Nini 787 dreamliner na tugemee nini?

Nini 787 dreamliner na tugemee nini?

Wana Jukwaa. Ni jana tu tumetoka kushuhudia kuwasili kwa ndege yetu inayoitwa Boeing 787 dreamliner. Wengi wetu nadhani bado hatufahamu kwa kina ni nini hasa kimewasili na mategemeo ni yepi katika kukuza uchumi wa Taifa hili.

Hii ni ndege ambayo imeundwa rasmi na kampuni na Boeing kutoka marekani kwa ajili ya kuruka umbali mkubwa (long haul aka long range) na ina uwezo wa kupakia abiri kuanzia 242 hadi 335 kutegemea na jinsi utakavyopanga viti. Uzinduzi rasmi wa ndege hizi za dreamliner ulifanyika kwa mbwembwe nyingi mnamo July 8 2007. wadau mbali mbali dunia nzima walichangia katika ujenzi wa ndege hizi na kufika December 15, 2009 Dreamliner ilifanya safari yake ya kwanza na ilipofika mwaka 2011, Boeing walitangaza rasmi kuwa sasa Dreamliner zipo tayari kwa mauzo.

Kufikia October 26, 2011 Shirika la ndege la Japan liitwalo ALL NIPPON Airways walitoa oda yao ya kwanza kununua dreamliner, ndege hizi ziliingia kwenye ushindani rasmi wa kibiashara mnamo August 7 2014 na mpaka kufikia mwezi May mwaka huu 2018 Dreamliner tayari wameuza ndege 1,377 nyingi zikinunuliwa na shirika la ndege la Marekani liitwalo American Airlines. Tangu kuundwa kwake na kuanza kuruka ndege hizi zimeshuhudia matatizo kadhaa ikiwemo kuripuka kwa battery (on board fire) wakati zinaruka kibishara. Hio ndio historia fupi ya mgeni wetu huyu dreamliner ambapo imewagharimu Boeing kiasi cha dola za Kimarekani billioni 32 kama gharama za matengenezo.

Kama nilivyoainisha kabla Boeing wamepokea oda zipatazo 1,377, lakini hadi sasa ni ndege 691 pekee ambazo tayri zimefika mikononi mwa wateja tokea kuundwa kwake.

January 8 2013 Shirika la ndege la Japana waligundua uvujaji wa mafuta katika moja ya dreamliner zake, na hivyo kusitisha safari ya kuelekea Boston ghafla wakati abiria wakiwa tayari kwa safari.
January 9 Shirika la ndege la Marekani walilalamika kutokea kwa chichi za moto (wiring problem) karibia kabisa na bettry.
January 13, 2013 uklitokea tena kuvuja kwa mafuta.
January 14, 2014, Kuonekana kwa moshi ndege ikiwa angani tena karibu kabisa na bettery. Na kasoro nyingi nyenginezo.

Tutegemee mwanzo mgumu sana. Kuwa na ndege moja inayoruka umbali mrefu (long haul) kuna ugumu wake hasa linapojitokeza suala la technical issues na ikalazimika ndege kutokuruka, kitu ambacho ni cha kawaida sana katika mambo ya ndege na ndio maana wenzetu Ethiopian Airways wakajenga hoteli zao maalum (ziligharimu Dola milioni 91) kwa ajili ya abiria inapojitokeza delay kama hizi inagwa wenzetu wapo na ndege nyingi za kuwasaidia kuhaulisha haraka inavyowezekana. Hapo tategemee Delay, na hili lisipofanyiwa kazi linaweza kutugharimu baadae kibiashara, na pia kujiandaa na kipindi cha matengenezo ambapo ni lazima ndege isafiri (labda Ethiopia) kwa matengenezo ambayo nao huchukua muda.

