Ningependa kumzungumzia huyu adui namba moja ambaye ni Ujinga

ASIWAJU

JF-Expert Member
Nov 18, 2022
1,939
1,625
Wakati wa uanzishwaji wa falsafa ya ujamaa na kujitegemea, Mwalimu alitaja maadui watatu wakubwa wa kupambana nao ili taifa liweze kupata ustawi ulio bora maadui hao ni pamoja na :-
i, UJINGA
ii, UMASIKINI
iii, MARADHI

Ningependa kumzungumzia huyu adui namba moja ambaye ni Ujinga.

UJINGA
Kwa tafasiri nyepesi ya kiswahili, ujinga ni kuto kufahamu jambo.

Katika taifa letu toka tumepata uhuru wa bendera mpaka sasa hatuja weza kabisa kupambana na adui ujinga na kumshinda.

Bila kumshinda adui ujinga kama taifa ustawi ulio bora wa nchi kamwe hatuwezi kuupata. jambo baya zaidi ni kuwa adui ujinga kadiri miaka inavyo songa ndivyo anavyo pata nguvu na kutawala vichwani mwa Watanzania kwa kiwango kikubwa.

Elimu yetu kwa asilimia kubwa imeshindwa kabisa kupambana na huyu adui bali ndio inachangia kwa kiwango kikubwa kuongeza ujinga hapa nchini.

Ushiriki wa Watanzania katika mambo ya msingi upo chini sana, michango ya Watanzania katika mambo ya msingi upo chini sana, ufahamu wa Watanzania kuhusu mambo ya msingi upo chini sana.

Vitu vya kijinga kwa asilimia kubwa ndivyo vinavyo pewa nafasi kubwa hapa taifani kadiri miaka inavyo songa mbele lakini mambo ya msingi yana pewa nafasi ndogo sana kupita maelezo.

CCM wana fahamu fika wana tawala watu wajinga na watu wajinga kwa tawala za kipumbavu kwao ni faida kuliko watu werevu.

CCM hawana mikakati ya kuondoa ujinga hapa nchini kwa kuwa kwao ni faida na pia Watanzania hatutaki kuondoa ujinga vichwani mwetu kwa juhudi zetu binafsi.

Hatuwezi kuwa shinda hao maadui wote watatu[ maradhi, umasikini na ujinga] kama bado hatuja weza kumshinda huyu mmoja mkubwa ambaye ni ujinga huku mipango na jitahada za kumshinda kutokuwepo.
 
Mazingira ndo yanachangia Maisha watu kuwa wajinga pia Hali Ngumu ya Maisha Watz wengi Maisha bado yanawapiga TKO

Pia tuhakikishe tunakataa Ndoa ili tusijiaAtach na umasikini
 
Back
Top Bottom