Nini asili ya jina Tanganyika na Nani alilitunga jina hili?

ni tanga+nyika, nyika ikimaanisha pori(bara kipindi hiko) na tanga ni pwani!
hii ni kutoka kwa babu yangu binafsi nilimuamini ndo maana nikachangia kwny uzi huu

neno tanga lina maana ya shamba hii ilitumiwa na mababu zetu waliokuwa wakiishi hasa maeneo ya pangani enzi za ukoloni na sasa walikuwa wakienda shamba kulima na shamba waliita tanga ambapo kwa ss ndio tanga mjini.....pwani illitwa sahil kama ckosei!..na neno nyika lina maana ya pori...kama kuna mwenye uelewa zaidi ya hapa tuelimishane..akhsante
 
Tanga = kutembea bila kujua unakwenda wapi
Nyika = Pori
TangaNyika=Mtembea na Pori
 
Kumekuwepo na maswali mengi juu ya jina la tanganyika na baadaye tanzania
sisi twajua yakwamba jina tanzania lilitokana na munganiko wa nchi mbili tanganyika na zanzibar,
sasa swali nikwamba Tanganyika ilitokana na nini?
Na nini maana ya Tanganyika?
Na ninani aliyependekeza jina Tanganyika?
 
Asili ya Jina Tanganyika bila kupotosha ukweli. Neno Tanganyika limetokana na uwepo wa ziwa Tanganyika lililopo magharibi mwa nchi yaani Mkoa wa Kigoma na Rukwa. Kabila la WAHA waishio Mkoani Kigoma wao wanaweza kuwa na majibu maana ya neon Tanganyika. Bahati mbaya, leo tunahitaji kujua asili ya neno hilo tunakimbilia kumuuliza Mchaga, Mzaramo, Mgogo, Mhehe na Mnyakyusa. Ni busara waulizwe wenyeji wa maeneo hayo. Nakumbuka hata Nyerere alipoulizwa ni kwa nini Tanzania Bara iliitwa Tanganyika, na yeye alishangaa akajibu, hajui wakoloni walilitoa wapi. Suala hapa sio wakoloni walilipata wapia, ebu tuwaulize Waha au Wafipa neno Tanganyika kwao lina maana gani. Tena tunataka tusiitwe Tanzania Bara bali tuiitwe Tanganyika.
 
Tanganyika ni eneo lililohusisha mkoa wa Kigoma, Tabora na sehemu za Rukwa. Hii habari niliipata huko Kigoma. Mzee mmoja anasema eneo lingine la Tanganyika ya leo liliitwa Azania. Hivyo Tz Bara =Tanganyika +Azania.

Researchers watujuze.
 
Thread ya namna hii nadhani imeshawahi kuwepo hapa JF ila sikumbuki ni mwaka gani...
Kama kumbukumbu zangu zipo sahihi, basi kuna wakati nimeshawahi kusikiliza hotuba ya Baba wa Taifa, JK Nyerere...
Katika hotuba hiyo Julius alitamka ya kwamba, asili ya neno Tanganyika ni samaki wawili wapatikanao katika Ziwa hilo...
Samaki hao walipewa majina ya TANGA na mwingine alikuwa na jina NYIKA, na muunganiko wao ndio jina TangaNyika...
Mmoja wa samaki hao kuna wakati alikuwa akitumika kama nembo katika kifungashio cha chumvi ile ya Uvinza...

Kulingana na Wikipedia, wao wameandika hivi:

The name "Tanganyika" is derived from the Swahili words tanga ("sail") and nyika ("uninhabited plain", "wilderness"). It might, therefore, be understood as a description of using Lake Tanganyika: "sail in the wilderness".[SUP][1][/SUP]
 
Neno Tanganyika linamaanisha 'nyika ya Tanga'. Watembezi 'explorers' wa kizungu waliokuja wakti wa zamani, walishukia Tanga, na wakaingia bara kutafuta chanzo cha mto Nile. Maeneo yale waliyotembea wakayaita 'nyika ya Tanga' au Tanganyika. Soma zaidi hapa:

Tanganyika Territory - Wikipedia, the free encyclopedia

Yaweza kuwa..........Kwa watu wa Tanga (na baadhi ya Wapare ambao awali walikuwa sehemu ya mkoa wa TANGA) mtu yeyote atokaye eneo nje ya la kwao huitwa Mnyika, yaani mtu wa nyika ambayo maana yake ni pori. Wajerumani ndio walio anza kulitumia neno Tanga & Nyika (kutofautisha TANGA na maeneo mengine waliyoyatawala wakati huo) awali kabla ya kuliunga na kuwa Tanganyika. Ziwa lile lilipewa jina baada ya hapo. Nina hakika wenyeji wa Kigoma wana jina lao kwa ziwa lile!
 
kidogo@dingswayo@unajaribu kuleta maana kamili,
ebu tuendelee kuchambua,

Neno Tanga laweza kuwa lilianzia kwa Wabondei ambao kwa Nt'hanga ni shambani na inasadikiwa kuwa maeneo ya TANGA ya leo yalikuwa mashamba makubwa ya minazi ambapo Wabondei walikuwa wakilima pasi na kuishi (wakienda na kurudi kwao Bonde)....ukimsikia Mbondei anasema " Naita Nt'hanga'' ujue anamaanisha naenda shamba....
 
Neno Tanganyika linamaanisha 'nyika ya Tanga'. Watembezi 'explorers' wa kizungu waliokuja wakti wa zamani, walishukia Tanga, na wakaingia bara kutafuta chanzo cha mto Nile. Maeneo yale waliyotembea wakayaita 'nyika ya Tanga' au Tanganyika. Soma zaidi hapa:

Tanganyika Territory - Wikipedia, the free encyclopedia
Tanganyika Tanga+Nyika
1.Tanga-zunguka,angaika
2.Nyika-Msitu

Unfortunately definition hii ambayo imekuwa inatumika kwa muda mrefu sana kuhusiana na jina Tanzanyika inapotosha. Mara baaya ya vita ya dunia ambapo Germany East Africa ilipotoweka, waingereza hawakutaka kuiita eneo hili kuwa British East Africa hivyo wakadakia jina Tanganyika mwaka huo wa 1922 kwa kutania kuwa ni nyika iliyokuwa nyuma ya Tanga, lakini jina Tangayika lililikuwepo tangu kabla ya mjerumani likiwa ni jina la hilo Ziwa Tanganyika. Nikipata nafasi nitatafiti kujua ni nani aliyeliita jina hilo lakini Speke na Burton walipofika ziwani pale mwaka 1859 waliandika kuwa wamefika kwenye Ziwa Tanganyika, ikiwa na maana kuwa walilikuta likiwa linaitwa vile. Angalia article hii ya Speke aliyoandika mwaka 1859 kuhusiana na ziwa hilo. Kwa hiyo jina la Tanganyika linatokana na ziwa Tanganyika siyo Nyika za Tanga.
 
Attachments

  • speke-1859-blackwoods-nile.pdf
    6.8 MB · Views: 102

kwahiyo hili ziwa Tanganyika lilikuwa likiitwa hivyo toka mwaka gani?
Maana hata jina la ziwa limetokana na watu kulipa jina,
 
Neno Tanganyika linamaanisha 'nyika ya Tanga'. Watembezi 'explorers' wa kizungu waliokuja wakti wa zamani, walishukia Tanga, na wakaingia bara kutafuta chanzo cha mto Nile. Maeneo yale waliyotembea wakayaita 'nyika ya Tanga' au Tanganyika. Soma zaidi hapa:

Tanganyika Territory - Wikipedia, the free encyclopedia

Kwa hiyo comrade unatuambia kwamba jina Tanga lilikuwepo kabla ya jina Tanganyika? Na kama ni hivyo sasa mkoa wa Tanga ulikua uko ndani ya nchi inayoitwaje?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom