Nini hatma ya TCU baada ya kauli ya Rais Magufuli?

Nini hatma ya TCU baada ya kauli ya Rais Magufuli?

Kimsingi Rais hajaifuta TCU,alichosema TCU ibaki na majukumu ya Regulation kwa Elimu ya juu na kuacha swala la Udahili wa pamoja (CAS)
Kwa maagizo hayo system ya Central admission wenda ikafutwa badae na kila mwanafunzi aombe udahili direct chuo husika anachokipenda.

Rejea nukuu hizi;
Mmbea wa jiji:
'Wanafunzi wanalazimishwa kupelekwa kwenye kachuo ambako hakana hata jina'- JPM [HASHTAG]#UzinduziHOSTELUDSM[/HASHTAG]

'Niombe Wizara ya elimu, TCU tubadilishe utaratibu wa kuchagua wanafunzi, wanafunzi wenyewe wachague badala ya TCU'-JPM [HASHTAG]#UzinduziHOSTELUDSM[/HASHTAG]

'Wakati mwingine wakuu wa vyuo wanaenda TCU kuomba wapangiwe wanafunzi pamoja na kwamba sina ushahidi'-JPM [HASHTAG]#UzinduziHOSTELUDSM[/HASHTAG]

Rais Magufuli: Ishu si kuwa na vyuo vikuu vingi, ishu ni kuwa na vyuo vichache vinavyotoa wanafunzi wengi wenye vigezo vya juu [HASHTAG]#JFLeo[/HASHTAG]

'Wanafunzi wachague vyuo wanavyovitaka ambavyo havitachaguliwa vife, kwa nini mnalazimisha'-JPM [HASHTAG]#UzinduziHOSTELUDSM[/HASHTAG]

'Kuna vyuo ambavyo haviko kwenye Standard vina hakikisha vinapata wanafunzi kwa sababu wanapata mkopo'-JPM [HASHTAG]#UzinduziHOSTELUDSM[/HASHTAG]
Kimsingi ninaungana na Rais,tcu ni rushwa tupu kupitia vyuo binafsi ili wapate mikopo kupitia wanafunzi
 
Naungana kabisa na JPM...kwanini mtu alazimishwe kusoma asichotaka katika chuo kisichokuwepo?
Simpendi huyu baba ila kwa jana kidogo kwenye hili ameongea kitu. Wadogo zetu wanapata shida mtu kipato chako kidogo mara unajikuta umepelekwa chuo ada kubwa balaa. Bora iwe kama zamani tulivyosoma sisi. Chuo wachagua mwenyewe chuo kinadahili hawa TCU walikuwa wanakula hela tu na system zao zero ikizingua kidogo umekosa chuo. Ila we sizonje bado nchi imekuelemea ......hospital hazina madawa kila kitu mtu unalipia
 
Central admision system isifutwe bal ifanyiwe marekebisho tu.

Tukiiondoa bas wanafunzi wengi watakosa chuo na procedure itakuwa ndefu bcz kuna ambao watapata chuo zaid ya kimoja huku wengine wakikosa.

Rais umekosea.
 
Nadhani rais katika ili amepotoka, amepotoshwa na amepotosha tena kwa makusudi kabisa, kwa sababu zifuatazo....

1/Mfumo wa udahili wa Central Admission System(CAS) ilifanyiwa utafiti kwanza na mwisho ukapendekezwa kutumiwa na TCU ili kurahisicha udahili wa wanafunzi wa Chuo kikuu.

2/Mfumo wa CAS uliongeza ufanisi sana na kuondoa matatizo ya udahili ambayo yalijitokeza miaka ya nyuma baada ya watahiniwa kuongezeka na vyuo kuongezeka.

3/Kwa idadi ya vyuo tulivyonavyo Tanzania kwa sasa na uwingi wa waombaji wa vyuo, hakuna namna yoyote unaweza kufanikiwa bila kutumia CAS, na hakuna chombo imara na cha uhakika kinachoweza kusimamia CAS tofauti na TCU.