Ukifikiria hayo na mengine mengi utaona tuna safari ngumu sana ya kwenda kwa mfano mgeni huyu anatumia lita 6,811 kwa saa, utaona ugumu uliopo katika kuendesha ndege hii. Nilitegemea mapokezi ya kimya kimya na badala yake kutumia muda mwingi kuwaza na kuwazua ni kwa vipi mgeni huyu ataleta faida. ITS NOT GONNA BE EASY FELLAS!!!
View attachment 805866


HAPA UONGO MWINGI SANA
 
Dream liner ni ndege mbovu zilizokataliwa duniani kote. Hivyo ni janga litakalotuletea mabalaaaaa
Aliyelinunua atapata taaabu sanaaa...
Hahaha unachekesha sana brother. American airways , Luftansa, air france na mashirika mengine ya ulaya yasinge kuwa yanatumia hizi ndege.

Ndio toleo la mwanzon lilileta shidah, boeing walisitisha uzalishaji wa ndege hizi ili kutengeneza solution ya matatizo ya hiz ndege. Na walifanikiwa na zikarudi sokoni.

Kwa taarifa yako tu ethiopian airways wanazo, kenya airways wanazo, south african wanazo pia. So unaposema zilikataliwa fanya research upya
 
Mimi naomba tupeane moyo sio kuvunjana

Mtoa mada katoa angalizo based on facts ya hizo dream liner, suala la kutiana moyo ni la kwako, ila hixo ndio baadhi ya changamoto zake. Ikifanya kwa mafanikio ni sawa, ila ikizingua sijui Makonda atapiga risasi wangapi kwani hizo kelele zake sipati picha.
 
Watatembea na spana angani kama marubani walioileta walivyofanya! Au tatizo hilo halikutokea? Kama halikujitokeza, itachukua muda gani kujitokeza?
Routine maintenance huwa inafanyika kila ndege inapotua uwanjani. Si mpaka iharibike, check ups zote zinafanyika kabla ndege haijaondoka na hii inafanyika kila ndege inapotua..
Ni utaratibu wa dunia nzima.
 
Hizo changamoto ni za kawaida. Ni kama zilivyo kwa Airbus na hata aina nyingine za ndege za abiria!

Liliniumiza ni gharama za ununuzi aisee!

Yani dola Bilioni 32?
Hivi hii ni sawa na Bajeti ya wizara gani?

Mkuu kuna sehemu nimeielewa post yako namba moja, ila hapo kwenye manunuzi kwa $32b ni aidha huna taarifa za kutosha au unapotosha kwa makusudi. Mimi simkubali Magufuli kabisa na hata yeye anajua kwani ni member humu ndani, lakini katika kutomkubali kwangu sipendi kupotosha figure kwani inashusha heshima yako na kupoteza maana halisi ya ukosoaji. Rekebisha hapo kwenye bei ya ndege ili tunaokosoa tusionekane tunaendeshwa na chuki.
 
Hizo changamoto ni za kawaida. Ni kama zilivyo kwa Airbus na hata aina nyingine za ndege za abiria!

Liliniumiza ni gharama za ununuzi aisee!

Yani dola Bilioni 32?
Hivi hii ni sawa na Bajeti ya wizara gani?
Wizara ya ulinzi na usalama
 
mimi sina shida na uwepo wa ndege nyingi za ATCL
tatizo ni jinsi zinavyonunuliwa na ukizingatia hadi sasa hatujaona financial statements za bombadier ili tuproject performance ya dreamliner
Tumejifunza nini Kutokana Na Mikataba Mibovu na Ya Siri Nadhani Tuanzie Hapa
 
Hizo changamoto ni za kawaida. Ni kama zilivyo kwa Airbus na hata aina nyingine za ndege za abiria!

Liliniumiza ni gharama za ununuzi aisee!

Yani dola Bilioni 32?
Hivi hii ni sawa na Bajeti ya wizara gani?

Duuuuh. Uwezo wako wa akili mdogo sana. Hustahili kuandika chochote humu
 
Back
Top Bottom