Nini hasa maana ya utu? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nini hasa maana ya utu?

Discussion in 'Jukwaa la Lugha' started by EMT, Nov 14, 2011.

 1. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #1
  Nov 14, 2011
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  WanaJF,

  Jana kuna MwanaJF alianzisha thread akilalamika kuwa mbunge wake wa Arumeru Mashariki ni mgonjwa sana na hivyo hawana mwakilishi jimboni kwao. Alitaka kujua serikali inaonaje kama Wana-Arumeru wakifanya uchaguzi mwingine ili wapate muwakilishi mwingine. Kwenye ile thread wapo waliosema kuwa “wakati mwingine tuweke utu mbele, thamani ya mtu ni utu, ubinaadamu ndio unatangulia na mengine yote yanafuatia..” Wengine wakasema kuwa “suala sio kubeza ugonjwa wa mbunge bali ni uwakilishi wa wanajimbo la Arumeru Mashariki full stop.”

  Pia jana hiyo hiyo, Faiza Foxy alipewa ban ya miaka miwili kwa kwa kutenda “kosa dhidi ya UTU” ikiwa na maana ya “Kukejeli na kubeza marehemu na sababu zilizopelekea kifo chake ni kosa tena kukosa Heshima.”

  Swali langu ni nini hasa maana ya utu? Ni utu kuendelea kumwacha madarakani kiongozi ambaye ni mgongwa sana to the extent kuwa hawezi hata kuwawakilisha tena waliomchagua? Je, mtu unaweza kula ban hapa JF kwa kutokuwa na utu? Ni vigezo gani tunavyotumia kujua kama mtu hana utu au amefanya jambo ambalo halina utu?

  Nim-quote Gaijin: “Utu ndio kitu gani? Utu unau define vipi? Kwa standards za nani? Tunaweza kusemaje nani ana utu zaidi kuliko mwingine kwa kufanya vitendo gani?”
   
 2. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #2
  Nov 14, 2011
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  Mimi nataka kuanza na msingi kabisa wa neno "utu"

  Unapofungua neno "utu" kwenye kamusi linakurejesha kwenye neno mtu ambapo unakutana na definition hii


  Sasa kwa tafsiri hiyo ya neno "utu" sielewi unawezaje kwanza kumpiga mtu ban kwa kukosa utu.
   
 3. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #3
  Nov 14, 2011
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  Tuseme kutompokonya mtu cheo chake cha uwakilishi wa wananchi japo hawezi kuwatumikia ni "utu" kwa Mbunge huyo, lakini hawa wananchi tumewafanyia "utu" nao?

  Ni "utu" kuwaachia watu katika jimbo wakae zaidi ya mwaka mmoja bila ya mwakilishi wao Bungeni?


  Nani ana-define huu "utu"?
   
 4. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #4
  Nov 14, 2011
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Katika kutafuta maana halisi ya utu nimekutana na thread moja ya zamani kidogo titled "Ni nini Utamaduni wa Mtanznia" ambapo Azimio Jipya alikuwa anachambua maana ya utu:

  "Kwa kinachote kilichowahi kufikiwa ili kujua true value za Mtanzania...jibu lilikuja moja... Ni UTU! Nafikiri kazi kubwa iko kwenye kutafsiri maana ya utu!

  Lakini wataalamu wa "elimu ya utu" dhidi ya "elimu ya akili" wanadai kuwa kila binaadamu alizaliwa na thamani inayoitwa UTU na utu unaweza kukuwa (To grow) au kufifia mtu anavyoendelea kuutumia, kuishi na umri kuongezeka. Lakini ukweli ni kuwa ingawa kila mtu anazaliwa na UTU ni wachache wanaulinda, kuukuza, na kuupenda hata kufa nao. Ni Wachache wanakufa wakiwa na UTU. Wengi wanakufa wanyama au karibu na hapo.

  Tumbili anaweza kuuliza utu ni nini, lakini sio mtu. Mwanadamu ataulizaje asili yake? Tumbili hakuumbwa kuwa na utu, hivyo anaweza kuushangaa, kuulizia na kutaka kuujua. Mtu anayeuliza maana ya UTU ina maana amesha upoteza..yaani amesha upoteza Utanzania.

  Mtanzania ni mtu mwenye utu!

  Utu ni character au zaidi unaweza kuwa ni Utamaduni!