4/Japokuwa mfumo wa CAS nao umeonyesha mapungufu fulani wakati wa kuutumia, lakini matatizo mengi yalitokana na waombaji kushindwa kuutumia vyema huo mfumo wa CAS, na yote hayo ni kutokana na uelewa mdogo sana kuhusu kozi zinazotolewa na vyuo vikuu miongoni mwa waombaji.

5/Mfumo wa CAS ilikuwa unajiendesha mwenyewe automatically huku TCU ikiuratibu(Programming) na kuusimamia(Monitoring) na sio matakwa ya mtu mmoja mmoja. Na huu ndio ubora wa mfumo huo.

6/Sio kweli na wala sio sahihi kabisa kwa serikali(Rais) kuviona vyuo binafsi kama vitaasisi vya elimu vya ovyo ovyo na huku akiona vyuo vya serikali kama UDSM, SUA na UDOM kama vyuo bora vya Elimu. Ukweli ni kwamba ujio wa vyuo vikuu binafsi ndio ulioleta mapinduzi makubwa ya Elimu ya juu katika kuleta ushindani, kuongeza wahitimu na Tafiti.

7/Kuruhusu kwa mfumo wa zamani wa kila chuo kudahili watahiniwa wake binafsi bila kupitia mfumo wa uratibu wa TCU kutazaa mambo haya

-Baadhi ya waombaji kukosa vyuo(maana unaruhusu mlulindikano wa watahiniwa wengi kuomba chuo kimoja, na watakaokosa hicho chuo hawatakuwa na nafasi kusoma chuo kingine kama waliomba chuo kimoja tu)
-Muombaji mmoja anaweza kupata udahili kwenye vyuo viwili au zaidi na kumnyima nafasi muombaji mwingine(Multiple admission complications)
-Usumbufu kwa waombaji kwa kuwa itawahitaji kuwasiliana na chuo kimoja kimoja ili kuomba nafasi.
-Sarakasi za Rushwa, Upendeleo na kujuana zitaibuka upya vyuoni(Maana kila chuo kitakuwa na Mamlaka ya mwisho ya kumdahili mtu)
-Ucheleweshaji wa kupata mikopo (Maana itahitaji kila chuo kukamilisha zoezi la udahili na kila mwanafunzi kukamilisha usajiri kwenye chuo chake ndio mkopo utumwe)

-Kupotea kwa standard za udahili wa wanafunzi(Kila chuo kitatengeneza utaratibu wake wa kudahili wanafunzi wake)
Imesimama 100%
 
Kuna jambo ambalo wengi hatulielewi. TCU hawampangii mtu course (hili si kweli), TCU wanakupangia kutokana na ulichoomba. Shida iliyopo ni competition kubwa.

Unapoomba kozi flani pamoja na watu wengine 1000 wakati capacity ya chuo ni 70 hutapata. TCU kwa kutambua ndoto ya wengi ni kusoma chuo, wanaangalia wapi demand ilikuwa ndogo na qualification zako zimetimia wanakupangia. Its a matter of stay (wakuache) au go for your dream (walau utimize ndoto ya kusoma chuo).

Mpango unaopendekezwa una athari nyingi ambazo watu hawazioni. Ntaanisha chache;

1. Direct application kwenda chuo itaongeza gharama maradufu kwa maana kila chuo utalazimika kulipa application fees, gharama za stationeries etc.

2. Mfumo huu utapelekea watu wengi kukosa fursa ya kusoma elimu ya juu. Mathalani wote wakaomba UDSM, ARU, SUA na UDOM, kitakachotokea mwenye highest qualifications aweza kupata admission vyuo vyote akaziba nafasi za wengine.

Pili kwa kuwa application hufanyika baada ya matokeo ya F6 na muda mdogo kabla ya kufungua chuo, ni wazi atakaekosa vyuo labda vitatu ulivyoomba utachelewa kujua wapi kuna nafasi ukaombe hivyo mwaka huo kukupita na kukuacha mtaani.

