Nini athari za kupunguza kodi ya kuingiza magari nchini?

Iko hivi magari mengi madogo enzi za JK yalikuwa yanalipiwa ushuru wa sh mil 2 laki 6 hadi milioni 2 laki tisa, ilikuwa inachezea hapo sasa Mzee mzima alipoingia alibaini kuna magari mengi yanaingia akaona ni fursa kwake kuongeza ushuru ili akusanye zaidi ndio akaongeza kama double ikawa mil 5 hadi 6 sasa ukijumlisha unakuta bei inakuwa ghali wakati mwingine kununua unaloliona hapa nchini kwa anayetumia na ana shida na hela, ni rahisi kuliko kununua nje ya nchi pamoja na kuwa tunahitaji ubora wa Japan lakini wakati mwingine inakuwa ngumu sana. nilikuwa nanunua Subaru Wagon kwa CIF dola 1800 hadi elf 2 wakati huo ilikuwa kama sh mil 4 hivi, sasa ushuru niilikuwa nalipia mil 2 laki 7 huku nilikuwa nauza mil 8 hadi 10 maana ilikuwa inalipa. alipoingia jamaa na kuongeza ushuru niliacha kabisa nlijikuta ushuru na kununua inafika mil 9 hadi 10 sasa nitauza ngapi nani atanipa mil 12 hakuna niliamua kuacha kabisa. ila ndo hivyo
Hizo gharama za miaka mingi, enzi za jk yalipita kwa ujanja ujanja,details zako sio za kweli.
 
Kama ni za ujanja ujanja kwanini wanatoa risiti halali, tuwekee hapa gharama unazosema ni za ukweli ila uweke proforma Invoice walizokupa kwa kulipia na mimi nitaweka tujue nani mkweli, proforma Invoice ni zile za TRA kutoka kwenye system, weka hapa nijue kama wewe ni mkweli
 
Hizo gharama za miaka mingi, enzi za jk yalipita kwa ujanja ujanja,details zako sio za kweli.
Hakuna ujanja ujanja kodi ya magari inajulikana kua ipo juu kuliko uhalisia wake!! Serekali inaamini ukiwa na hela ya kununua gari wewe ni tajiri sana hizi ni fikra za miaka ya 70 na 80 sio miaka ya sasa!! Magari yakiwa mengi barabarani kodi ya serekali inaongezeka hasa kwenye mafuta, vipuri,maegesho,ajira za madereva na gereji. Waache fikra za kmaskini
 
Wafanya biashara wanaleta risiti feki ambayo sio bei halisi ya gari ili walipe kodi ndogo, lakini TRA si walishaangalia bei halisi ya magari ya Japana kutokana na condition zake na wakaamua kuweka bei halisi na bei ya ushuru wake?
Ndiyo mjadala unaoongelewa hapa.
Waliopanga hizo kodi na utitiri wa maushuru, kwanini wapange kodi kubwa kuliko bei ya gari? Hilo ndiyo swali la kujadili hasa na kutoa mapendekezo.
 
Aisee siwaelewi kabisa mbona hata ukileta risiti halali kodi ni kubwa kuliko??
Kwani kwenye ujanja ni kwenye magari tuu?
Mbona ukinunua nguo za milion 20 china kodi haulipi milioni 50??
 
Ukitaka kuingiza gari bila kulipa kodi, agiza trekta. Hii ni zero rated. Unanunua tractor unaenda nalo kazini... Msimu wa kikimo, unalipeleka shamba.
 
Iko hivi magari mengi madogo enzi za JK yalikuwa yanalipiwa ushuru wa sh mil 2 laki 6 hadi milioni 2 laki tisa, ilikuwa inachezea hapo sasa Mzee mzima alipoingia alibaini kuna magari mengi yanaingia akaona ni fursa kwake kuongeza ushuru ili akusanye zaidi ndio akaongeza kama double ikawa mil 5 hadi 6 sasa ukijumlisha unakuta bei inakuwa ghali wakati mwingine kununua unaloliona hapa nchini kwa anayetumia na ana shida na hela, ni rahisi kuliko kununua nje ya nchi pamoja na kuwa tunahitaji ubora wa Japan lakini wakati mwingine inakuwa ngumu sana. nilikuwa nanunua Subaru Wagon kwa CIF dola 1800 hadi elf 2 wakati huo ilikuwa kama sh mil 4 hivi, sasa ushuru niilikuwa nalipia mil 2 laki 7 huku nilikuwa nauza mil 8 hadi 10 maana ilikuwa inalipa. alipoingia jamaa na kuongeza ushuru niliacha kabisa nlijikuta ushuru na kununua inafika mil 9 hadi 10 sasa nitauza ngapi nani atanipa mil 12 hakuna niliamua kuacha kabisa. ila ndo hivyo
Na kwy spares za magari na yenyewe ikoje kwa sasa
 
Sijawahi fanya biashara ya spea za magari ila nasikia ina changamoto sana maana magari ni mengi na aina yake kuuza ni kama kubahatisha hivi kinachokusaidia ni muingiliano wa matumizi ya spea
 
Ukitaka kuingiza gari bila kulipa kodi, agiza trekta. Hii ni zero rated. Unanunua tractor unaenda nalo kazini... Msimu wa kikimo, unalipeleka shamba.
Tatizo sio kutolipa kodi mkuu nazungumzia ukubwa wa kodi gari unanunua japan $2,00 kuipata inafika milion 14... Kodi iwe reasonable hata 20%-40% ya bei ya kununulia.
Pia je trekta hulipi kodi kabisa au kuna baadhi ya kodi tuu unasamehewa??
 
Tatizo ni kuwa tumelalamika sana humu lakini hakuna hata wa kuliongelea bungeni na kulitolea ufafanuzi yakini
Kweli kuna wadau walishaongelea hili na kusema huenda ni kutokutaka tuwe dampo la used car ingawa halina mashiko sana
Na wengine wanasema hatuna barabara za kumudu magari mengi ambalo hilo pia halina ukweli
Tunahitaji majibu ya kushiba ni kwanini kodi iwe kubwa hivyo?

Bora wangepandisha kodi kwenye road tax na mengine kuliko ushuru wa bandari
 
Hoja aina mashiko hii. Wacha magari yawe mengi Kama simu, serikali itapata faida kwy petrol na vipuri na tasnia nzima ya utengenezaji
Mimi naona kama kodi itapungua au itakua rahisi kwa kila mtu kuingiza gari let say kwa sasa wa tz tuko milioni 50 haya tutoe watoto hapo kama milioni10 sasa imagine magari yawe milioni 40 je tutayaendeshea wapi? hivi hivi tu foleni kibao sasa ndio yawe mengi kama simu tutaendeshaje? Na kama hayataendesheka serikari itapataje kodi kwa upande wa mafuta? itapata tu kodi ya kuingizia magari nchini. Haya ukiangalia na hasara zingine pollution etc hata mabasi watu hawatapamda maana kila mtu ana gari yake kwa hiyo hata kodi kwa wafanyabishara wa magari itapungua wacha iwe hivi hivi tu bana tupunguze msongamano na balance katika biashara.
 
roho nzuri
 
Makadirio yako hayana uhalisia sio kila mtu mzima anamudu kununua gari tunacho sema ushuru uwepo ila uwe reasonable huwez kuweka ushuru mkubwa unaozidi gharama ya manunuzi ya gari pamoja na freight charges mpaka linafika.

Tungekua na viwanda sawa ila kwa hili linaumuza sana yaan kodi inadouble bei ya gari sio sawa maana wakiounguza bei wengi watamudu na mapato ya mafuta licence itaongezeka pia soko la vipuri litaongeza wigo wa kodi
Tunaviwanda vya magari sasa tukiachia tu magari yaingie hovyohovyo tutauwa viwanda vyetu. Tena napendekeza waongeze kodi iwe sawa na bei ya gari mpya. Tukilinde Kiwanda chetu cha nyumbu
 
Makadirio yako hayana uhalisia sio kila mtu mzima anamudu kununua gari tunacho sema ushuru uwepo ila uwe reasonable huwez kuweka ushuru mkubwa unaozidi gharama ya manunuzi ya gari pamoja na freight charges mpaka linafika.
Hoja yako ni sawa ila nilikua narespond kwa jamaa hapo juu aliyesema angependa magari yawe mengi kama simu na nnavyojua kwa sasa karibu kila mtanzania anamiliki simu sasa fikiria idadi ya simu ndio iwe idadi ya magari itakuaje hapo
 
Tatizo kubwa la ushuru wa magari ni pale kwenye excise duty due to age pale ndo hela nyingi inatafunwa na uchakavu yani theory ile ni yabkipumbavu sana sababu haizingatii uhalisia mfano watanzania wengi wanamudu kununua magari ya kuanzia 2002-2010 sasa hapo kuna kua na uchakavu unaofanya bei uliyonunulia gari kuzidi ime umenunua gari $2500-3000CIF unakuja kulipa kodi $2900 au 3500 ndo jambo gani pia hata ukisema ununue gari ya kuanzia 2015 hadi 2019 bado kodi na gharama yake ipo juu sana yani hakuna unafuu wowote ule ni upuuzi mtupu sababu Tanzania hakuna kiwanda cha magari kinacholindwa
 
Kwa maisha ya Sasa gari Sio luxury Ni necessity serikali ipunguze tu Kodi za magari watu wengi wanunue itapata Kodi nyingi kupitia mafuta yanayojazwa kwenye hayo magari ambapo Kodi ziko kibao kwa kila lita
 
Kwani kipindi hiki kwenye Calculator ya TRA nini kimeongezeka mpaka hiyo kodi ikaruka hivyo? Au ni zile short cut zimepanguliwa tu.... Halafu wanaolalamika ni walewale wauzaji na madadali wakati kwa wanunuzi bei bado ina range mulemule tu....
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom