Nini athari za kupunguza kodi ya kuingiza magari nchini?

Nini athari za kupunguza kodi ya kuingiza magari nchini?

Serikali inashindwa nini kuwasiliana na wauzaji? Ingetengeneza sub agency ya kushughuliakia suala hilo ili kuondoa vilio vya waagizaji magari. Doesnt make sense gari inaagizwa kwa dola 3000 (CIF) ikija bandarini unalipia karobia 20M. Kosi pekee inaenda dola 8000.
Ni waahenz tuu wale wamekalia uroho wa kodi
 
Tatizo kubwa kwa Tanzania ni kodi kubwa kiasi cha kufanya wengi kushindwa ama kuagiza magari toka nje au kushindwa kuyakomboa bandarini. Kwa nini serekali isiweke mfumo rahisi wa kulipia mapato ya kuagiza gari toka nje na iwe rahisi kama kodi ya kuagiza simu au nguo?? Najua ni rahisi ila sijui kwa nini wamefanya vile.

Ipo CALCULATOR ya TRA lakini kuitumia kwa mtu asiye mzoefu inakuingiza majanga ya kushindwa Kulipia gari bandarini. Napendekeza iwe hivi.

Magari yaliyotengenezwa mwaka flan hadi flan kodi yake iwe kwenye % let say 2000 kurudi nyuma =50%
2001-2009=35%
2010-2019=20%

Garama nyingine ziwe kwenye mfumo wa % ili iwe rahisi kwa mwananchi kujikadiria garama halisi kabla ya gari kufika bandarini.

Unaweza kupunguza garama za kuagiza gari kwa 25% ikapelekea mapato kuongezeka kwa 150% ambayo yatatokana na umunuzi wa mafuta, Ajira, leseni, vipuri, vibali mbalimbali, kuimarika kwa usafiri hasa vijijini,

Kuwe na utaratibu wa mwananchi kulipia garama zote na gari kabla ya kufika bandarini. ikifika bandarini unaichukua tuu. Hii itaepusha kubambikiwa garama zisizoeleweka. Ukishalipia garama zote gari ikafika bandarini garama nyingine zitazokuja baadae hazikuhusu labda kama ulidanganya taarifa halisi za gari.

Wigo wa msamaha wa kodi uingezwe kidogo hadi kwenye magari ya usafirishaji kama Canter, Fuso na Pikup. Hizi ziwe zinafanya kazi maeneo ya vijijini na mikoani katika kusaidia kusafirisha mizigo na mazao ya wakulima na kuinua kilimo na uchumi wa vijijini. Hapa tunaweza kuweka kuweka mfumo gari hizi kupewa special namba na kupakwa rangi maalumu na zipewe maeneo maalumu ya kufanya kazi hasa vijijini na mashambani. Hii itainua kidogo na kupunguza adha ya usafurishaji wa mazao.

NB: kuweka kodi kubwa kwenye magari yaliyetengenezwa miaka mingi kwa kigezo cha kuchafua mazingira sio SAWA kwa kua magari yanachafua mazingira kwa kiwango kidogo kuliko viwanda na shughuli nyingine za binadamu. Tanzania sio mchafuzi wa maIngira, Pia magari yalitotengnezwa kwati ya 1990-1999 kama pikup,canter, na malori ya saizi ya kati mi imara kuliko ya 2005+ pia yanastahimili sana mazingira ya Tanzania ambapo barabara ni mbovu hivyo kurahisisha shughuli za maendeleo kama usafirishaji wa mazao toka mashambani na shughuli mbalimbali za maendeleo.

Nawasilisha
Nimependa sana maoni yako. Na umezungumza kitu very positive.

Unfortunately, hawa tunaowaita ni viongozi wanapumbazika na mishahara na marupurupu mazuri tunayowapatia kwa damu, jasho na nguvu zetu za kimasikini ambazo tunahangaika kila uchao ila bado wanatudharau mbwa hawa.
 