3. Mfumo unaopendekezwa utawaacha watoto wa masikini wengi nje ( mfumo huu unaruhusu kupachikana kirahisi kwani kila mtu awe za kuja na majina ya nduguze chuoni kwake). Sambamba na hili la kupachikana kuna tatizo jingine la fedha, ni kweli kwamba bodi ya mikopo eitha haipeleki au huchelewesha kulipa ada za wenye mikopo, kutatua hili vyuo vinaweza kuopt kuchagua wanaojiweza kiuchumi wengi na kuwatupa nje watoto wa walalahoi wengi.

4. Tutatengeneza tatizo kubwa mbeleni la typology ya wanafunzi. Pamoja na TCU kuwa na matatizo wamejitahidi sana kubalance sana diversity ya wanafunzi vyuoni. Athari za direct entry zinaweza kuleta ukabila, chuo flani kimejaza nshomile wengi au wachaga wengi n.k (hii sio tuhuma mpya). Kuna jingine la udini, mathalani SAUT na associates wake wanaweza kujaza wakatoliki chuoni au MUM wakajaza radical islamist watupu na vyuo vingine n.k

5. Quality assurance itakuwa ngumu sana. Nilitegemea TCU waongezewe nguvu ya kuamua kuhusu ubora ikiwa ni pamoja na kupewa mamlaka ya kuamua entry qualification ili kulinda ubora wa vyuo vyetu. Tunarudi kule kule kwenye kila chuo kujiamulia sifa zake, vyuo vidogo na visivyo fahamika vitalazimika kushusha entry qualifications ili kufetch wanafunzi waliobaki (wenye sifa dhaifu) ili kuendelea kuwapo.

Rais ashauliwe vema kuhusu sera au kauli zake kuhusu elimu. Mara zote anapokuwa Mlimani ameonesha waziwazi kupendelea chuo hicho na kuviacha vyuo vingine kama vile si vya serikali au havina umuhimu. Leo inataka kuanzishwa sera ya ajabu ili kuipa UDSM autonomous ya kujiamulia mambo yenyewe, si sera mbaya ila vipi kuhusu vyuo vingine?

Hostels UDSM, Mabasi UDSM vipi wengine hawahitaji mambo hayo? Kwa nini tusiwe na treatment moja kwenye taasisi za elimu ya juu zote?
Mkuu Ushauri Wako ni Mzuri mno mno mno, Labda nikolezee tu hapo Hao Wanaolilia TCU ifutwe Labda Tu wapo vizuri Financial kuna Vyuo vitaangalia Background ya Mwanafunzi kams atakuwa willing kulipa mkwanja hata mkopo ukichelewa Au Usipokuwepo Wata dahiri kwa Matabaka mpaka TCU ikumbukwe, Kwa Wanaojiweza Kifedha TCU sio inshu kabisa ni Karaha kwao Wanakosa chance kusoma Top universities ila kwa wenzangu wa mabonde kuinama chonde chonde kuna vyuo mtavisikia kwenye bomba tu, Pesa na Connection kwanza Qualifications Kali baadae uko
 
Mkuu yupo sawa kabisa...watu tunatemwa vyuo vyenye hadh tukiwa na point pendekezi..kwa mfano Nina one naomba udsm natemwa DUCE vivyohivyo afu naenda Kutupwa private..kuna haja ya kuliweka sawa hilo..
 
Mm ningemshauri rais asifanye hivyo Bali vyuo vyote vikae kwaa ajili ya maboresho.
Mfano wakati wa udahili basi vyuo viwe vinashirikishwa kwenye uhakiki wa cut off points.
CAS ni njia bora zaidi inahitaji tu maboresho
Vyuo vinashirikishwa hata sasa, tatizo hawatoi data zinazo onyesha mtu amechaguliwa kwa misingi gani na aliepata selection ya mwisho anapoint ngapi ili alie achwa ajiridhishe kwamba point zake kweli hazikutimia. Kwa ufahamu wangu ni UDSM pekeee wanafanya hili. Hata TCU wangekuwa wanatoa taarifa kwa nini mtu hajachaguliwa au watoe cut off za kila degree kwa kila chuo baada ya selection kwisha watu wajionee wenyewe. Dawa ni kuboresha na sio kuiondoa.
 
