Nini hatma ya ndoa hii? Naombeni ushauri urgent

Nini hatma ya ndoa hii? Naombeni ushauri urgent

Wasalam wana Jamvi!

Ni matumaini yangu kuwa mu wazima wa afya tukimalizia weekend yetu murua kabisa!!

Niweke mada mezani bila kupoteza muda!

Siku ya leo nimefanya kitendo ambacho sikuwahi kufikiria kukifanya katika maisha yangu. Tumepishana kauli na mke, sasa huwa nikiwa na hasira nina desturi ya kukaa kimya na kuondoka, na Mara zote huwa naepusha ugomvi kwa namna hiyo, ndugu zetu akina mama wamejaliwa kuongea sana tofauti na sisi wanaume, hasa mimi yaani sipendi kelele kabisa kama kuna issue tusemeshane taratibu tuongee tumalize sio kelele

Ilikuwa majira ya saa mbili na nusu asubuhi ya leo, wakati tumetoka tu kanisani ibada ya Alfajiri.

Issue ni ndogo sana, mimi naandaa nguo zangu kwa ajili ya safari yangu siku ya kesho, sasa kuna baadhi ya mashati yangu aliyatunzaga kabatini nikawa namwagiza anipatie, kidogo majibu yake hayakuwa mazuri ukizingatia ni mke wangu sio hawara, na mimi alivyonijibu ilikuwa kwa dharau flani au anamjibu mdogo wake au mtoto kiukweli sikupendezwa, nikamuuliza unamfanyia nani hayo? Ikaanza kelele wewe, nikamwambia sikuelewi !! Ahaa bhana niache huwezi kuchukuaa mwenyewe, nikawa mpole nikamwambia sipendi kelele inatosha, ikaanza mada nyingine ambayo haihusiani, kuhusu maswala ya fedha na aseti ikawa kelele zaidi nikamwambia haya nimekuelewa inatosha, ehee mwenzangu hanisikii wala haelewi, nikamwambia basi toka chumbani mimi sitaki sharii, ahaa sitokiii!! Kelele ikawa kubwa sana!! Nikashindwa kujizuia kiukweli nikampiga! Tangu hiyo asubuhi hatujasemeshana kabisa, wala kumwona sijamwona, maana nyumba ina vyumba vingi vingine siwezi ingiwa sababu ni vya wasaidizi wetu wa kike !! Ila naisikia sauti humu humu ndani!!

Baada ya hayo kutokea nikaenda kwenye mizunguko yangu nikarudi saa Tisa, aliyenitengea chakula ni shemj yangu yaani mdogo wake wa kiume ambaye pia tunaishi naye hapa!!

Jionii hii pia chakula nimekula na huyo shemj yangu yeye sijamwona!!

Sijui pia hali yake ikoje mpaka sasa!

Naombeni ushauri juu ya-:

1) Nimwombe msamaha kwa kitendo hicho?

2) Au nikae tu kimya ?

3) Kesho nisafiri kama nilivyopanga ?

4)Na ushauri mwingine wowote nipo tayari kuupokea!!

Nawasilisha karibuni kwa ushauri na michango mbalimbali!!

Hata kama kosa ni lake ila sasa wewe ndo mwenye makosa. Hupaswi kumpiga mtu ( mke). Tujifunze kucontrol hasira na kupunguza mfumo dume. Ulivyoona hanyamazi na ukakereka ulipaswa kuondoka mpaka hali itulie. No justification kwenye kupiga, omba msamaha yaishe.
 
Mkuu, nimesoma mada yako vizuri.
Binafsi nikiwa nasafari ni lazima nigombane na wife...since nimeoa!! Akijua nasafiri lazima tugombane.

Nakushauri we pima advantage ya hiyo safari yako, if it Worth usiache.
Muhimu call her apologies then Go on.

Hajapenda wewe kusafiri na kumwacha mwenyewe.
 
Kwa roho mbaya na kiburi nilicho nacho swezi kumuomba mwanamke msamaha ...hvi viumbe kukaa navyo inabid uwe dikteta afu katili sana yani unakua romantic pale ukitaka kula mzgo ...! Mwanamke anapata wapi ujasiri wa kubishana na mwanaume? Ukikaa na mwanamke kidkteta yani nyumba inakua na amani ugomvi wa kijinga kunakua hamna
Vijana ambao hamjaoa nawashauri "Tafuta mwanamke anae kupenda sana usijitie uchizi kumpenda mwanamke utahenyeka mpka ukome
 
Mkuu, nimesoma mada yako vizuri.
Binafsi nikiwa nasafari ni lazima nigombane na wife...since nimeoa!! Akijua nasafiri lazima tugombane.

