Ningeweza kulibeba hili jengo ningefanya hivyo!

Ningeweza kulibeba hili jengo ningefanya hivyo!

Engineer ambae hata chooni anaenda kunnyyya pembeni akipewa kujenga huu mjengo si ndo atajenga uharo
 
Mkuu hilo jengo limeoverturn kwa uzembe wa contractor au designer. kitaalam unapokuwa na slope site inabidi ucheki slope stability na kama slope itakuwa unstable kuna njia za kufanya kuongeza slope stability kama 1)cutting bench 2)reduce the slope angle na kama eneo litakuwa dogo basi utajenga retaining wall. Sasa kosa la designer hapo linaweza kuwa hakucheki slope stability vizuri. Kosa la contractor ni kwenye kumwaga kifusi nyuma ya jengo maana kinaongeza uzito na force kwenye slope hata kama slooe ilikuwa stable kwenye design ila wakati wa design hakuconsider hicho kifusi kitamwagwa hapo basi ndo madhara hayo.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mmmh, mbona unanirudisha nyuma tena, bila hilo shimo kuchimbwa jengo lingeanguka, regardless ni slope or not?
 
Wewe jamaa sijui una matatizo gani? picha ya nane uliyoweka imekuelewesha clearly kabisa kilichotokea, kwamba tatizo halikuwa kwa maengineer wala madesigner, tatizo na hao machoko waliochimba shimo kwa mbele kwa ajili ya garage bila kufanyia reinforcement hilo shimo, halafu kifusi wakaenda kukiweka kwa nyuma, mvua ilivyonyesha kingo za shimo zililainika na ukiongeza na uzito wa msukumo wa kifusi walichoweka nyuma ya jengo basi shimo likaporomoka na kuangusha jengo.
Wewe itakuwa ni msomi wa hali ya juu,Mungu akubariki sana,umeelezea,na kimeeleweka,asante sana kwa maelezo yako.Yaonyesha Tanzania tuna wasomi wazuri wa kiwango kizuri kama chako.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wahandisi wazawa si ndo walioweka taa za kuongozea magari pale chini ya daraja la TAZARA mchina kaja kuwaaibisha na round about Ubungo
Kwahiyo hujawahi kuona mazuri yeyote yaliyofanywa na Wahandisi wazawa hapa Tanzania zaidi ya hayo mapungufu uliyoyasema?Kuwa fair kiongozi, Wahandisi wamepambana na wanaendelea kupambana kwaajili ya Tanzania unayoiona💪💪
 
Mainjinia wanafanya kazi yao tusihukumu bila kua na taaluma husika
Ila mimi huwa najiulizaga, mbona madaktari wakiua mtu chumba cha oparesheni huwa watu wanasema ni kazi ya Mungu, ila wajenzi wanapoangusha jengo (very rarely though) watu husema ni wazembe, hivi ni kwanini lakini?
 
Sasa kama unakiri tatizo ni shimo lililochimbwa, mbona ukawa unasema kwamba eneo lilikuwa ni slope na kwamba proper consideratiob za sloping topography hazikufanyika?
Mkuu angalia hiyo picha namba 8 hilo shimo lilikuwa na slope na mimi naongelea slope ya hilo shimo. na ukiangalia kwa umakini ameionyesha failure ya hiyo slope na unapokuwa na slope yoyote kwenye construction lazima ucheki stability ya slope, na utaona mtaalamu kwenye picha anasema improper support of the excavation Iakini kapoint mshale kwenye slope ya shimo. Na pia mimi kule juu niliongelea vitu viwili slope na kifusi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom