuyapa uzito maelezo hayo na mwisho ungetueleza nini cha kufanya ili tuweze kuupata huo upinzani/ushindani wa kisiasa. Labda cha ziada, kama itawezekana utueleze jinsi ya kuuendesha upinzani huo na labda utupe majina ya akina nani wanastahili kuwa viongozi wa upinzani huo.
Sisi wengine, pengine hatujui system ni nini na watu gani wamo au hawamo katika system yenyewe.
Ahsante kwa maswali yako.Mie sielewi point yako ipo wapi?Unamaanisha wananchi wasiviunge mkono vyama vya upinzani kwa sababu vyote vipo kwenye system?Je njia mbadala ni ipi?Kwa nini usianzishe chama chako kisicho kwenye system ili utuonyeshe mfano?
3) Ninayatowa haya kwa kuhofia yasitufike kama ya Kenya, kwani ni wengi walipomchaguwa Kibaki walijuwa kuwa ni mpinzani wa kweli, lakini masikini roho zao, damu inamwagika huko Kenya, simply kwa sababu Kibaki alikuwa kwenye system
Ama kweli asiyejuwa maana haambiwi maana, sijakisema vibaya chama chochote cha upinzani, usitie mameno yako katika mdomo wangu. Koma!Hebu tujadili mambo yenye mantiki na tuachane na huyu anayetutaka tuanze kujadili hisia bila kuwepo na ushahidi wa mazingira ama wa moja kwa moja.
Ukiangalia ushahidi wake utaona kuwa amejaribu kusema vibaya CUF na TLP ila vyama vingine hajavisema sasa asitufanye watoto wadogo.
Wako tayari kuutetea ufisadi kwani ndio unawafanya waishi........
Ama kweli asiyejuwa maana haambiwi maana, sijakisema vibaya chama chochote cha upinzani, usitie mameno yako katika mdomo wangu. Koma!
Nimesema viongozi wa upinzani na majina nimeyataja, soma vizuri kabla hujapayuka.
halafu mara sina ushahidi mara ushahidi wake, ndio tukuelewe vipi? au ni lazima useme tuu, hata kama hujuwi ukisemacho ni nini? au huijuwi system ni nini?
au huijuwi system ni nini?
Ninalijua Ri-jamaa hapa JF ambaye yuko radhi kuwanunulia viongozi wa CCM anything, lakini sio ndugu zake wala wazazi wake, Ri-jamaa litawanunulia hata watoto wao mizawadi isiyokuwa na mfano, litajipendekeza weee, mpaka kuwafuata viongozi kwenye majimbo yao ya uchaguzi na kujifanya lina NGO huko majuu, kumbe ni Ri-ongo likubwa na viongozi walishalishitukia, lakini hata uliambie nini ni kazi bure,
Ahsante Wakuu!
Ahsante, siwezi kujenga hoja kwa nisolo lijuwa, nimebainisha na kuweka wazi niliyoambiwa na mmoja wa hao watu aliyekuwa kwenye system.Kama tungejivunza kujenga hoja zetu kimantiki na kutumia evidence kidogo ingetusaidia sana. Tatizo moja kubwa tulilonalo kama taifa ni kwamba watanzania mara nyingi tumekuwa wepesi sana kukubali propaganda. Sasa kwa mfano kwa kuwa huyu ndugu yetu aliambiwa na mzee Kassim Maguto, basi imekuwa kweli as if huyu mzee alikuwa na uwezo wa kusoma yaliyomo nyoyoni mwa hao viongozi wa upinzani bila hata kutafakari kidogo lengo la Maguto kusema hivyo lilikuwa ni nini. Hivi, kwa mfano, leo ukienda kuongea na Tambwe kuhusu CUF au upinzani kwa ujumla unategemea kusikia nini zaidi ya kashfa na matusi lukuki dhidi ya upinzani?
Sasa mkuu, ungekuja na argument strong kidogo, lakini hii ya kuanzisha thread nzima on such a big topic kwa kutumia maneno uliyoyasikia kwa mzee Maguto kidogo ni below the standard of this forum.
Tufike mahala pia tuache kuwaweka wapinzani wote katika kapu moja. Tusiwe kama wazungu wanaofikiri Afrika yote ni moja, wakiona wanyarwanda wanauana basi wanajua ndio wafrika wote walivyo. Sasa vyama vya upinzani vipo zaidi ya 15 so far na inawezekana kesho kikazaliwa kingine. Tuwe very specific, ni chama gani tunaongelea. Tuachane na hii tabia ya kusema jumlajumla wapinzani, hii haitusaidii sana kwa sababu hata CHAUSITA, NLD, pia ni vyama vya upinzani.
Nakumbuka Mwalimu aliwahi kusema kuwa upinzani wa kweli utatokea ndani ya CCM, sasa sijui ndio alikuwa anatuandaa tukiona watu wanatoka CCM kuanzisha chama kingine tuone huo ndio upinzani wenyewe haswa na wale ambao hawakuwa CCM(ila enzi za chama kimoja sidhani kama kuna watu ambao hawakuwa CCM) wakianzisha vyama tuwaone si wapinzani wa kweli bali wababaishaji tu.
Sasa kama hiyo ni kweli je nitakosea kuhitimisha kuwa Mwalimu alikusudia CCM iendelee kuongoza nchi daima dumu?
Mie nadhani nyie ndio hamjitambuwi na wala hamuelewi mambo yanakwendaje, mnayatazama kijujuu tuu. Kama nyinyi ndio wapinzani wenyewe, basi kazi ipo kweli kweli, si leo wala si kesho, kwa sababu hata ninachokisema hamkijuwi wala hakiwaingii hata kidogo, lakini kwa kuwa tupo kwenye gari moja, haya twendeni tutafika tuu, iwe leo iwe kesho, Je huijuwi system ni nini?Kitila thanks kwa kumwelimisha huyu jamaa kwani hajitambui na pia hajijui bila shaka ........
Dotori, hiyo unayosema inaweza ikawa ni kweli kabisa na pia inawezekana kuwa viongozi wengine wapo kwa kuwa wamekula kiapo cha system, mpaka waondoke hao na waje ambao hawajalishwa kiapo, ndipo tutakapoona upinzani wa kweli. Jee huijuwi sysytem ni nini?Mtazamo wangu: Kwa sasa upinzani bado ni mchanga mno. Upinzani wa kweli utatokea pale chama tawala kitapomeguka na baada ya hapo itachukua miaka kama kumi ya kupata upinzani wa kweli.
Kinachoondelea sasa hivi ni kwamba walio wengi ni wapinzani kwa maslahi binafsi.