Dharra
JF-Expert Member
- Jun 23, 2017
- 1,661
- 2,931
Wana Jukwaa. Ni jana tu tumetoka kushuhudia kuwasili kwa ndege yetu inayoitwa Boeing 787 dreamliner. Wengi wetu nadhani bado hatufahamu kwa kina ni nini hasa kimewasili na mategemeo ni yepi katika kukuza uchumi wa Taifa hili.
Hii ni ndege ambayo imeundwa rasmi na kampuni na Boeing kutoka marekani kwa ajili ya kuruka umbali mkubwa (long haul aka long range) na ina uwezo wa kuchukua abiria kuanzia 242 hadi 335 kutegemea na jinsi utakavyopanga viti. Uzinduzi rasmi wa ndege hizi za dreamliner ulifanyika kwa mbwembwe nyingi mnamo July 8 2007. wadau mbali mbali wa safari za ndege duniani nzima walichangia katika ujenzi wa ndege hizi na mpaka kufika December 15, 2009 Dreamliner ilifanya safari yake ya kwanza na ilipofika mwaka 2011, Boeing walitangaza rasmi kuwa sasa Dreamliner zipo tayari kwa mauzo.
Kufikia October 26, 2011 Shirika la ndege la Japan liitwalo ALL NIPPON Airways walitoa oda yao ya kwanza kununua dreamliner, ndege hizi ziliingia kwenye ushindani rasmi wa kibiashara mnamo August 7 2014 na mpaka kufikia mwezi May mwaka huu 2018 Dreamliner tayari walishapokea oda ya ndege 1,377 nyingi zikinunuliwa na shirika la ndege la Marekani liitwalo American Airlines. Tangu kuundwa kwake na kuanza kuruka ndege hizi zimeshuhudia matatizo kadhaa ikiwemo kuripuka kwa battery (on board fire) wakati zinaruka kibishara. Hio ndio historia fupi ya mgeni wetu huyu dreamliner ambapo imewagharimu Boeing kiasi cha dola za Kimarekani billioni 32 kama gharama za matengenezo.
Kama nilivyoainisha kabla Boeing wamepokea oda zipatazo 1,377, lakini hadi sasa ni ndege 691 pekee ambazo tayri zimefika mikononi mwa wateja tokea kuundwa kwake.
January 8 2013 Shirika la ndege la Japana waligundua uvujaji wa mafuta katika moja ya dreamliner zake, na hivyo kusitisha safari ya kuelekea Boston ghafla wakati abiria wakiwa tayari kwa safari.
January 9 Shirika la ndege la Marekani walilalamika kutokea kwa cheche za moto (wiring problem) karibia kabisa na mahala ilipo battry.
January 13, 2013 ilitokea tena kuvuja kwa mafuta katika moja ya dreamliner.
January 14, 2014, Kuonekana kwa moshi wakati ndege ikiwa angani tena karibu kabisa na mahala ilipo battery. Na kasoro nyingi nyenginezo.
Tutegemee mwanzo mgumu sana. Kuwa na ndege moja inayoruka umbali mrefu (long haul) kuna ugumu wake hasa linapojitokeza suala la technical issues na ikalazimika ndege kutokuruka, kitu ambacho ni cha kawaida sana katika mambo ya ndege, na ndio maana wenzetu Ethiopian Airways wakajenga hoteli zao maalum (ziligharimu Dola milioni 91) kwa ajili ya abiria inapojitokeza kuchelewa kwa ndege kwa sababu za kiufundi (delay) kama hizi nilizoainisha hapo juu, inagwa wenzetu wapo na ndege nyingi za kuwasaidia kuhaulisha abiria na haraka inavyowezekana. Hapo tutegemee Delay, na hili lisipofanyiwa kazi linaweza kutugharimu baadae kibiashara, na pia kujiandaa na kipindi cha matengenezo ambapo ni lazima ndege isafiri (labda Ethiopia) kwa matengenezo ambayo nayo huchukua muda.
Ukifikiria hayo na mengine mengi utaona tuna safari ngumu sana ya kwenda kwa mfano mgeni huyu anatumia lita 6,811 kwa saa, piga hesabu Dar/Mwz ni mwendo wa saa moja na robo kwenda na kurudi masaa mawili na nusu utaona ugumu uliopo katika kuendesha ndege hii. Nilitegemea mapokezi ya kimya kimya na badala yake kutumia muda mwingi kuwaza na kuwazua kutafakari ni kwa vipi mgeni huyu ataleta faida. ITS NOT GONNA BE EASY FELLAS!!!