Nini athari za kupunguza kodi ya kuingiza magari nchini?

Iko hivi magari mengi madogo enzi za JK yalikuwa yanalipiwa ushuru wa sh mil 2 laki 6 hadi milioni 2 laki tisa, ilikuwa inachezea hapo sasa Mzee mzima alipoingia alibaini kuna magari mengi yanaingia akaona ni fursa kwake kuongeza ushuru ili akusanye zaidi ndio akaongeza kama double ikawa mil 5 hadi 6 sasa ukijumlisha unakuta bei inakuwa ghali wakati mwingine kununua unaloliona hapa nchini kwa anayetumia na ana shida na hela, ni rahisi kuliko kununua nje ya nchi pamoja na kuwa tunahitaji ubora wa Japan lakini wakati mwingine inakuwa ngumu sana. nilikuwa nanunua Subaru Wagon kwa CIF dola 1800 hadi elf 2 wakati huo ilikuwa kama sh mil 4 hivi, sasa ushuru niilikuwa nalipia mil 2 laki 7 huku nilikuwa nauza mil 8 hadi 10 maana ilikuwa inalipa. alipoingia jamaa na kuongeza ushuru niliacha kabisa nlijikuta ushuru na kununua inafika mil 9 hadi 10 sasa nitauza ngapi nani atanipa mil 12 hakuna niliamua kuacha kabisa. ila ndo hivyo
Aisee we jamaa acha uongo uongo hatujaanza kununua magari leo,tangu enzi za JK kodi za magari ni tatizo tu.
 
HUO USHURU MKUBWA UNATUKATISHA TAMAA WENGINE KUNUNUA GARI KUTOKA NJE
 
Cha ajabu ni kwamba document za TRA zinakinzana yani hakuna uhalisia wa wanachokisema mfano ukiangalia hii document ya kozi mpya za mwaka 2019/2020 inaonesha kwamba gari yenye 2500CC inatakiwa ilipiwe 300,000 kama ada ya usajili kwa mara ya kwanza lakini kwenye ile calculator ya TRA inasomeka 500,000 pia adui mkubwa ni hio excise duty due to age hio bei beforwrd inauzwa $3000 CIF ila ukiicheki hio excise duty due to age ni $1724 kwa hesabu za haraka haraka ukichukua hio total taxes USD 4710.15 - 1724 = 2986 x 2300 = 6,878,000 ambayo inalipika kirahisi tofauti na ukiwepo huo uchakavu
 
Attachments

  • Screenshot_20190808-163019_Samsung Internet.jpg
    Screenshot_20190808-163019_Samsung Internet.jpg
    130.8 KB · Views: 33
  • Screenshot_20190808-163232_Adobe Acrobat.jpg
    Screenshot_20190808-163232_Adobe Acrobat.jpg
    195.4 KB · Views: 33
Aisee we jamaa acha uongo uongo hatujaanza kununua magari leo,tangu enzi za JK kodi za magari ni tatizo tu.
Tena enzi zile unalinunua huko hujui nini utakutana nacho! Gari $1500 hadi Bongo unashtukia makadirio kodi 8m! Sasa hivi hii calculator ya TRA inakuwezesha kujua kabla gari haijafika. Ila ukiagiza december kuwa makini maanake january wanaweka bei mpya, niliisoma namba!
 
Acha maneno weka proforma invoice inayotoka kwenye system ya TRA na mimi nikuwekee tumalize ubishi wako
Aisee we jamaa acha uongo uongo hatujaanza kununua magari leo,tangu enzi za JK kodi za magari ni tatizo tu.
 
Tatizo kubwa la ushuru wa magari ni pale kwenye excise duty due to age pale ndo hela nyingi inatafunwa na uchakavu yani theory ile ni yabkipumbavu sana sababu haizingatii uhalisia mfano watanzania wengi wanamudu kununua magari ya kuanzia 2002-2010 sasa hapo kuna kua na uchakavu unaofanya bei uliyonunulia gari kuzidi ime umenunua gari $2500-3000CIF unakuja kulipa kodi $2900 au 3500 ndo jambo gani pia hata ukisema ununue gari ya kuanzia 2015 hadi 2019 bado kodi na gharama yake ipo juu sana yani hakuna unafuu wowote ule ni upuuzi mtupu sababu Tanzania hakuna kiwanda cha magari kinacholindwa
Kuna jamaa yangu alinunua gari CIF $37000 jipaya zero mileage alitaka kulikimbia TRA mungu anawaona
 
Kwa maisha ya Sasa gari Sio luxury Ni necessity serikali ipunguze tu Kodi za magari watu wengi wanunue itapata Kodi nyingi kupitia mafuta yanayojazwa kwenye hayo magari ambapo Kodi ziko kibao kwa kila lita
Shida ya serikali inapenda mambo ya kubania raia wake mpaka inakera yaan ipo tayari ikose hata mapato kama hili la magar na la passport ambalo uliwahi liongelea sana
 
Mimi naona kama kodi itapungua au itakua rahisi kwa kila mtu kuingiza gari let say kwa sasa wa tz tuko milioni 50 haya tutoe watoto hapo kama milioni10 sasa imagine magari yawe milioni 40 je tutayaendeshea wapi? hivi hivi tu foleni kibao sasa ndio yawe mengi kama simu tutaendeshaje? Na kama hayataendesheka serikari itapataje kodi kwa upande wa mafuta? itapata tu kodi ya kuingizia magari nchini. Haya ukiangalia na hasara zingine pollution etc hata mabasi watu hawatapamda maana kila mtu ana gari yake kwa hiyo hata kodi kwa wafanyabishara wa magari itapungua wacha iwe hivi hivi tu bana tupunguze msongamano na balance katika biashara.
Haiwezi kufikia idadi ya magari kufikia milioni 40 kati ya watu milioni 50. Tena idadi imiwakubwa sio kwamba yataendeshwa kwa wakati mmoja yote. Kuongezeka kwa idadi ya simu na mapato ya simu yameongezeka pia .magari mengi yatachangia usafirishaji wa mazao na huduma za kijamii
 
Cha ajabu ni kwamba document za TRA zinakinzana yani hakuna uhalisia wa wanachokisema mfano ukiangalia hii document ya kozi mpya za mwaka 2019/2020 inaonesha kwamba gari yenye 2500CC inatakiwa ilipiwe 300,000 kama ada ya usajili kwa mara ya kwanza lakini kwenye ile calculator ya TRA inasomeka 500,000 pia adui mkubwa ni hio excise duty due to age hio bei beforwrd inauzwa $3000 CIF ila ukiicheki hio excise duty due to age ni $1724 kwa hesabu za haraka haraka ukichukua hio total taxes USD 4710.15 - 1724 = 2986 x 2300 = 6,878,000 ambayo inalipika kirahisi tofauti na ukiwepo huo uchakavu
Yani we we unatumia alhaji techno halafu unajitutumua hapa unataka kuagiza Mercedes Benz,kweli?
 
Mimi naona kama kodi itapungua au itakua rahisi kwa kila mtu kuingiza gari let say kwa sasa wa tz tuko milioni 50 haya tutoe watoto hapo kama milioni10 sasa imagine magari yawe milioni 40 je tutayaendeshea wapi? hivi hivi tu foleni kibao sasa ndio yawe mengi kama simu tutaendeshaje? Na kama hayataendesheka serikari itapataje kodi kwa upande wa mafuta? itapata tu kodi ya kuingizia magari nchini. Haya ukiangalia na hasara zingine pollution etc hata mabasi watu hawatapamda maana kila mtu ana gari yake kwa hiyo hata kodi kwa wafanyabishara wa magari itapungua wacha iwe hivi hivi tu bana tupunguze msongamano na balance katika biashara.
Mkuu hapa kwenye mbanano, ni swala la miundombinu tu, kodi itakayopatikana ndio itatumika kuendeleza miundombinu bora kwa ajili ya usafirishaji!!

Hata nchi zilizoendelea, hutoa kipaumbele sana katika swala la usafiri, na kwa wenzetu Gari ni basic need!!! Sisi bado tuko zama za ujima kuwa gari ni anasa.

Pia kwanini watu wanapozungumza swala la magari (wingi, mahitaji na wahitaji) fikra zao huishia Dar tu, kwani mikoani watu hawahitaji?? Mikoa mingi sana bado kunauhaba wa magari na uhitaji ni mkubwa, sema kipato kwa wakazi wa mikoa hiyo sio rafiki kutokana na kodi kuwa kubwa.

Naungana na mtoa post hii kuwa, Serikali inapoteza fedha nyingi sana kutokana na kodi kuwa sio rafiki, kama tungekuwa wazalishaji basi kodi hii ingekuwa sehem ya ku discourage importation ili viwanda vya ndani vikue, badala yake imekuwa kinyume, inchi (wanachi wanauhitaji lakini kodi ni kubwa na serikali inakosa mapato haswa.

Nadhan viongozii wauangalie tena mfumo wa kodi za magari, naamini ni sehem itakayo iongezea serikali makusanyo kwa haraka zaidi kwakuwa itakuwa imepanua wigo wa makusanyo katika
1. Ongezeko la uingizaji magari
2. Ongezeko la matumizi ya mafuta
3. Matumizi ya vipuri
4. Usafirishaji wa mazao hasa huko viijini (mashambani)
5. Ongezeko la watumia magari (leseni)
6. Bima za Magari.

Swala la uchafuzi wa mazingira nadhani kwa inchi yetu bado saana kwa kuwa badon kuna uhaba wa magari, isitoshe kwa sasa tunahamia technologia ya matumizi ya gesi ili kupambana na uharibifu wa mazingira.

Lakini pia, kuna haja ya kuanzisha sera ya matumizi ya magari kwa mikoa au majiji yenye msongamano! Mfano, kuanzisha makusanyo ya ushuru wa kuingia na gari katikati ya mji ( japo kuna challenges) lakini inawezekana, na ushuru huu uwe rafiki, eg Tsh 10,000 kwa Gari dogo na 20,000 kwa gari kubwa!! Lengo ni ku discourage matumizi ya magari binafsi hasa maeneo yanayokusanya watu wengi kwa wakati mmoja ( kama posta kwa dsm)
 
Hoja yako ni sawa ila nilikua narespond kwa jamaa hapo juu aliyesema angependa magari yawe mengi kama simu na nnavyojua kwa sasa karibu kila mtanzania anamiliki simu sasa fikiria idadi ya simu ndio iwe idadi ya magari itakuaje hapo
Garama za kumiliki gari haziwezi kufananishwa na garama za kumiliki simu! Kama gari inauzwa $ 1,200 japan ikifika bandarini Dar ukaipata kwa milion 6 bado wataomiliki ni wachache ila sio kama inafka dar kwa milion 12. Asilimia kubwa itakua wafanyakazi na wafanyabiashara. All in all gari sio anasa
 
Wakati zanzibar ushuru ukikalukulatiwa through (FOB) Bei ya bidhaaa peke yake kwetu wameinclude mpaka bei yake bima na usafiri
 
Mkuu hapa kwenye mbanano, ni swala la miundombinu tu, kodi itakayopatikana ndio itatumika kuendeleza miundombinu bora kwa ajili ya usafirishaji!!

Hata nchi zilizoendelea, hutoa kipaumbele sana katika swala la usafiri, na kwa wenzetu Gari ni basic need!!! Sisi bado tuko zama za ujima kuwa gari ni anasa.

Pia kwanini watu wanapozungumza swala la magari (wingi, mahitaji na wahitaji) fikra zao huishia Dar tu, kwani mikoani watu hawahitaji?? Mikoa mingi sana bado kunauhaba wa magari na uhitaji ni mkubwa, sema kipato kwa wakazi wa mikoa hiyo sio rafiki kutokana na kodi kuwa kubwa.

Naungana na mtoa post hii kuwa, Serikali inapoteza fedha nyingi sana kutokana na kodi kuwa sio rafiki, kama tungekuwa wazalishaji basi kodi hii ingekuwa sehem ya ku discourage importation ili viwanda vya ndani vikue, badala yake imekuwa kinyume, inchi (wanachi wanauhitaji lakini kodi ni kubwa na serikali inakosa mapato haswa.

Nadhan viongozii wauangalie tena mfumo wa kodi za magari, naamini ni sehem itakayo iongezea serikali makusanyo kwa haraka zaidi kwakuwa itakuwa imepanua wigo wa makusanyo katika
1. Ongezeko la uingizaji magari
2. Ongezeko la matumizi ya mafuta
3. Matumizi ya vipuri
4. Usafirishaji wa mazao hasa huko viijini (mashambani)
5. Ongezeko la watumia magari (leseni)
6. Bima za Magari.

Swala la uchafuzi wa mazingira nadhani kwa inchi yetu bado saana kwa kuwa badon kuna uhaba wa magari, isitoshe kwa sasa tunahamia technologia ya matumizi ya gesi ili kupambana na uharibifu wa mazingira.

Lakini pia, kuna haja ya kuanzisha sera ya matumizi ya magari kwa mikoa au majiji yenye msongamano! Mfano, kuanzisha makusanyo ya ushuru wa kuingia na gari katikati ya mji ( japo kuna challenges) lakini inawezekana, na ushuru huu uwe rafiki, eg Tsh 10,000 kwa Gari dogo na 20,000 kwa gari kubwa!! Lengo ni ku discourage matumizi ya magari binafsi hasa maeneo yanayokusanya watu wengi kwa wakati mmoja ( kama posta kwa dsm)
Mkuu umefafanua vizuri sana maana wanaangalia kodi kwenye kuingiza gari bila kuangalia kodi itayopatikana baada ya kupounguza ushuru wa kuagiza magari..unaweza kupunguza kodi kwa 25% ikapelekea mapato kuongezeka kwa 150% maana hapa tunazungumzia mapato ya
Mafuta
Leseni
Ajira
Vipuri
Kuimarika kwa huduma za usafiri n.k
 
Mi kuna kitu huwa kinanishangaza, lengo la kuweka kodi kubwa mfano kama tulivyofanya kwenye maziwa ni ili kulinda wazalishaji maziwa wa ndani, lakini kwenye magari hatuna viwanda, sasa hii ni kuumizana tu
Waafrica bado tunaamini kuwa na gari ni luxury, tungelikuwa tunaamini ni basic hayo ya kodi kubwa yasingekuwepo
 
Surw mkuu hata kazini ukimiliki gari tu hata kama huna nyumba wanaona una maisha bora sana na wanaweza kwenda mbali sana kusema fisadi ... Wakisikia una nyumba wanakuona kawaida tuu
 
Umetia na chumvi na ndimu mazee!

Back
Top Bottom