Kabla hawajalifanyia kazi wazo lako wajenge shortcut way zote za jijin dar es Salaam na za kuconect mikoa ili isije kuwa usumbufu mkubwa kuliko uwo wa bandalini apo


Hahaha Nachangia tu Mzee
Hata wakishusha kodi watu wenye uwezo wa kumudu kumunua magari sio wengi kiasi hicho hadi waweze kuleta changamoto ya kimiundo mbinu hivyo.
 
Hakuna ujanja ujanja kodi ya magari inajulikana kua ipo juu kuliko uhalisia wake!! Serekali inaamini ukiwa na hela ya kununua gari wewe ni tajiri sana hizi ni fikra za miaka ya 70 na 80 sio miaka ya sasa!! Magari yakiwa mengi barabarani kodi ya serekali inaongezeka hasa kwenye mafuta, vipuri,maegesho,ajira za madereva na gereji. Waache fikra za kmaskini
True.... Na kama kutatokea msongamano tutatafuta namna na mbinu ya kusolve hilo tatizo.
 
Mimi naona kama kodi itapungua au itakua rahisi kwa kila mtu kuingiza gari let say kwa sasa wa tz tuko milioni 50 haya tutoe watoto hapo kama milioni10 sasa imagine magari yawe milioni 40 je tutayaendeshea wapi? hivi hivi tu foleni kibao sasa ndio yawe mengi kama simu tutaendeshaje? Na kama hayataendesheka serikari itapataje kodi kwa upande wa mafuta? itapata tu kodi ya kuingizia magari nchini. Haya ukiangalia na hasara zingine pollution etc hata mabasi watu hawatapamda maana kila mtu ana gari yake kwa hiyo hata kodi kwa wafanyabishara wa magari itapungua wacha iwe hivi hivi tu bana tupunguze msongamano na balance katika biashara.
Watu wangapi unaowajuwa wewe wenye uwezo wa kununua magari.... Wewe katika raia wote wa Tanzania unadhani wote wanaweza kuendesha magari, wote wanapendelea kero za kumiliki gari, wote hawapandi daladala, wote ni wanaume kusema hakuna wale wanawake wanaondoka na magari ya waume wao.....?!
 
Hoja yako ni sawa ila nilikua narespond kwa jamaa hapo juu aliyesema angependa magari yawe mengi kama simu na nnavyojua kwa sasa karibu kila mtanzania anamiliki simu sasa fikiria idadi ya simu ndio iwe idadi ya magari itakuaje hapo
Unatakwimu za tra ndugu. Unaposema kila mtanzania kuna nyumba huko vijijini simu ni moja katika kaya ya watu 20.....

Na hata hapa dar mara kibao huwa nakutana na mafundi ujenzi, wafanya usafi hawana simu hadi unamgombeza kuwa anakuwaje hana mawasiliano hadi unamtafuta kwa shida.
 
Tatizo kubwa la ushuru wa magari ni pale kwenye excise duty due to age pale ndo hela nyingi inatafunwa na uchakavu yani theory ile ni yabkipumbavu sana sababu haizingatii uhalisia mfano watanzania wengi wanamudu kununua magari ya kuanzia 2002-2010 sasa hapo kuna kua na uchakavu unaofanya bei uliyonunulia gari kuzidi ime umenunua gari $2500-3000CIF unakuja kulipa kodi $2900 au 3500 ndo jambo gani pia hata ukisema ununue gari ya kuanzia 2015 hadi 2019 bado kodi na gharama yake ipo juu sana yani hakuna unafuu wowote ule ni upuuzi mtupu sababu Tanzania hakuna kiwanda cha magari kinacholindwa
Inatia hasira sana mkuu.... Hapa unaongea hivi nimeuma meno huku kwa hasira kwa maana naona ni unaingea yale niliyonayo moyoni.
 
Kwani kipindi hiki kwenye Calculator ya TRA nini kimeongezeka mpaka hiyo kodi ikaruka hivyo? Au ni zile short cut zimepanguliwa tu.... Halafu wanaolalamika ni walewale wauzaji na madadali wakati kwa wanunuzi bei bado ina range mulemule tu....
Haupo serious na maisha wewe....
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom