Nini hasa maana ya utu?

ETM na Gaijin sheria zimabadli kabisa maana ya utu, narudia tena si kila sheria au haki ni utu, kinacho tutofautisha na wanyama ndio utu wetu, utu anaostahiki mtu wa usa ndio anastahiki mtanzania, kuna baadhi ya watu wanageuza matakwa yao binafsi(kama ushoga)kuwa eti haki za msingi na ni utu

Kumhukumu kifo na kumuua mhalifu aliyeua ni unyama au ubinaadamu?
 
Hivi mnajua katika utu huu tunaongelea kuna nchi kama uswisi kuna utu wa kutambua right to die

Sasa katika kuona utata wa hili neno UTU tujaribu kutazama concept nyingine yahaki/maamuzi ya kufa.

  • Je ni utu klazimisha mtu kuendelea kuishi hata kama mtu huyo hataki. Niliona true-story documentary. kijana wa 45 yrs baaada ya kupata ajali na kuwa kwenye wheel chair for two years akachoka maisha . Kijana anajiona si mtu sababu hawezi kufanya mambo aliyoweza fanya kama mtu. Anajiona hana utu.kijana anataka aruhusiwe kufa . Kijana anajiona yeye kakosa utu na kuosa kwake utu kawa mzigo kwa familia. Familia yake inapinga lakinii kijana yeye anaona familia hawana utu . So sababu nchini kwake hawaruhusu kijana anaamua kufuta utu wa kufa nchini uswis.
Maana thamani ya msingi mwanzo ya utu niyoelewa mimi ni uhai na kuishi . Lakini sasa wenzetu tayari wako hatua moja kuwa kumbe thamani ya utu pia ni maamuzi na uhuru wa mtu kuamua ni wakati gani afe.

Kwa kweli niliangalia ile documentary kwa watu kama watatu hivi nilibakii sina jibu.
  • Ni utu kuwakatailia wanaotaka kufa hata kama wana sababu za msingi?
 
Asha dii unajaribu kusema nini dada yangu, bado sijakusoma uzuri


Hahaha.... Nitarudi badae Paulss... Kama hujaielewa inamaana hata mimi nikiisoma sitaielewa hivo not coherent na ikiwa hivo I will re-write it. Hii topic imetulia ndo matatizo ya kuchangia akili haijatulia... Hivo poleni....
 
  • Thanks
Reactions: EMT
Mtazamaji,

Mkuu heshima yako.
Hili nimelisemea toka awali matakwa binafsi sio utu, unaweza kutaka kitu fulani kwa kusukumwa na jambo fulani, lakini in general mbele ya macho ya jamii sio utu
Sio kila sheria ni utu na si kila utu ni sheria
 
Mkuu heshima yako.
Hili nimelisemea toka awali matakwa binafsi sio utu, unaweza kutaka kitu fulani kwa kusukumwa na jambo fulani, lakini in general mbele ya macho ya jamii sio utu
Sio kila sheria ni utu na si kila utu ni sheria

Nakubalina na wewe kiasi fulani na ndio maana ufafanuzi wangu wa mwazo nikataja utu katika concept ya jamii ambayo wewe uliekea kuhoji kidogo.

Otherise Mkuu tuko pamoja lakini pakua na tazama documntary hii uone hilo neno utu lilivyo complicated. uone maslahi ya utu kati ya mtu binafsi na jamii ya watu au utamaduni fulani yanaweza kuwa tofauti.

@EMT
Kwangu
  • Tanzania tukitambua ushoga through process ziliztotumia kwa UK, USA, etc na wengine kutambua ushoga inaweza ikawa ni utu lakini tanazania kutambua ushoga kwa sababu ya external pressure sio utu bali ni maigizo ya utu na kudhalilishwa utu
  • Tanzania kwenda kuomba misaada nje ya nchi kufanya jambo fulani bado hakutuondelei utu lakini Kuletewa msaada ambao hujaomba japo unauhitaji na kuagizwa ufanyie nini na utumike vipi na masharti kibao hapo hakuna utu. Au kukubali misaada yenye masharti ya kukuondoa kwenye misingi wa utu wakona kutupeleka kwenye msingi wa utu wa ucopy na kupaste huo si utu ni sanaa.
Ndiyo kwa mtazamo wangu kwa nchi kama Tanzaniai hatujafikia level ya kuondoa adhabu ya kifo. Tumeiga utu wa watu wengine na kuondoa adhabu hii.
 
Ha ha ha EMT

Na mishahara na posho za wabunge jee zinafuata kanuni za utu wa Mtanzania kweli?

Hii haifuati kanuni na utu wa majukumu sababu kuna watu wana kazi muhimu zaidi na zinahusisha eneo kubwa zaidi la kimajukumu kuliko mbunge lakini mishahara yao iko chini. Linganisha umuhimu na ukubwa wa kazi ya afisa kilimo wa wilaya au Mkoa au RPC na mbunge alafau tazama maslahi yao . Utaona utu wa mwanasiasa Tanzania uko juu
 
Nakuja empirical kidogo, na nitanukuu watu ambao sio scholars, hawakutunga great theories na in fact labda hawakua na utu wowote.

Kuna mmishonari mmoja alienda Congo in 1600s. Alipofika akamuuliza mfalme wa Kongo Empire (Mfalme Nzinga Ankuvu I):

nyinyi mnamuabudu nani?

Nzinga Ankuvu akasema: Tunamuabudu Nzambi.

Mmishonari akasema: Unaja, Yesu ndie Mungu pekee apaswaye kuabudiwa.

Nzinga Ankuvu: Basi Yesu ndie Nzambi

Mmishonari: Na unajuaje Yesu ndio Nzambi?

Nzinga ankuvu: Sababu 'Nzabi nde Nzabi' (Mungu ni Mungu). Huwezi kum-define Mungu, you can only feel him, live him.

Na mimi naona hapa tunaweza kuendelea hadi kesho na tusipati Jibu. Utu ni Utu na mtu akikosa Utu utaona matokeo yake kwa watu wanao mzunguuka. Uki-exercice Utu wako, huwezi kuleta negative effect katika jamii. Social symbioses,peace and harmony will prevail. Utu haupimwi on an individual level, unapimwa kukiwa na watu.
Najua kuna watu watataka kujua what is symbiosies, harmony and peace ila sitajibu. they too are things we can only define through their materialisation.
 
Ha ha ha EMT

Na mishahara na posho za wabunge jee zinafuata kanuni za utu wa Mtanzania kweli?

Hasa kwenye taifa hili changa, ambalo linajali heshima na utu wa binadamu. Nimesoma sehemu kuwa wabunge hawahitaji fedha za ziada kuliko mtu mwingine yeyote. Kama ni kukuta masahibu yanayowataka watumie fedha zao za mfukoni hilo huwakumba wengine na inatokana na utu wala si wajibu.
 
Kumhukumu kifo na kumuua mhalifu aliyeua ni unyama au ubinaadamu?

Mkuu kama utarudi nyuma hatua kadhaa kidogo kwenye hiki "kigoda cha Utu", utaona nimeandika mahali fulani kuwa moja kati ya kanuni za msingi za utu ni "Two wrongs cant make it right"...kutoa uhai wa mtu kwa kuwa mwingine ametoa uhai wake. Utu hauhitaji kutumia "unyama" kwa mtu aliyekosa utu, bali kutumia kanuni za msingi za utu kwa aliyekosa utu....Utu unaenda kinyume kabisa na "retribution" and "revenge" ila una demand "disciplining"

Cha kufanya ni kuwa na system au setting (kwa maana ya tafsiri nilizotoa hapo awali) za kumuadhibu huyu aliyefanya kosa, lakini wakati huo huo ule utu wake ukitiliwa umaanani......h

So in its generality and reality (in the name of Utu), kumuua mtu aliyeua sio utu
 
Mkuu RR hebu tendeeni haki hiki "KIGODA CHA UTU" kwa kukiweka kuwa Sticky thread ili iwasaidie hata wanaofanya review ya katiba wahakikishe angalau wanaweka tafsiri ya "utu" kwa lugha yetu kutusaidia hasa kwa kuzingatia mkuu Gaijin anapata tabu sana kukosekana kwenye tafsiri za sheria zetu na zaidi kwenye katiba

Ni ombi
 
Mtazamaji,

If the person decided himself that he want to die na utu wa jamii yake uko upande wake, then sioni tatizo. But remember Terry Shiavo's story? The unconscious woman who for 15 years was living on substances she received from her feeding tube, died from starvation caused by the removal of her breathing tube. Since the time she lost consciousness from lack of oxygen, she was kept in the center in a persistent vegetative state in a hospice.

Terry's legal custodian, her husband, believed that Terry should be allowed to die and so insisted on the removal of the tube. Her parents, on the contrary, insisted that Terry 's life should be sustained further arguing that their daughter was responsive to outside stimuli. Both sides had their supporters that stage street protests in support of their viewpoints.

Nani alikuwa ana utu hapo? Husband or her parents and their supporters? Hii inaonyesha utu unatofautiana mpaka kwenye familia.
 
Mtazamaji,
Kwa hiyo tulivyo-incoporate human rights kwenye katiba yetu miaka ya 1980s due to external pressures utu wetu haukudhalilishwa? Au IMF and WB walivyo pressurize to adopt zile structural adjustment programmmes, hatukulalilisha utu wetu pale tulipozikubali na kuamnua kuua kabisa ujamaa ambao mojawapo ya nguzo yake kubwa ilikuwa ni utu?
 
@RussianRoulette,

RR una maana gani unaposema utu ni utu? I am lost. lol
 
Tunaweza kusema mtu kakosa "utu" kwa kufanya kitendo ambacho kwa hali ya kawaida binadamu aliye na akili timamu asingeweza kufanya. Tunaweza kulinganisha utu na kukosa huruma kwa binadamu wenzako kwa kufanya matendo yanayoweza tafsiriwa kuwa binadamu hapaswi kumtendea mwingine. Mf. Kushabikia kifo cha mtu asiye na hatia ni kukosa utu na hiki ndicho alichokifanya F.Fox.

Tukirudi kwenye swala la Mbunge, anaweza kukosa sifa ya uwakilishi kwa sababu kadhaa ikiwemo kupoteza akili na ama kuugua katika hali ambayo hawezi kuendelea na majukumu yake na iwapo kitaalam imethibika hivyo. Mfano. Mfanyakazi wa serikali akiugua kwa miezi sita mfululizo bila kuhudhuria kazini anapoteza sifa za kuwa mfanyakazi.

Hii haimanishi sheria haina utu, hapana. Lengo ni kuweza kuwapa wananchi fursa ya kupata huduma. NIONAVYO MIMI HILI LA ARUMERU LINAPASWA KUZUA MJADALA IWAPO KUNA HAJA YA KUWASTAAFISHA, KWA SABABU ZA UGONJWA, WABUNGE AMBAO WATAKUMBWA NA TATIZO LA KUUMWA KWA MDA MREFU. IKUMBUKWE KUWA TOFAUTI NA NAFASI NYINGI ZA UWAKILISHI WA WANANCHI MBUNGE HANA MSAIDIZI YAANI MAKAMU. HIVYO ANAPOUGUA KWA KIPINDI KIREFU WANANCHI WANAKOSA UWAKILISHI.


Kwa maelezo haya na kwa muktadha wa hoja iliyoko mbele yetu kufungiwa kwa F.Fox kusitafsiriwe kama uonevu
 
RR una maana gani unaposema utu ni utu? I am lost. lol
Maana yangu ni kwamba lugha (ya kiswahili na zingine zote) are weak and distorted. Tukianza kutafsiri UTU kwa kutumia maneno tutaishia kusema vitu vingine, na sio UTU. The only way to apprehend the concept is to define related concepts, na kudefine abscence ya UTU kwa binadam, na consequences zake.
 
EMT,

Yes utu ni complicated lakini mfano unatoa wewe ni mwepesi kiogo sababu muhusika mkuu hawezi kuzungumza . Sijui yule Rais wa israel naye mpaka leo anaishi kwenye mashine sababu ya utu au alisharuhusiwa kufa kufa sababu ya utu.

Nasikia hata mwalimu Nyerere naye ilikuwa ni maamuzi ya utu ya pande mbili zinazotofautiana. Aendelee kuishi kwa utu wa mashine kwa siku kadhaa zaidi au familia ikubali apumzike kwa utu. Je yeye mwenyewe mwalimu angeweza kuzungumza nini kwake ilikuwa ni utu.

Complication na changamto inakuja zaidi pale mhusika mkuu anayetaka kufa anaweza kuongea na anaogea akiwa na akili zake. Kweye documenary hiyo kuna mmoja anasema akifikia stage fulani ya mattaizo yake atapenda kufa.

kuna mwingine inaonyesha mpaka safari yake ya kwenda uswisi kufa ki-utu. Mkewe hakutaka hivyo lakini ilibidi akubaliane. Very complicated Nadhani hiyo hospitali ya uswisi ni maarfu sana duniani. Watu wanaenda kufuatu utu wao wa kufa huko.
Kumbuka hiyo hopitali hawaui vichaa au watu ambao wamepoteza uwezo wao wa kuelewa. na kutambua mambo yanayowazunguka.
 
Back
Top Bottom