Nini 787 dreamliner na tugemee nini?

Nini 787 dreamliner na tugemee nini?

Duuuuh. Uwezo wako wa akili mdogo sana. Hustahili kuandika chochote humu
Ungenisaidia niwe na uwezo wa akili walau kama wako kwa kunionesha nilipokosea na kupewa nishani ya uwezo mdogo sana wa akili ningeshukuru.

Ila kuishia kunizuia kuandika humu ni dhahiri wate mimi na wewe tunauwezo mdogo sana wa akili, angalau mimi najielwwa wewe ni severely abdnomal. Very retarded man!
 
Dream liner ni ndege mbovu zilizokataliwa duniani kote. Hivyo ni janga litakalotuletea mabalaaaaa
Aliyelinunua atapata taaabu sanaaa...
ndo mana me nawaza tu kuwa WATAPATA TAAABU SANA na msiwastue haya makosa yanayowajia tuwaache tu na ''kinyumenyume'' chao likilipuka ni lao
 
Mtegemee kupata taabu sana kwa umbeya wenu. Mngekuwa na akili za kuangalia financial projections na profitability mngewasaidia dada zenu wanaouza kwa bei ya hasara sasa hivi. Mtapata taabu sana nasema.
anza wewe kumsaidia dadako coco
 
mimi sina shida na uwepo wa ndege nyingi za ATCL
tatizo ni jinsi zinavyonunuliwa na ukizingatia hadi sasa hatujaona financial statements za bombadier ili tuproject performance ya dreamliner
Financial statements kutoka ATCL? Itakubidi usubiri mpaka awamu ya sita.
 
"mfano mgeni huyu anatumia lita 6,811 kwa saa" hili jambo unauhakika nalo, kutoka USA mpaka TZ itatumia lita ngapi? kwa muda wa masaa 13 hadi 16? mnapoongea muwe na uhakika. unajua hiyo ni Sh ngapi mafuta tu. hapa kunauongo kabisaaa.
Bado hujasaidia Kama kasema kweli au uongo.... Ungetuambia saa moja inakula lita hizi na siyo alivyosema mleta uzi.....
 
Hakuna mafanikio yaliyokuja lelemama, ili ufanikiwe lazima uwetayari kukumbana na magumu.

lkn pia lengo hasa si biashara ya ndege bali ni utalii mfano kama ndege italeta hasara ya 300bil huku imekuza utalii na tukavuna mfano tr 7 from let say 1tr hiyo itakuwa ni hasara au faida?

akili za kuambiwa.
 
Kuna sababu nyingine ya kufikia conclusion kuwa Zimepitwa na wakati au ni kwa sababu ya Marekani kuondoka?
Sababu kubwa na ya msingi, ambayo hata serikali yetu iliishaikubali na kuitekeleza katika zoezi zima la ubinafsishaji, ni kwamba, serikali kazi yake kubwa ni kuhakikisha nchi ina mazingira mazuri ya kufanya biashara, si serikali kujiingiza katika kufanya biashara.

Hususan kwa makampuni ambayo yanaleta hasara.

Ndiyo maana tukabinafsisha mashirika mengi ya umma, CCM wakasema wanataka kubinafsisha mashirika, hususan yaliyokuwa yanaendeshwa kwa hasara.

Cha ajabu wamebinafsisha yaliyokuwa yanaendeshwa kwa faida (NBC, Container Terminal ya Bandari) wakati makampuni yanayoendeshwa kwa hasara kama ATC serikali bado inayakumbatia mpaka leo.

Serikali ya Marekani ilishagundua kwamba biashara ya mashirika ya ndege ni biashara kichaa, ni biashara ambayo serikali ikijiingiza, inajiingiza zaidi kwa kujionesha "na sisi tupo duniani" zaidi ya kufanya biashara yenye faida.

Ndiyo maana wenzetu wajanja wakajitoa katika biashara hiyo kama serikali, wakaachia sekta binafsi ipambane, serikali ikawa imeweka mazingira mazuri tu ya ushindani.

Sisi kwetu mpaka leo tunapiga mark time ya Vienna Waltz, one step forward, two steps back.

Leo tunataifisha, kesho tunabinafsisha, keshokutwa tunataifisha tena!
 
Hizo changamoto ni za kawaida. Ni kama zilivyo kwa Airbus na hata aina nyingine za ndege za abiria!

Liliniumiza ni gharama za ununuzi aisee!

Yani dola Bilioni 32?
Hivi hii ni sawa na Bajeti ya wizara gani?
Hizo ni sawa na trillion ngapi za kitanzania
 
Wana Jukwaa. Ni jana tu tumetoka kushuhudia kuwasili kwa ndege yetu inayoitwa Boeing 787 dreamliner. Wengi wetu nadhani bado hatufahamu kwa kina ni nini hasa kimewasili na mategemeo ni yepi katika kukuza uchumi wa Taifa hili.

Hii ni ndege ambayo imeundwa rasmi na kampuni na Boeing kutoka marekani kwa ajili ya kuruka umbali mkubwa (long haul aka long range) na ina uwezo wa kuchukua abiria kuanzia 242 hadi 335 kutegemea na jinsi utakavyopanga viti. Uzinduzi rasmi wa ndege hizi za dreamliner ulifanyika kwa mbwembwe nyingi mnamo July 8 2007. wadau mbali mbali wa safari za ndege duniani nzima walichangia katika ujenzi wa ndege hizi na mpaka kufika December 15, 2009 Dreamliner ilifanya safari yake ya kwanza na ilipofika mwaka 2011, Boeing walitangaza rasmi kuwa sasa Dreamliner zipo tayari kwa mauzo.

Kufikia October 26, 2011 Shirika la ndege la Japan liitwalo ALL NIPPON Airways walitoa oda yao ya kwanza kununua dreamliner, ndege hizi ziliingia kwenye ushindani rasmi wa kibiashara mnamo August 7 2014 na mpaka kufikia mwezi May mwaka huu 2018 Dreamliner tayari walishapokea oda ya ndege 1,377 nyingi zikinunuliwa na shirika la ndege la Marekani liitwalo American Airlines. Tangu kuundwa kwake na kuanza kuruka ndege hizi zimeshuhudia matatizo kadhaa ikiwemo kuripuka kwa battery (on board fire) wakati zinaruka kibishara. Hio ndio historia fupi ya mgeni wetu huyu dreamliner ambapo imewagharimu Boeing kiasi cha dola za Kimarekani billioni 32 kama gharama za matengenezo.

Kama nilivyoainisha kabla Boeing wamepokea oda zipatazo 1,377, lakini hadi sasa ni ndege 691 pekee ambazo tayri zimefika mikononi mwa wateja tokea kuundwa kwake.

January 8 2013 Shirika la ndege la Japana waligundua uvujaji wa mafuta katika moja ya dreamliner zake, na hivyo kusitisha safari ya kuelekea Boston ghafla wakati abiria wakiwa tayari kwa safari.
January 9 Shirika la ndege la Marekani walilalamika kutokea kwa cheche za moto (wiring problem) karibia kabisa na mahala ilipo battry.
January 13, 2013 ilitokea tena kuvuja kwa mafuta katika moja ya dreamliner.
January 14, 2014, Kuonekana kwa moshi wakati ndege ikiwa angani tena karibu kabisa na mahala ilipo battery. Na kasoro nyingi nyenginezo.

Tutegemee mwanzo mgumu sana. Kuwa na ndege moja inayoruka umbali mrefu (long haul) kuna ugumu wake hasa linapojitokeza suala la technical issues na ikalazimika ndege kutokuruka, kitu ambacho ni cha kawaida sana katika mambo ya ndege, na ndio maana wenzetu Ethiopian Airways wakajenga hoteli zao maalum (ziligharimu Dola milioni 91) kwa ajili ya abiria inapojitokeza kuchelewa kwa ndege kwa sababu za kiufundi (delay) kama hizi nilizoainisha hapo juu, inagwa wenzetu wapo na ndege nyingi za kuwasaidia kuhaulisha abiria na haraka inavyowezekana. Hapo tutegemee Delay, na hili lisipofanyiwa kazi linaweza kutugharimu baadae kibiashara, na pia kujiandaa na kipindi cha matengenezo ambapo ni lazima ndege isafiri (labda Ethiopia) kwa matengenezo ambayo nayo huchukua muda.

Ukifikiria hayo na mengine mengi utaona tuna safari ngumu sana ya kwenda kwa mfano mgeni huyu anatumia lita 6,811 kwa saa, piga hesabu Dar/Mwz ni mwendo wa saa moja na robo kwenda na kurudi masaa mawili na nusu utaona ugumu uliopo katika kuendesha ndege hii. Nilitegemea mapokezi ya kimya kimya na badala yake kutumia muda mwingi kuwaza na kuwazua kutafakari ni kwa vipi mgeni huyu ataleta faida. ITS NOT GONNA BE EASY FELLAS!!!
View attachment 805866
Hayo ni maneno ya wapinga maendeleo wote! Hata wakati wa Mwalimu Nyerere tulipokuwa tunajenga Reli Ya TAZARA, walisema mengi sana, hasa wakoloni na wapambe wao eti hii ni bamboo rail haitadumu mara hili mara lile ili mradi kuonyesha kujeli ya aina moja au nyingine ingawa walikuwa anajua ukweli kuwa reli hiyo "ni chuma cha pua" na silaha muhimu dhidi ya ukoloni. Na historia imewaumbua kama itakavyo waumbua watu wengi katika nchi hii wasiopenda kuuona ukweli wa uwekezaji wa aina hii. Ndege imefika jan, nyingine inakuja na picha zitazidi kupigwa - iwe mvua iwe jua iwe masika iwe el nino!
 
Tuwe tunaangalia na mazuri pia ya serikali yetu
Ukilitimba unaweza chelewesha maendeleo
Leo hapa ingefuatwa process huenda hadi magu anatoka tusingenunua hata ndege ya abiria kumi
Raisi alitumia kamati ya bunge ya fedha kuhidhinisha.... na ni sheria kufanya hivyo....
 
Hayo ni maneno ya wapinga maendeleo wote! Hata wakati wa Mwalimu Nyerere tulipokuwa tunajenga Reli Ya TAZARA, walisema mengi sana, hasa wakoloni na wapambe wao eti hii ni bamboo rail haitadumu mara hili mara lile ili mradi kuonyesha kujeli ya aina moja au nyingine ingawa walikuwa anajua ukweli kuwa reli hiyo "ni chuma cha pua" na silaha muhimu dhidi ya ukoloni. Na historia imewaumbua kama itakavyo waumbua watu wengi katika nchi hii wasiopenda kuuona ukweli wa uwekezaji wa aina hii. Ndege imefika jan, nyingine inakuja na picha zitazidi kupigwa - iwe mvua iwe jua iwe masika iwe el nino!

Hapa ni facts tu ukitaka meza hutaki tema. Hapo hakuna sijui kupinga maendeleo sijui Mwalimu nyerere ni facts tu mkuu baba Jungo Mota. The TAZARA project was built from 1970 to 1975 as a turnkey project financed and supported by China. na hio ndio fact.... TAZARA has faced operational difficulties from the start and was kept running by continued assistance from China, several European countries, and the United States. Huyo nyerere aliejenga TAZARA yupo wapi hapo
 
mimi sina shida na uwepo wa ndege nyingi za ATCL
tatizo ni jinsi zinavyonunuliwa na ukizingatia hadi sasa hatujaona financial statements za bombadier ili tuproject performance ya dreamliner
My friend ni uendawazimu kukimbilia kununua midege mikubwa wakati zilizopo hazijaxi abiria, na pia kwa safari za nje tusahau tu maana hatutapata wateja maana kikampuni chenyewe hakuna anaekijua,wenzetu wanapanda ndege kulingana na sifa zake,sasa haka kandege kamoja mfyuuuu.akili za kibashite zitatuvuruga sana
 
My friend ni uendawazimu kukimbilia kununua midege mikubwa wakati zilizopo hazijaxi abiria, na pia kwa safari za nje tusahau tu maana hatutapata wateja maana kikampuni chenyewe hakuna anaekijua,wenzetu wanapanda ndege kulingana na sifa zake,sasa haka kandege kamoja mfyuuuu.akili za kibashite zitatuvuruga sana

Mkuu celinawetu sio mbaya kuanza moja lakini nadhani kwanza wengejikita zaidi katika kutafuta soko la ndani na la kati kabla hawajaamua kuleta fleet kubwa na kutangaza tunaenda London, nenda kwanza Rwanda, Burundi, congo, Bujumbura, Nairobi, south africa na kwengineko Africa, Mungu ana makusudi yake kumfanya binaadamu awe anakuwa kwa stage, kuanzia kichanga kisichojiweza hadi kuwa mtu mzima kamili. Pale kuna funzo kubwa kwa chochote unachotaka kuanzisha katika mfumo wa kimaisha kwa mwanadaamu. Tusikimbilie tu kutaka makubwa.
 
Back
Top Bottom