Nini 787 dreamliner na tugemee nini?

Nini 787 dreamliner na tugemee nini?

Unasema hesabu hazidanganyi, ni kweli. Mimi pia nakubali hesabu hazidanganyi.Ingawa uhasibu na takwimu vinaweza kudanganya vizuri tu.

Tatizo JPM haheshimu hesabu, uhasibu wala takwimu, anaendekeza siasa.

Angeheshimu hesabu na uhasibu, angenunua ndege kwa hela za bajeti na kwa tenda iliyo wazi.

Ushajiuliza, kwa nini hakununua ndege kwa hela zilizopitishwa kwenye bajeti?

Sasa hivi inawezekana katupiga mamilioni ya dola humo na hakuna anayejua, kwa sababu kama nilivyosema, manunuzi yamefanyika nje ya bajeti na kwa kificho.

Na hata kama hajatupiga, kanunua kwa moyo mzuri tu, that is even worse. Ameacha wanaomsema wapate mwanya wa kusema kanunua ndege bila kufuata bajeti. Kwa sababu gani?

Hutakiwi kusema hesabu hazidanganyi wakati hata bei ya kununulia ndege ni ipi na mikataba ya matengenezo inaendaje hujui.

Ukitaka kuja kuangalia baada ya mwaka kama ndege inaenda kwa hasara au faida na Return On Investment tutarudisha lini, utapigaje hiyo hesabu?

Umeongelea habari nzima ya kufufua utalii.

Tatizo siasa nyingi bila nia ya kweli.

Tanzania tumeweka VAT kwenye utalii, tumewanyanyasa watalii mpaka ambao walishafanya booking na kulipia ikabidi walipe tena, with hardly a weeks notice, wakati wao malipo walishafanya kabla VAT haijawekwa.Juzi nimeona picha moja horrible reviews za airport yetu ina trend instagram. Huwezi kuvutia wataliikwa ndege nzuri halafu uwanja wa ndege choo mgogoro, huduma mbovu

Serikali yenyewe inaharibu utalii kwa kupandisha kodi kwa namna ya ajabu kwa muda mfupi bila hata taarifa nzuri na mpangilio, halafu inatakakupandisha utalii kwa kununua ndege?

Hao watalii wa kimataifa ndege washaziona sana hizo, kitu cha kufanya kuvutia utalii ni kuongeza huduma nzuri kwa watalii na kama kuna kupandisha kodi, kufanyike gradually, sio 185 at a go.

Soma chini hapo uone utekelezwaji mbaya wa VAT kwenye utalii ulivyoharibu utalii Tanzania.

Tanzania VAT hike sends safari industry into pandamoneum

Upheaval in the Safari Industry As the Impact of New Tanzania Vat Tax Starts to Bite – SafariBookings

New tourism tax roils Tanzania safari industry: Travel Weekly

Is VAT causing tourists to pick Kenya over Tanzania? see link --> {{title}} Tourism Update
What should be done then?
 
What should be done then?
Kwenye hili, rais alazimishwe aeleze.

1. Kwa nini kanunua ndege nje ya bajeti?
2. Kwa nini hajafuata utaratibu wa open tender?
3. Kwa nini haweki wazi gharama za manunuzi na mikataba ya ukarafati ya ndege?

Bila ku address haya masuala, tunaweza kushangikia kama ng'ombe anayeshangilia huku anapelekwa machinjioni.
 
How to do that? Suggestion ya Njia za kufanya haya
 
How to do that? Suggestion ya Njia za kufanya haya
Wabunge kazi yao ni nini? Hususan wa upinzani. Zitto ameshaanza kuizia mikataba.

Hata CCM nako kunatakiwa kuwe na upinzani wa ndani.

Waandishi wa habari waandije ubaya wa kushangikia bila kuchunguza. Wamulike haya mambo. Mara nyingi huwa kinachoonekana juu ni "tip of the iceberg". People are as honest as they are compelled to be. That is, if tge president is not compelled to be transparent by the people, he could pull all kinds of shoddy deals. Thats why we have checks and balance.

Wananchi wako wapi? Wahasibu wako wapi? Wachumi wako wapi?

Hii nchi haina watu wanaofikiri?

Watu hawana confidence? Wana woga?
 
Wana Jukwaa. Ni jana tu tumetoka kushuhudia kuwasili kwa ndege yetu inayoitwa Boeing 787 dreamliner. Wengi wetu nadhani bado hatufahamu kwa kina ni nini hasa kimewasili na mategemeo ni yepi katika kukuza uchumi wa Taifa hili.

Hii ni ndege ambayo imeundwa rasmi na kampuni na Boeing kutoka marekani kwa ajili ya kuruka umbali mkubwa (long haul aka long range) na ina uwezo wa kuchukua abiria kuanzia 242 hadi 335 kutegemea na jinsi utakavyopanga viti. Uzinduzi rasmi wa ndege hizi za dreamliner ulifanyika kwa mbwembwe nyingi mnamo July 8 2007. wadau mbali mbali wa safari za ndege duniani nzima walichangia katika ujenzi wa ndege hizi na mpaka kufika December 15, 2009 Dreamliner ilifanya safari yake ya kwanza na ilipofika mwaka 2011, Boeing walitangaza rasmi kuwa sasa Dreamliner zipo tayari kwa mauzo.

Kufikia October 26, 2011 Shirika la ndege la Japan liitwalo ALL NIPPON Airways walitoa oda yao ya kwanza kununua dreamliner, ndege hizi ziliingia kwenye ushindani rasmi wa kibiashara mnamo August 7 2014 na mpaka kufikia mwezi May mwaka huu 2018 Dreamliner tayari walishapokea oda ya ndege 1,377 nyingi zikinunuliwa na shirika la ndege la Marekani liitwalo American Airlines. Tangu kuundwa kwake na kuanza kuruka ndege hizi zimeshuhudia matatizo kadhaa ikiwemo kuripuka kwa battery (on board fire) wakati zinaruka kibishara. Hio ndio historia fupi ya mgeni wetu huyu dreamliner ambapo imewagharimu Boeing kiasi cha dola za Kimarekani billioni 32 kama gharama za matengenezo.

Kama nilivyoainisha kabla Boeing wamepokea oda zipatazo 1,377, lakini hadi sasa ni ndege 691 pekee ambazo tayri zimefika mikononi mwa wateja tokea kuundwa kwake.

January 8 2013 Shirika la ndege la Japana waligundua uvujaji wa mafuta katika moja ya dreamliner zake, na hivyo kusitisha safari ya kuelekea Boston ghafla wakati abiria wakiwa tayari kwa safari.
January 9 Shirika la ndege la Marekani walilalamika kutokea kwa cheche za moto (wiring problem) karibia kabisa na mahala ilipo battry.
January 13, 2013 ilitokea tena kuvuja kwa mafuta katika moja ya dreamliner.
January 14, 2014, Kuonekana kwa moshi wakati ndege ikiwa angani tena karibu kabisa na mahala ilipo battery. Na kasoro nyingi nyenginezo.

Tutegemee mwanzo mgumu sana. Kuwa na ndege moja inayoruka umbali mrefu (long haul) kuna ugumu wake hasa linapojitokeza suala la technical issues na ikalazimika ndege kutokuruka, kitu ambacho ni cha kawaida sana katika mambo ya ndege, na ndio maana wenzetu Ethiopian Airways wakajenga hoteli zao maalum (ziligharimu Dola milioni 91) kwa ajili ya abiria inapojitokeza kuchelewa kwa ndege kwa sababu za kiufundi (delay) kama hizi nilizoainisha hapo juu, inagwa wenzetu wapo na ndege nyingi za kuwasaidia kuhaulisha abiria na haraka inavyowezekana. Hapo tutegemee Delay, na hili lisipofanyiwa kazi linaweza kutugharimu baadae kibiashara, na pia kujiandaa na kipindi cha matengenezo ambapo ni lazima ndege isafiri (labda Ethiopia) kwa matengenezo ambayo nayo huchukua muda.

Ukifikiria hayo na mengine mengi utaona tuna safari ngumu sana ya kwenda kwa mfano mgeni huyu anatumia lita 6,811 kwa saa, piga hesabu Dar/Mwz ni mwendo wa saa moja na robo kwenda na kurudi masaa mawili na nusu utaona ugumu uliopo katika kuendesha ndege hii. Nilitegemea mapokezi ya kimya kimya na badala yake kutumia muda mwingi kuwaza na kuwazua kutafakari ni kwa vipi mgeni huyu ataleta faida. ITS NOT GONNA BE EASY FELLAS!!!
View attachment 805866
Tuikatekateee waiuzeee scraper mkuuu...
 
Sina taarifa lakini kutuambia Boeing wametumia dola bil 32 yaani shilingi trillion 64 kutengeneza dreamliner inatia mashaka.
F 35 Stealth fighter yenyewe mbali na kuwa the most expensive fighter jet, haifikii gharama hiyo. Aliyesema haya aweke sawa taarifa zake.
Kama huna taarifa kamili ni bora ukakaa kimya.
 
Wabunge kazi yao ni nini? Hususan wa upinzani. Zitto ameshaanza kuizia mikataba.

Hata CCM nako kunatakiwa kuwe na upinzani wa ndani.

Waandishi wa habari waandije ubaya wa kushangikia bila kuchunguza. Wamulike haya mambo. Mara nyingi huwa kinachoonekana juu ni "tip of the iceberg". People are as honest as they are compelled to be. That is, if tge president is not compelled to be transparent by the people, he could pull all kinds of shoddy deals. Thats why we have checks and balance.

Wananchi wako wapi? Wahasibu wako wapi? Wachumi wako wapi?

Hii nchi haina watu wanaofikiri?

Watu hawana confidence? Wana woga?
Kinadharia inawezekana upo sawa. Ila ukweli hata wewe unauelewa, namna Jamii ya waTz tunavyoishi, mambo tunayoendekeza na mtindo wetu wa kukosoa serikali, labda kama una suggest tubadilike na hiyo si kazi rahisi au ndogo.
 
Hususan kwa sababu RC kashasema wazi atawashughulikia wasiomuimbia mapambio muheshimiwa.

Hivibwatu wazima na ndevu zao wanakaangalia hako katoto kanawatisha, kwa sababu ya cheo cha serikali?
 
Hususan kwa sababu RC kashasema wazi atawashughulikia wasiomuimbia mapambio muheshimiwa.

Hivibwatu wazima na ndevu zao wanakaangalia hako katoto kanawatisha, kwa sababu ya cheo cha serikali?
Hahaha. Nadhani kwa sentensi yako tupo on the same side kwa sasa. Kusubiri muda utoe tathmini yake.
 
Sawa boss lakini Sasa tufanyaje zaidi ya kusubiri kama upo sahihi tushuhudie hizo hasara? Kwa sababu hakuna la kufanya zaidi ya kutoa maoni, basi we wait and see who was right and who was wrong. Kuna msemo unasema if you don't like what a leader is doing, climb up. Overthrown his/her leadership and do what you blv is right. Kinyume na hapo Toa maoni then relax and watch the show.
Mkuu,maamuzi ya wafrika wote yamegubikwa na hisia kuliko kuangalia uhalisia wa jambo husika,Tanzania ilikuwa haina haja kununua ndege inayotumia dollar za kimarekani 13,000$ kwa saa,Tanzania inahitaji kuimaimarisha usafiri wa Anga wa ndani,halafu ndio ingekurupuka kununuahiyo Boeing..

Leo nimesima ya "Article" moja ya jamaa aliebobea katika mambo ya Anga anaeitwa Tomas Chlumecky,nafikri huyu jamaani mmarekani..Jamaa amesema hiyo ndege inagharimu dolaa za Kimarekanin 30,000 kwa kupaki kiwanjani,halafu inagharimu dollar za kimarekani 15,0000 kwa saa kama iko angani,hiyo ndege inahitaka iruke masaa +4000 kwa mwaka kwa kwa hesabu za haraka hiyo ndege inatakuwa inagharimu 62,8 mil dolar za kimarekani,hiyo inamaana hiyo ndege lazima itegengeze zaidi ya dolla za kimarekani 62,8mil kwa mwaka.hapo bado hajaongelea matengenezo madogo madogo ya ndege nk..

Watanzania ni watu wapole na wasikivu sana,sema bado hawajapata Kiongozi madhubuti wa kiwaongoza,Nchi inaendele na kupata maendeleo mazuri ya kiuchumi na kijamii kama wananchi wake wananidhamu ya Maisha,watanzani tayari wana nidhamu kinachokosekana ni Kiongozi madhubuti anaewapenda raia wake....

Magufuli kanunua ndege kwa hisia zake binafsi hata ukisikiliza hotuba yake ya kuipokea ile ndege imejaa Hisia kuliko uhalisia au utaalamu wa kwanini ile ndege imenunuliwa..Ndege ubavuni imeandika "Hapa kazi",imeandikwa Kilimanjaro bila ya kufanunua Kilimanjaro Mlima,Mkoa au Bia,Tumeshindwa hata na KLM ubavuni mwa ndege kumeandikwa "Mt Kilimanjaro" inayomaanisha kuwa wamekusudia Mlima wa Kilimanjaro..

Nchi ya Wajinga Raisi wao ndio kubwa la wajinga...😀
 
Nchi ya Wajinga Raisi wao ndio baba wa wajinga...😀
Nimeisoma hiyo article. Jamaa kachambua vizuri' Ila simfahamu na sijui undani wa aliyosema sababu sifahamu chochote kuhusu ndege. Ningekuwa Nina muda ningefuatilia uhalali wa alichosema Ila kwa sasa nahangaikia kipato zaidi' hayo mengine ngoja niwe mtazamaji na Mtoa maoni pale nilipo na ufahamu. Ila kama jamaa yupo sahihi aisee itakuwa mbaya sana.
 
Tujifunze kusikilize wataalamu sio kila kinamuliwe kisiasa,Mkurugenzi wa Ethiopia Airline alipoulizwa majuzi na DW kwanini shilika la hio la Ndege limefanikiwa sana ijapokuwa kuna changamoto sana za kisiasa Ethiopia,alichojibu ni kuwa Ethiopia Airline inaendeshwa kitaaluma sio kisiasa,Serikai ya Ethiopia haingilii kabisa juu ya maamuzi na uendeshaji wa Shirika hilo..
 
Kama huna taarifa kamili ni bora ukakaa kimya.
Kutokuwa na taarifa haimaanishwi ulishwe matango pori. Kama huna taarifa basi tumia hata reasonableness au logic kuhoji jambo ambalo halina uhalisia vinginevyo utakuwa tofauti na wale wanaosema ndiyo kwa kila jambo yaani wewe ni Zuzu, sasa sijui na wewe nikuweke kwenye kundi hilo.
 
"mfano mgeni huyu anatumia lita 6,811 kwa saa" hili jambo unauhakika nalo, kutoka USA mpaka TZ itatumia lita ngapi? kwa muda wa masaa 13 hadi 16? mnapoongea muwe na uhakika. unajua hiyo ni Sh ngapi mafuta tu. hapa kunauongo kabisaaa.
kaka nakwambia tz tuna watu wajinga kwa kiwango cha lami. yaan wanaongea tu. ndo rais aliwaita mazwazwa. lita 6000 ni tani6 za uzito eti kwa saa, hayo mafuta inayabebea wapi, hebu jaribuni kuwa mnafanya ka utafiti kidogo kabla ya kuleta nyuzi humu, jf ni great thinker, sio whatsap humu
 
Back
Top Bottom