Nini hatma ya ndoa hii? Naombeni ushauri urgent

Nini hatma ya ndoa hii? Naombeni ushauri urgent

Mremaaa

JF-Expert Member
Joined
Jul 1, 2015
Posts
293
Reaction score
325
Wasalam wana Jamvi!

Ni matumaini yangu kuwa mu wazima wa afya tukimalizia weekend yetu murua kabisa!!

Niweke mada mezani bila kupoteza muda!

Siku ya leo nimefanya kitendo ambacho sikuwahi kufikiria kukifanya katika maisha yangu. Tumepishana kauli na mke, sasa huwa nikiwa na hasira nina desturi ya kukaa kimya na kuondoka, na Mara zote huwa naepusha ugomvi kwa namna hiyo, ndugu zetu akina mama wamejaliwa kuongea sana tofauti na sisi wanaume, hasa mimi yaani sipendi kelele kabisa kama kuna issue tusemeshane taratibu tuongee tumalize sio kelele

Ilikuwa majira ya saa mbili na nusu asubuhi ya leo, wakati tumetoka tu kanisani ibada ya Alfajiri.

Issue ni ndogo sana, mimi naandaa nguo zangu kwa ajili ya safari yangu siku ya kesho, sasa kuna baadhi ya mashati yangu aliyatunzaga kabatini nikawa namwagiza anipatie, kidogo majibu yake hayakuwa mazuri ukizingatia ni mke wangu sio hawara, na mimi alivyonijibu ilikuwa kwa dharau flani au anamjibu mdogo wake au mtoto kiukweli sikupendezwa, nikamuuliza unamfanyia nani hayo? Ikaanza kelele wewe, nikamwambia sikuelewi !! Ahaa bhana niache huwezi kuchukuaa mwenyewe, nikawa mpole nikamwambia sipendi kelele inatosha, ikaanza mada nyingine ambayo haihusiani, kuhusu maswala ya fedha na aseti ikawa kelele zaidi nikamwambia haya nimekuelewa inatosha, ehee mwenzangu hanisikii wala haelewi, nikamwambia basi toka chumbani mimi sitaki sharii, ahaa sitokiii!! Kelele ikawa kubwa sana!! Nikashindwa kujizuia kiukweli nikampiga! Tangu hiyo asubuhi hatujasemeshana kabisa, wala kumwona sijamwona, maana nyumba ina vyumba vingi vingine siwezi ingiwa sababu ni vya wasaidizi wetu wa kike !! Ila naisikia sauti humu humu ndani!!

Baada ya hayo kutokea nikaenda kwenye mizunguko yangu nikarudi saa Tisa, aliyenitengea chakula ni shemj yangu yaani mdogo wake wa kiume ambaye pia tunaishi naye hapa!!

Jionii hii pia chakula nimekula na huyo shemj yangu yeye sijamwona!!

Sijui pia hali yake ikoje mpaka sasa!

Naombeni ushauri juu ya-:

1) Nimwombe msamaha kwa kitendo hicho?

2) Au nikae tu kimya ?

3) Kesho nisafiri kama nilivyopanga ?

4)Na ushauri mwingine wowote nipo tayari kuupokea!!

Nawasilisha karibuni kwa ushauri na michango mbalimbali!!
 
Kama kuna uwezekano wa kuahirisha safari ahirisha, mwombe msamaha, usafiri mkiwa mko powa.

Kitu cha muhimu, anza kuchunguza nini kinampa kiburi, na ili upate jibu ni lazima uwe umejishusha.

Ingawa story ni ya upande mmoja, nime assume hali iko kama ulivyoileta.
 
Halafu mkuu mwanamke hapigwi anapigwa na kipande cha kanga lakini katika unaweka jiwe
..
Au mpe ela bandia ataenda pigiwa sokoni

Anyway muombe samahani kuepusha Shari unaeza mwagiwa maji ya moto usiku huu ukiwa umelala
 
Namshukuru mkuu nimepokeaa!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu jishushe mwite mkae muongee mpe sababu kwann ulimpga na uongee kwa lugha ya kiungwana myamalize inawezekana na yeye alikujibu alikua na stress zake .. Mazungumzo ni njia bora kuliko kuliana buyu mnakua kama watoto
 
Halafu mkuu mwanamke hapigwi anapigwa na kipande cha kanga lakini katika unaweka jiwe
..
Au mpe ela bandia ataenda pigiwa sokoni

Anyway muombe samahani kuepusha Shari unaeza mwagiwa maji ya moto usiku huu ukiwa umelala
Nimepokea mkuu!! Mwanamke akiwa na hasira maamuzi yoyote ni sawa kwake!! Maana hata sasa hajaingia chumbani, na simu kazima tangu hiyo asubuhi!!
 