Nakushauri we pima advantage ya hiyo safari yako, if it Worth usiache.
Muhimu call her apologies then Go on.

Hajapenda wewe kusafiri na kumwacha mwenyewe.
Mkuu nimeupenda ushauri wakoo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Duh tupe mrejesho mwingne mkuu.
Nashukuru Ahmad!

Namshukuru Mungu nilifika salama safari yangu Jana usiku, sikuwasiliana naye siku nzima ya Jana wala sms sikuandika, ila usiku huu nimempigia simu kumjulia hali yeye na mtoto na wengine tunaoishi nao.

Ila sijaongelea chochote kuhusu ugomvi wetu!

Tukaagana usiku mwema! Kwishaa habari!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyo mke uliolewa ama ulioa mwenyewe? Mkeo unaogopa kuingia chumba cha wadada una mila za kizamani sana wewe mtu. Ngoja akulalie na mwanaume humo ndani ndio akili zitakusogea. Fanya ambush kila chumba hana adabu.

watoto wake nyumba yake et anaogopa kuingia vyumbani 😀😀😀😀
 
Wasalam wana Jamvi!

Ni matumaini yangu kuwa mu wazima wa afya tukimalizia weekend yetu murua kabisa!!

Niweke mada mezani bila kupoteza muda!

Siku ya leo nimefanya kitendo ambacho sikuwahi kufikiria kukifanya katika maisha yangu. Tumepishana kauli na mke, sasa huwa nikiwa na hasira nina desturi ya kukaa kimya na kuondoka, na Mara zote huwa naepusha ugomvi kwa namna hiyo, ndugu zetu akina mama wamejaliwa kuongea sana tofauti na sisi wanaume, hasa mimi yaani sipendi kelele kabisa kama kuna issue tusemeshane taratibu tuongee tumalize sio kelele

Ilikuwa majira ya saa mbili na nusu asubuhi ya leo, wakati tumetoka tu kanisani ibada ya Alfajiri.

Issue ni ndogo sana, mimi naandaa nguo zangu kwa ajili ya safari yangu siku ya kesho, sasa kuna baadhi ya mashati yangu aliyatunzaga kabatini nikawa namwagiza anipatie, kidogo majibu yake hayakuwa mazuri ukizingatia ni mke wangu sio hawara, na mimi alivyonijibu ilikuwa kwa dharau flani au anamjibu mdogo wake au mtoto kiukweli sikupendezwa, nikamuuliza unamfanyia nani hayo? Ikaanza kelele wewe, nikamwambia sikuelewi !! Ahaa bhana niache huwezi kuchukuaa mwenyewe, nikawa mpole nikamwambia sipendi kelele inatosha, ikaanza mada nyingine ambayo haihusiani, kuhusu maswala ya fedha na aseti ikawa kelele zaidi nikamwambia haya nimekuelewa inatosha, ehee mwenzangu hanisikii wala haelewi, nikamwambia basi toka chumbani mimi sitaki sharii, ahaa sitokiii!! Kelele ikawa kubwa sana!! Nikashindwa kujizuia kiukweli nikampiga! Tangu hiyo asubuhi hatujasemeshana kabisa, wala kumwona sijamwona, maana nyumba ina vyumba vingi vingine siwezi ingiwa sababu ni vya wasaidizi wetu wa kike !! Ila naisikia sauti humu humu ndani!!

Baada ya hayo kutokea nikaenda kwenye mizunguko yangu nikarudi saa Tisa, aliyenitengea chakula ni shemj yangu yaani mdogo wake wa kiume ambaye pia tunaishi naye hapa!!

Jionii hii pia chakula nimekula na huyo shemj yangu yeye sijamwona!!

Sijui pia hali yake ikoje mpaka sasa!

Naombeni ushauri juu ya-:

1) Nimwombe msamaha kwa kitendo hicho?

2) Au nikae tu kimya ?

3) Kesho nisafiri kama nilivyopanga ?

4)Na ushauri mwingine wowote nipo tayari kuupokea!!

Nawasilisha karibuni kwa ushauri na michango mbalimbali!!
Umefanya vema,hawa viumbe wanataka starter sometimes. We tulia hivohivo,atakuja tu.
Endelea na majukumu

Luckman1
 
Duuh!! Ama kweli ndoa zina mengi.

Nadhani ifikie wakati muwe ni wenye kubadilika sasa mana mliyoyafanya ni kama watu waliooana juzi wakati kwa jinsi unavyoelezea watoto sijui nini na nini ni dhahiri ndoa yenu ina muda kidogo.

Yakishaisha inabidi mkae chini muambiane hiyo tabia si nzuri ya kwanza kurushiana maneno kama watoto wadogo pia kumpiga mkeo nako sidhani kama ni nzuri hiyo mana hapo si ajabu alivyokaa humo chumbani kwa watoto sijui kwa mdada ni dhahiri yote yaliyotokea amewahadithia na hapo si ajabu maneno aliyowaambia yakaanza kujenga chuki kwa watoto na wanafamilia wanaokuzunguka wakati hawakupaswa kuyajua hayo.

Nionavyo mjitahidi kubadilika yaani mkigombana mjitajidi yaishie humo humo chumbani kwenu kama mnuno uishie humo humo sababu huwa hayaepukiki hayo.
 
Kuna wakati wake zetu hutaka kupigwa japo kakofi tu.

Nakushauri, tazama mazingira, na mchape japo vikofi viwili-vitatu, halafu mpige kazi ya maana, naamini mtazungumza lugha moja.
 
Ukweli Hatustahili kupiga wanawake,ila inapobidi Kama jamaa unafanya hivyo tena Hakuna kuomba msamaha.
Yataendelea hayo hayo kwani atasema nilimkomesha mpaka aliponiomba msamaha hatatambua makosa yake.

Lazima ifike Mahala ieleweke Mume na mke ni nani.
Udhaifu wako ni kundoka bila kumtafuta ndani uhakikishe yupo au hayupo ili swali la Kwanza liwe ulikuwa wapi Kama hakuwa ndani
Wewe ni mkuu wa kaya pekua Kila mahali kwenye nyumba ikibidi wengine watoke nje.
Pia epuka kula home kukiwa na tafrani,Hasira huamua bila busara waweza lishwa sumu au kukukomoa

Ulitakiwa utoe agizo uandaliwe Nguo za safari ila si vibaya kujiandalia au kumsaidia kosa linaanza pale aliyesaidiwa hatambui kuwa ni jukumu lake tana anajibu kwa Dharau na kufoka

Wanawake niwaambie kitu -hakuna Hakuna mwanaume anayependa kelele na kufokewa na Dharau ni kosa no moja kubwa Sana na ikatokea sehemu akukutana na Mwanamke mnyenyekevu ndoa inaota Mbawa uwe na hela ,uwe mzuri ,uwe unajua mapenzi na mapishi Haijalishi ,utachukua nafasi ya mchepuko na mchepuko atachukua yako

Ukweli hii tabia ya kufoka,kelele na Dharau iko na wanawake wengi wa siku hizi ila nashukuru kwangu niliikomesha tena alienda mpaka kwao nikabaki kimya akapiga simu mtoto anaumwa nikatuma hela ya Dawa na kwenda kumwona mwisho nikaondoka bila kusema chochote ,nikawa napiga simu kujua mtoto anaendeleeje basi na sikuwa na Mchepoko, mwisho nikaombwa nauli ya kurudi nikakaza Kwanza - nilikutuma wapi,nikaombwa msamaha na kubembelezwa nikatuma nauli tukaja kukaa kujadili na kupeana mikakati mipya.

Siyo kwamba Nilikuwa simpendi au siumii hapana nilitaka yasije kujirudia tena .
Hivyo hawa watu wanahitaji kuwekwa sawa kwa hata kofi mbili wanapo lazimisha kufanya hivyo
 
Ukiendekeza mambo ya wanawake utakuwa zuzu wewe endelea na majukumu yako kama kawaida yeye aendelee kujifungia akichoka atatoka tu mwenyewe ila ukimbembeleza atajua huo ndio udhaifu wako utautumia kukutesa
 
Back
Top Bottom