kwakweki kitendo cha tcu kunipeleka st.joseph wakati nilichagua dit, must, udsm kilinifanya niahirishe fursa ya kusoma mwaka 2013. Wanaharibu mipango ya wanafunzi kwa faida yao. I swear hakuna mwanafunzi anaejielewa ataenda chuo kama DMI ST.JOSEPH
We jamaa bna sijui nkikuita kilaza ntakuwa nimekosea sasa Mpaka unakosa Admission Dit, MUST au UD si ni kwamba mapafu yako Hayawezi huo mkiki kama unajielewa ungepasua Poa Ukaingia popote
 
ttzo la bwana yule maneno yake na vitendo vyake vinapishana
 
TCU sitaisahau kwanza mlolongo mrefu sana.

Wakati unaweza ukaenda direct chuoni ukachukua form ukaijaza. Ukaenda bank ukalipa ada ya udahili na ukajua kabisa umepata chuo.
 
TCU sitaisahau kwanza mlolongo mrefu sana.

Wakati unaweza ukaenda direct chuoni ukachukua form ukaijaza. Ukaenda bank ukalipa ada ya udahili na ukajua kabisa umepata chuo.

Nani kakuambia kuwa chuo unapata kirahisi hivyo. Waulize wenzio wanaopply nje ya nchi au masters Tanzania. Kuna vigezo na masharti lazima vizingatiwe.
 
We jamaa bna sijui nkikuita kilaza ntakuwa nimekosea sasa Mpaka unakosa Admission Dit, MUST au UD si ni kwamba mapafu yako Hayawezi huo mkiki kama unajielewa ungepasua Poa Ukaingia popote
mkuu mi sii kwamba ni kilaza hapana nilikotoka na diploma nilikuwa na gpa ya 4.0/5.0 shida inakuja pale tulipofika chuoni wale wa diploma wote story ni moja yaan kila aliyejaza st.joseph hata kama ilikuwa ni last choice alipelekwa pale. Na hii ilikiwa ni dili kati ka tcu na chuo na hilo lipo wazi kabisa
 
Hata mwenyewe nilikuwa sipendi TCU kupangia watu chuo yaani ni sawa na TCRA akupangie utumie mtandao gani kwa matumiziyako binafsi,ni kama EWURA akwambie uwe unanunua mafuta ya BGP tu,Nakubaliana na Mh. JPM,TCU wawe regulator tu.

Kuhusu swala la kuchagua chuo,ningeshauri formu moja iwe na First Choice,second choice na third choice yaani hakuna ulazima wa mwanafunzi ku-apply vyuo zaidi ya kimoja kwa kujilinda just incase hakikosa hiko chuo kimoja,Form moja iwe na Choices tatu za vyuo ili akikosa cha kwenye form zipelekwe Chuo kingine etc.
 
Kwa hili Mh Rais Jpm yuko Sawa kabisa. Kitendo cha TCU kuwachagulia wanafunzi vyuo .
 
Kwa hili Mh Rais Jpm yuko Sawa kabisa. Kitendo cha TCU kuwachagulia wanafunzi vyuo .
Ni kweli ndio maana sie tunahosimamia ukweli Rais akifanya jambo zuri tunasifia maana hatuendeshwi na mihemko bali Facts,Hawa ccm jambo zuri akifanya mpinzani lazima wataponda mwanzo mwisho kisa amefanya mpinzani.
 
Naunga mkono hoja.mimi mwenyewe TCU ilinifanyia vibaya mwaka 2010. ilinipeleka pasipo tarajia .....JPM ungekuwa raisi 2005 haya yangenipitia mbali.....hapo kwa kauli hiyo nakuuunga mkono.....
 
Kuna jambo ambalo wengi hatulielewi. TCU hawampangii mtu course (hili si kweli), TCU wanakupangia kutokana na ulichoomba. Shida iliyopo ni competition kubwa.

Unapoomba kozi flani pamoja na watu wengine 1000 wakati capacity ya chuo ni 70 hutapata. TCU kwa kutambua ndoto ya wengi ni kusoma chuo, wanaangalia wapi demand ilikuwa ndogo na qualification zako zimetimia wanakupangia. Its a matter of stay (wakuache) au go for your dream (walau utimize ndoto ya kusoma chuo).

Mpango unaopendekezwa una athari nyingi ambazo watu hawazioni. Ntaanisha chache;

1. Direct application kwenda chuo itaongeza gharama maradufu kwa maana kila chuo utalazimika kulipa application fees, gharama za stationeries etc.

2. Mfumo huu utapelekea watu wengi kukosa fursa ya kusoma elimu ya juu. Mathalani wote wakaomba UDSM, ARU, SUA na UDOM, kitakachotokea mwenye highest qualifications aweza kupata admission vyuo vyote akaziba nafasi za wengine.

Pili kwa kuwa application hufanyika baada ya matokeo ya F6 na muda mdogo kabla ya kufungua chuo, ni wazi atakaekosa vyuo labda vitatu ulivyoomba utachelewa kujua wapi kuna nafasi ukaombe hivyo mwaka huo kukupita na kukuacha mtaani.

3. Mfumo unaopendekezwa utawaacha watoto wa masikini wengi nje ( mfumo huu unaruhusu kupachikana kirahisi kwani kila mtu awe za kuja na majina ya nduguze chuoni kwake). Sambamba na hili la kupachikana kuna tatizo jingine la fedha, ni kweli kwamba bodi ya mikopo eitha haipeleki au huchelewesha kulipa ada za wenye mikopo, kutatua hili vyuo vinaweza kuopt kuchagua wanaojiweza kiuchumi wengi na kuwatupa nje watoto wa walalahoi wengi.

4. Tutatengeneza tatizo kubwa mbeleni la typology ya wanafunzi. Pamoja na TCU kuwa na matatizo wamejitahidi sana kubalance sana diversity ya wanafunzi vyuoni. Athari za direct entry zinaweza kuleta ukabila, chuo flani kimejaza nshomile wengi au wachaga wengi n.k (hii sio tuhuma mpya). Kuna jingine la udini, mathalani SAUT na associates wake wanaweza kujaza wakatoliki chuoni au MUM wakajaza radical islamist watupu na vyuo vingine n.k

5. Quality assurance itakuwa ngumu sana. Nilitegemea TCU waongezewe nguvu ya kuamua kuhusu ubora ikiwa ni pamoja na kupewa mamlaka ya kuamua entry qualification ili kulinda ubora wa vyuo vyetu. Tunarudi kule kule kwenye kila chuo kujiamulia sifa zake, vyuo vidogo na visivyo fahamika vitalazimika kushusha entry qualifications ili kufetch wanafunzi waliobaki (wenye sifa dhaifu) ili kuendelea kuwapo.

Rais ashauliwe vema kuhusu sera au kauli zake kuhusu elimu. Mara zote anapokuwa Mlimani ameonesha waziwazi kupendelea chuo hicho na kuviacha vyuo vingine kama vile si vya serikali au havina umuhimu. Leo inataka kuanzishwa sera ya ajabu ili kuipa UDSM autonomous ya kujiamulia mambo yenyewe, si sera mbaya ila vipi kuhusu vyuo vingine?

Hostels UDSM, Mabasi UDSM vipi wengine hawahitaji mambo hayo? Kwa nini tusiwe na treatment moja kwenye taasisi za elimu ya juu zote?
Hao TCU ni wapuuz tu mfano mi dogo alichaguliwa kusoma architecture must kufika kule chuo wanasema hana sifa za kusoma hiyo koz japo alikuwa na vigezo maana kasomea science A level pcm
 
Back
Top Bottom