Labda nianzie hapa,,Ni nani mwenye makosa hapo kwa jinsi unavyoona??maana wewe ndie uliyekuwa kwenye tukio.be honest mkuu.
 
Mkuu nikuulize tu katika mahusiano yako una pesa za kutosha kumkidhi mkeo,only money make them calm..
mengine ni story tu za hapa na pale.
Pesa ninazo kiasi ambazo zinakimu mahitaji ya kawaida, sisi sote ni watumishi na kama familia kuna majukumu tumepeana na kwa hapo hamna shidaa sana mkuu!
 
Pole mkuu, umefanya la maana kumfundisha adabu kidogo, ila ni vzr mkamaliza hili kabla hujalala ili uende salama, muite mkalishe muelekeze vzr ataelewa. make sure anaelewa vzr ili kila mmoja aombe msamaha kwa kosa lake
 
Na hasira ni hasara

Mtafute bibie mbembeleze mambo yaishe naamini atakuelewa tu

Wanasemaga heri nusu Shari kuliko Shari kamili

Au hujaskia kwenye taarifa habari huko kanda ya ziwa wenzetu wanaviziwa wamelala wanakatwa uume... chanzo ni ugomvi majumbani kama huu
Nimepokea mkuu!! Mwanamke akiwa na hasira maamuzi yoyote ni sawa kwake!! Maana hata sasa hajaingia chumbani, na simu kazima tangu hiyo asubuhi!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa haraka nafikiri tatizo lote hilo limeanzia kwenye hiyo Safari
Inaonekana hayuko na amani kabisa
Aidha anaona unaenda kwa mchepuko maana wanachowazaga hawa watu huwa ni ngumu kuwaelewa kabisa hata kama utaotea anachowaza
Kumpiga ni mbaya zaidi maana ndio itakuwa tabia yako ya kumnyamazisha pindi kelele zikianza
Na hiyo ni mbaya sana
Omba msamaha tu yaishe na muagane kwa amani halafu muulize kama tatizo ni Safari hiyo
 
Kiukweli hata kama kosa lipo kwangu hakupaswa kunifokea kama mtoto mdogo, na kila mara namkataza hili jambo, kosa ni lake!!

Sent using Jamii Forums mobile app
Huu ni upande wako ndo tumeusikia..yeye hatujamsikia..lakini inaonekana wife wako anamzigo moyoni mwake..tafuta njia sahihi ya kuweza kuzungumza nae utakuja kugundua kuna vitu vingine unavyovifanya vinamkwaza sana na hakwambii..matokeo ndo kama haya sasa ..
 
Na hasira ni hasara

Mtafute bibie mbembeleze mambo yaishe naamini atakuelewa tu

Wanasemaga heri nusu Shari kuliko Shari kamili

Au hujaskia kwenye taarifa habari huko kanda ya ziwa wenzetu wanaviziwa wamelala wanakatwa uume... chanzo ni ugomvi majumbani kama huu
Ha ha ha na mimi niko kanda hiyo hiyo ziwa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa haraka nafikiri tatizo lote hilo limeanzia kwenye hiyo Safari
Inaonekana hayuko na amani kabisa
Aidha anaona unaenda kwa mchepuko maana wanachowazaga hawa watu huwa ni ngumu kuwaelewa kabisa hata kama utaotea anachowaza
Kumpiga ni mbaya zaidi maana ndio itakuwa tabia yako ya kumnyamazisha pindi kelele zikianza
Na hiyo ni mbaya sana
Omba msamaha tu yaishe na muagane kwa amani halafu muulize kama tatizo ni Safari hiyo
Safari ni ya Kimasomo, narudi masomoni ni kitu anafahamu vzr, nilikuwa nisafiri leo akaomba nisafiri kesho!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom