Ningemshauri huyu dada lakini ndio hatuna mazoea kabisa

Ningemshauri huyu dada lakini ndio hatuna mazoea kabisa

Huyu dada ni mpangaji mwenzangu hapa Kunecity (DSM). Hii ishu ilianza wiki kadhaa nyuma nilimskia mpanga mwenzangu akiongea na ndugu zake wa kaskazini uko nadhani ni moshi. Alikua anawashawishi kutoa kiasi kadhaa si chini ya laki 5 alianza na mwanamke akamshawishi kwa siku kadhaa uyo bidada akaingia kingi sasa ikabaki kumshawishi baba ake nae ajiunge na iyo biashara. Kiukweli mi sikujua ni biashara gani na wala sikutaka kufatilia nikidhani ni mitikasi ya mjini tu hapa na ukizingatia imekaa kifamilia familia basi ata sikutaka kujua.

Sasa jana jioni ndo nikajua bila hata kutarajia kumbee bwana ni walewale ndugu zetu wa lete watu wako wawili na wao wakileta wawili unapata commision ya million kadhaa na blah blah zao zile. Ayo yote nimeyajua alipokua anamshawishi rafiki yake nae aingie kingi daah nikamsikitia bidada wa watu anamwambia unamjua tajiri namba 2 duniani nae alipitia huku huku aliacha shule akaanza izi biashara mpaka akawa tajiri. Jaman jaman hawa watu wanatumia dawa gani kushawishi watu yani ukimskia uyu dada utadhani yeye ndie mwanzilishi wa hii kampuni X. Anazidi kumshawishi ati atapata offer kibao kutembelea nchi mbalimbali na kulala hoteli za nyota 3 hadi 5 pale akifanya kazi yake vyema na izo offer sio lazima apate yeye zote anaweza kuamua tu nani ambless akalale hoteli aliyoambiwa yeye alale na anamchagua mtu wake yeyote tu wa karibu.

Tatizo sijazoeana na uyu mdada ni salamu tu na kupita ivi walau ningeshauri chochote ila ndo ivo kazama mazima kwa hiyo kampuni kubwa duniani kwa usambazaji wa vitu mbalimbali na kama mjuavyo maisha ya kimjini mjini haya kuingilia mambo ya watu nikaona bora nije kuwapa story wanaJF.

Mimi hawa jamaa nilishawahi kwenda hadi uko ofisini kwako ilikua ni moroco nadhani mwaka juzi wana story nyingi za kufikilika. Nakumbuka niliwatafuta baada ya kupata mawasiliano yao fb nikaambiwa niende uko ofisini kwao basi bna tukaingizwa kwenye kiukumbi hapo hapo ofisini kwao kwasababu tulikua wengi kidogo. Wakatoa ushawishi waoo na shuhuda za uongo na ukweli, mwisho nikaja kugundua kua mule ndani walengwa tupo wachache ila wengi ni wenzao waliojifanya nao ni mala ya kwanza kwenda pale ili ukifika wakati wa kutoa pesa wale wenzao waanze kutoa kwa hamasa na sie walengwa tuhamasike tutoe chap aisee niliwastukia pale nikayeya walikua wanapiga simu mpaka walichoka sasa.

Bidada kauvaa ni suala la muda tu.

mkuu mimi nimekuelewa sana mwanzo mwisho sema mara nyingi watu huja kujilaumu kwa vitu ambavyo hawakuvifanya kuliko vile walivyovifanya.

mim inaona ungemwambia., uwe na point of reference we ongea point zako kisha itabaki kwake kufata ushauri wako au lah, najua kwa 70% hatakusikiliza ila utakua umepanda mbegu na utakua umejiondolea mzigo., hata likija kutokea huko mbele itakua ni juu yake na maamuzi aliyochukua licha ya ushauri uliompa..

usipomwambia akija kupata shida utajiskia vibaya Mkuu..
 
sio kweli,,..labda kama wewe unaishi masaki,, ila kwa nyumba zetu za kupanga kibongo bongo jirani akiongea na simu unasikia tu especially kwa wale wanaoongea kwa sauti.
Munashinda pamoja? Kwanini hio mada aizungumzie kila ukiwepo wewe? Mbado
 
Wewe mwambie akikubali sawa akikugomea sawa wewe shida yako mjumbe hauwawi hata akipigwa atakukumbuka ulimshitua akashupaza shingo yake, mwambie.
 
Hahaha sijamfatilia mkuu anaongea kwa sauti mno namsikia vizuri tu. Wala sina muda wa kumfatilia ila ndo ivo ananihabarisha bila mimi kutaka
 
Sio kampuni X itaje ni Qnet, Smile we care au?? Enewei wajinga ndio wali wao jamaa hawatumii uchawi wowote ila siku zote tapeli anatumia akili kuyashinda madhaifu ya mtu unakuta jitu ukiliambia kuna mchongo wa Million kadhaa domo lnatema udenda kwa tamaa acha wanyooshwe
Sijui uyo dada anashawishiwa na kampuni gani mkuu ila kwangu mimi ndo ilikua ni hiyo qnet
 
Ukiona wamekufuata wakupe fulsa ujue wewe ndo fulsa yenyewe. Hawa jamaa wa Qnet walishawahi kunipa invitation ofisini kwao ni kama miaka mitatu imepita, wana story nyingi jinsi ya kufanya ili uwe bilionea ndani ya mwaka . Utahadithiwa hadi vitabu vya kina Kiyosaki. Nliingia mitini na hadi leo sioni bilionea kutoka kwenye jopo lao.
 
Dah umeandika kitabu, bila shaka unajua muhusika yupo humu JF
 
Hatari sana ...

Na wakishashawishika huko ni kama vile wamekula ndimu kusumbua wengine...
 
Hatari sana ...

Na wakishashawishika huko ni kama vile wamekula ndimu kusumbua wengine...
Acha kabisa mkuu kuna mwingine alikua manzi yangu yeye alijiunga na hawa wasambazaji wa vipodozi aisee alijishawishi hadi akanilipia fee ya kuingia huko na mimi niwazungushie ivyo vipodozi vyao. Ile sikuielewaga ni kama unalifanyia kazi kampuni kwa nguvu na malipo yako ni kutokana na mauzo yako bidhaa zenyewe bei kinoma sabuni tu inauzwa elfu 9. Kuwapata hao wateja ni kwa mbinde afu unalishwa maneno na ahadi za muongeze huyu utalipwa na huyu akimpata huyu.
 
Back
Top Bottom