  Asiye na utu ..ameupoteza Utanzania.

  Ni kweli kuna wakati Kiwango cha UTU WA TAIFA LA TANZANIA kilikuwa juu!Hakijawahi kutokea afrika.

  Utu Kwenye UONGOZI

  Utu kwenye Familia.

  Utu kwenye kilimo.

  utu kwenye elimu

  Utu kwenye mavazi

  Utu kwnye muziki

  Utu kwenye vyakula

  Utu kwenye Biashara

  Utu kwenye siasa ya nchi

  Utu kwenye mifumo ya kiuchumi ya taifa..azimio la arusha? etc

  Utu kwenye mahusiano na nchi nyingine

  Utu kwenye kuweka mikataba muhimu ya Taifa

  Utu ndani ya bunge na wabunge wenyewe!

  Utu kwenye sehemu za kazi..(Walikuwa hata na msemo .. KAZI NDIO KIPIMO CHA UTU)

  Utu kwenye muungano kati ya Tanganyika na Zanziber

  Utu kwenye baraza la Mawaziri

  Utu kwenye chaguzi mbalimbali za kitaifa.

  Utu kwnye kuwajali wananchi wote kwa pamoja..bila kuwepo kwa matabaka.

  Utu kwenye VIONGOZI WASTAAFU WA NGAZI ZA JUU KITAIFA

  Utu kwenye kila kitu ilikuwa ndio utamaduni wa Mtanzania. Na Alama za kitaifa zilidhihirisha hivyo. Kauli mbiu mbalimbali zilidhibitisha hivyo..etc

  Kujibu swali kuwa UTAMADUNI HUU WA UTU/UTANZANIA unadevelope au ume kwama....Kasi ya kudidimia kwa Utanzania kama utu ni kubwa na inatisha.

  Maendeleo bila Utu..? wapi yalishawahi kuonekana hayo? Siasa na uchumi kuwa mikononi mwa viongozi wasio na utu/mafisadi...iyatawezekana vipi?

  Kiogozi asiye Mtanzania/asiye na utu anaweza kufanya unyama na kuudhihirisha zadi ya tumbili.

  Anaweza kudiriki kuweka saini upande wa kuliangamiza Taifa....badala ya kuweka saini pale pa Kulinda na kutetea Taifa na Maendeleo ya wanachi wake.

  Kiongozi asiye na Utu/Fisadi anaweza kuuza Migodi yote ya madili mali ya Taifa kwa robo kilo ya almasi.

  Utanzania Ni Utu na Utu umetoweka Tanzania karibu kwenye kila nyanja.

  Ndio Maana viongozi wengi waliopo kwenye uongozi wanakufa/watakufa bila UTU! Wanakufa na watakufa wamepoteza asili yao ya kibinaadamu na ya kitanzania.

  Swali ..Walizaliwa na UTU Wameupotezea wapi? Ni sahihi kufa kama Mnyama au bila kuwa na heshima ya kiutu?......"

  https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/13822-ni-nini-utamaduni-wa-mtanzania-print.html
   
 5. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #5
  Nov 14, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  utu ni kumjali mtu na kumheshimu kila mtu na kuheshimu fikra na mawazo ya kila mtu..
   
 6. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #6
  Nov 14, 2011
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  Mimi nakubali kuwa miongoni mwa hao waliokwisha kuupoteza utu wao wa asili; hivyo najipa haki ya kuuliza "utu ni nini?" @Azimio jipya

  Na ikiwa utu wa taifa umeanza kupotea na wengi wanakufa wakiwa karibu na unyama kuliko utu, utamhukumu vipi mwenzio kwa kukosa utu?
   
 7. Dena Amsi

  Dena Amsi R I P

  #7
  Nov 14, 2011
  Joined: Aug 17, 2010
  Messages: 13,137
  Likes Received: 254
  Trophy Points: 160
  Utu bado haijapata tafsiri/maana yake
   
 8. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #8
  Nov 14, 2011
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Kuna mbunge mmoja huko Kenya alisema kuwa mtu ambaye hana dini hajui utu ni nini. Je, dini inaweza kuwa kigezo cha kujua kama mtu ana utu or at least anajua maana ya utu? Kwamba watu wasio na dini hawana utu?
   
 9. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #9
  Nov 14, 2011
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Kwa hiyo tusitumie utu kama kigezo cha kufanya maamuzi?
   
 10. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #10
  Nov 14, 2011
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  Dini ni nini?
   
 11. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #11
  Nov 14, 2011
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 688
  Trophy Points: 280
  Aseee!!
  Mmempoteza rafiki yenu??
  anyway.....invizibo atamfungulia tu!!
  thats how it works!!
   
 12. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #12
  Nov 14, 2011
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  Wakati unajali na kuheshimu fikra za kila mtu, unaruhusiwa kutoa na fikra zako pia japo kama zinakinzana na za hao wengine?
   
 13. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #13
  Nov 14, 2011
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Hapo itabidi uwaulize wenye dini. lol. Kwenye kitabu cha Chachage na Cassam titled: African Liberation: The Legacy of Nyerere at page 51 wanasema: "Ujamaa embraced aspects of the Swahili concept of utu or common humanity (or Ubuntu as is called in South Africa). This [utu] is based on the philosophy of forgiveness, reconciliation and willingness to share." Tunaweza ku-define utu kama kusameheana, kusuluhishana na kusaidiana? Japokuwa wapo wengine watasema utu simply mean Uhuru Through Ujamaa. lol
   
 14. Mwali

  Mwali JF-Expert Member

  #14
  Nov 14, 2011
  Joined: Nov 9, 2011
  Messages: 7,032
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  katika mazingira ya Ban nadhani walitumia "utu" kwa kumaanisha vitu kama 'compassion, respect for the deceased, support to victims vs oppressors' etc. kumbukeni circumstances za post katika kuisoma Ban yenyewe.
  Mnaweza kukaa hapa na kuongelea theoritical concepts kama utu na ubinadam ila kumbukeni kuna watu wanamsiba sasa hivi. nadhani hiyo Ban ni katika kuwasupport hao watu, na kila mtu mwenye kuamini kulikua na 'victim' na kwamba huyo 'victim' anahitaji support.
  Kama mnajadili utu kama utu, na haya ya FF mnachukulia kama mfano, ni tofauti na basi nadhani mchango wangu sio wamaana hapa. ila kama mnachukua swala la FF na mnataka kutafuta theory iliotumika/ilitumiwa basi someni mazingira kwanza.
   
 15. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #15
  Nov 14, 2011
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  lol. tunajaribu tuu kutafuta maana hali ya utu. Tumekuwa tukilitumia hili neno mara nyingi, lakini tunajua maana yake hasa ni nini?
   
 16. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #16
  Nov 14, 2011
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  Hapo kwenye tafsiri ya [utu] umeruka neno moja muhimu-falsafa.

  [utu] kwa mujibu wa Nyerere ni falsafa nzima ya usuluhishi, usamehevu na usaidizi-lol

  Ikiwa hiyo ndio definition ya [utu], kwenye kesi ya Mbunge Vs wana jimbo, [utu] unahusikaje?
   
 17. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #17
  Nov 14, 2011
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
 18. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #18
  Nov 14, 2011
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Mwali dhumuni la mada ni kujadili utu kama utu. Ban ya FF nimetoa kama mfano tuu, b'se kigezo chake ni FF kutokuwa na utu. For the avoidance of double ndio maana nilitoa pia mfano wa hali ya uwakilishi ilivyo kwenye jimbo la Arumeru Mashariki. Kwa hito tunaomba mchango wako juu ya utu kama utu. Unaweza kutumia mifano mingine ambayo haimhusishi FF.
   
 19. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #19
  Nov 14, 2011
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Thanks for the correction. Should have been "This philosophy blal bla bla." Kama tu-apply hiyo definition ya Nyerere kwenye kesi ya Mbunge Vs wana jimbo sijaelewa kama wahusika watakuwa wanasuluhisha nini. Kwani kuumwa kwa mbunge ni kosa kwamba asamehewe? Hapo kwenye usaidizi labda watakuwa wanamsadia kimapato? Kwa sababu kuumwa kunahitaji matibabu na matibabu yanahitaji fedha? So, wakimwondoa watakuwa hawana utu kwa sababu atakosa fedha za matibabu? But vipi wao hawahitaji usaidizi wa kuwakilishwa?
   
 20. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #20
  Nov 14, 2011
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,560
  Likes Received: 1,929
  Trophy Points: 280
  Huyo dada naye alikuwa na roho mbaya sana.Ama sijui ni hasira ama some days?
   
Loading...