Nini 787 dreamliner na tugemee nini?

Nini 787 dreamliner na tugemee nini?

Kama kawaida yetu watanzania,kama kawaida yetu waafrika tuishio chini ya jangwa na sahara kwakweli Tanzania ilikuwa haina haja ya kununua hii Boeing 787 Dreamliner,tulikuwa tunatakiwa tujikite kwa nguvu zetu zote katika kukabili usafiri wa ndege wa ndani(local) ya nchi,kuliko kujingiza katika kutaka kusafiri nchi ya nchi..

Nimemsikia Raisi akisema hiyo Boeing 787 Dreamliner itafanya safari za kwenda India,Thainland nk,hivi kweli ATC inaweza kushindana na mashirika kama Emirates na Qatar mashirika ambayo yamewagaragaza mashirikamakubwa makubwa kama KLM,Lufthansa nk..

Hao watalii wanao wazungumza tulitakiwa tusubiri akina Emirates,Turkish airline,Qatar,Klm na mashirika mengine watumwagia hapa Tanzania,Halafu ATC inawasambaza watalii ndani ya Tanzania kwa ndege zetu,bomberdia ingelifaa sana kwa kazi hiii,mdogo mdogo baada ya kudhidhibiti safari za ndani,tungelianza kusafirisha wasafiri nchi jirani, baadae ndio tungeliamua kufikiria kuruka nje ya Afrika..

Raisi Kakurupuka,ataitia nchi katika hasara,/////Unajua shirika kubwa kama KLM kwa sasa limejikita Zaidi katika safari za ndani za mji kwa mji kuliko masafari marefu ili kuepusha hasara,kwanini ATC isiigie mfano wa KLM!?
Lengo kubwa la kununua hizi ndege hasa hii kubwa inaonekana ilikuwa ni kujijenga kisiasa na ndio maana imeandikwa hapa kazi tu.

Sidhani kama walijipa muda wa jinsi gani ya kufufua hili shirika kibiashara bali inaonekane waliwaza kulifufua kisiasa zaidi na ndio maana hata hii ndege imepokelewa kisiasa wakiamini wanawakomoa wapinzani na ndio maana pia walielekeza vijembe kwa wapinzani.

Si ajabu sasa ndio wanaumiza vichwa ni namna gani watamudu kuendesha hili shirika na hususani hiyo ndege kubwa na hizo zingine zinazotarajiwa kuwasili siku za usoni.

Wakati wao wanadhani zile mbwembwe zilikuwa ni za kutuma ujumbe kwa upinzani, ni mbwembwe hizo hizo ambazoni wapinzani watakuja kuzitumia kama reference wakati wa kuwasuta na kuwakosoa.

Time will tell.
 
Kila kitu kina matatizo madogo madogo ni wakati wa kufanya kazi na kuacha majungu juu ya hili suala tusiwe na mihemko kwenye keyboard zetu. Haiingi akilini hata kidogo mtu hajui chochote kuhusu vyombo vya usafirishaji wa hata nchi kavu lakini anavyoshikilia bango hili swala la ndege tena kwa story za vijiweni utadhani ana uelewa juu yake, haya mambo tuwaachie wenye taaluma zao maana ndege ni ya Tanzania lakini kuna uangalizi uliofanyika kimataifa ili kuepuka madhara.
 
Ndege zinanunuliwa bila kufuata bajeti wala tender process.

Halafu kuna watu wanashangilia.
Ujinga ndio mtaji wa watawala
Mpaka sasa 1.5tl zimepigwa bila maelezo na watu wanaendelea kushangilia ndege
 
Tuwe tunaangalia na mazuri pia ya serikali yetu
Ukilitimba unaweza chelewesha maendeleo
Leo hapa ingefuatwa process huenda hadi magu anatoka tusingenunua hata ndege ya abiria kumi
Nchi inayojiendesha bila kufuata Sheria haina tofauti na Kijiwe
kama Sheria mbovu mko wengi simzibadilishe ni ujinga MTU anaedhani mzalendo kuwa ndio sheria
 
Hayo ni maneno ya wapinga maendeleo wote! Hata wakati wa Mwalimu Nyerere tulipokuwa tunajenga Reli Ya TAZARA, walisema mengi sana, hasa wakoloni na wapambe wao eti hii ni bamboo rail haitadumu mara hili mara lile ili mradi kuonyesha kujeli ya aina moja au nyingine ingawa walikuwa anajua ukweli kuwa reli hiyo "ni chuma cha pua" na silaha muhimu dhidi ya ukoloni. Na historia imewaumbua kama itakavyo waumbua watu wengi katika nchi hii wasiopenda kuuona ukweli wa uwekezaji wa aina hii. Ndege imefika jan, nyingine inakuja na picha zitazidi kupigwa - iwe mvua iwe jua iwe masika iwe el nino!
Shida wengi wenu mnadhani biashara ya ndege ni kama Daladala
 
Dogo huyo mfianchi has a point. Ngoja nikufumbue macho kidogo tu ili ujitambue kiakili...Fikiria hii ndege ikiwa na routes za kwenda India, Mecca, Marekani, Ulaya na sehemu zingine waendazo watanzania kama zile routes za wauza unga wetu enzi za Kikwete (Pakistan, Afghanstan, Uturuki, Ugiriki, China)….abiria badala ya kununua ticketi kwa mashirika mengine wananunua ATCL unafikiri tutakuwa wapi in a year or so? Mtanzania hata kama unawapeleka wazee wako Marekani hauna wasiwasi wa wao kupotea au lugha gongana kwani wako ndani ya ndege yao na wahudumu wanazungumza lugha yao ya asili. Usiwe mwepesi wa kupenda kufumbuliwa kila kitu, tumia akili yako wewe mwenyewe. Unajihaibisha kijana Dharra mpaka unatia kinyaa. Hawa Zitto, Lissu, Nape na Mange wanawalostisha tu kwa sababu wana agenda zao ambazo haziwasaidii nyinyi bali wao tu na familia zao, jitambue dogo. Ni hayo tu.
Wadangayika tunapenda sana Maisha yakufiirika na huu ndio mtaji wa watawala
 
Hizo changamoto ni za kawaida. Ni kama zilivyo kwa Airbus na hata aina nyingine za ndege za abiria!

Liliniumiza ni gharama za ununuzi aisee!

Yani dola Bilioni 32?
Hivi hii ni sawa na Bajeti ya wizara gani?
Sina taarifa lakini kutuambia Boeing wametumia dola bil 32 yaani shilingi trillion 64 kutengeneza dreamliner inatia mashaka.
F 35 Stealth fighter yenyewe mbali na kuwa the most expensive fighter jet, haifikii gharama hiyo. Aliyesema haya aweke sawa taarifa zake.
 
Muda utasema. Hesabu hazidanganyi. Faida na hasara ni hesabu. Hizi ndege si za raisi, wala hazijaandikwa jina lake. Labda kuna mahesabu ambayo wameyaona wewe huyaoni. Hivyo muda utaongea. Wasi wasi wangu tu ni kwamba kama upo sahihi basi taifa tutakuwa tumepoteza muda na rasilimali. Hope haupo sahihi. Kwangu mm nadhani ubinafsishaji ulikuwa ni kosa.
Mawazo kama haya ni mtaji mkubwa wa watawala mufilisi wee unashindwa kusema hadi muda ufike Unajua kiliponunuliwa kivuko kibovu na watu kuhoji unajua Kimepelekwa wapi....naleo mnataka watu wasiseme mpaka Financial Statement ipelekwe Jeshini
 
Budget ya Wizara ya Habari na budget ya wizara ya Mazingira! Hatariiii
Hizo changamoto ni za kawaida. Ni kama zilivyo kwa Airbus na hata aina nyingine za ndege za abiria!

Liliniumiza ni gharama za ununuzi aisee!

Yani dola Bilioni 32?
Hivi hii ni sawa na Bajeti ya wizara gani?
 
Budget ya Wizara ya Habari na budget ya wizara ya Mazingira! Hatariiii
Dah aisee...si wangechota kiasi wa visenti warekebisha "ighulu la mwitundah na Kuluzilambwa" na Nyayo za Mguu wa Yesu kule Nkinto Mkalama ili watalii wafike? ...hahahaaa
 
mwalimu jkn alipofariki aliletwa nchini na ndege ya Atc ile ilienda wapi? nani alishiriki kuuwa shirika la ndege nani analifufua kama kweli? mpango kazi ni upi ama mwanunua kwakuwa rwanda wanazo. mme scan mazingira?
Ile ndege iliharibika ikiwa uwanja wa ndege wa mwanza. Damage ilikuwa kubwa mno kiasi kwamba kutengenezeka ilikuwa ni ngumu.
Waliipeleka kwenye karakana iliyoko uwanja wa ndege wa mwanza.

Since then serikal haijawahi kutoa tamko lolote kuhusu hiyo ndege. Wakakaa kimya.

Kilichoua shirika ni sera ya ubinafsishaji.
Sera mbovu kuliko zote.
 
Mawazo kama haya ni mtaji mkubwa wa watawala mufilisi wee unashindwa kusema hadi muda ufike Unajua kiliponunuliwa kivuko kibovu na watu kuhoji unajua Kimepelekwa wapi....naleo mnataka watu wasiseme mpaka Financial Statement ipelekwe Jeshini
Hapa pia ni njia ya kusema. Ulitaka kama sikubaliani/nakubaliana na ununuzi wa ndege niite waandishi? Muda utasema ndio sababu hakuna unaloweza kufanya wewe kama wewe zaidi ya kutoa maoni. Au ulitaka tufanyaje zaidi ya kutoa maoni na kusubiri matokeo?
 
Mkuu kweli watalii watapanda ATC waiache Qatar na Emirates na mashirika mengine ya kimataifa,kwanini Raisi asijiimarishe Zaidi katika ndege za matumizi ya ndani ya nchi,ndege zinazokwenda masafa mafupi,..kama vile Bombardier!?
Magufuli akiondoka si na Hiyo Boeing itakuwa iko juu ya mawe,nani atalipia matengenezo ya hiyo ndege kama ndege inatembea kwa hasara..
Sawa boss lakini Sasa tufanyaje zaidi ya kusubiri kama upo sahihi tushuhudie hizo hasara? Kwa sababu hakuna la kufanya zaidi ya kutoa maoni, basi we wait and see who was right and who was wrong. Kuna msemo unasema if you don't like what a leader is doing, climb up. Overthrown his/her leadership and do what you blv is right. Kinyume na hapo Toa maoni then relax and watch the show.
 
Back
Top Bottom