Ninapenda kuishauri Wizara ya fedha kuangalia kodi zifuatazo ili ziwe nafuu/rafiki kwa mfanyabiashara

Koryo2

JF-Expert Member
Nov 28, 2016
2,056
2,515
Natumaini miezi hii ndiyo Serikali iko kwenye maandalizi ya kutayarisha bajeti yake ya mwaka 2021/22.

Pamoja na hayo ninapenda kuishauri Wizara ya fedha kuangalia kodi zifuatazo ili ziwe nafuu/rafiki kwa mfanyabiashara au zijumuishwe kwa pamoja ili mlipa kodi anapolipa basi alipe moja kwa moja.

(1) Hotel levy huwa inalipwa kila mwezi kutokana na wateja. Hapa ndiyo kuna mgogoro. Ukifika ofisi ya biashara unakadiriwa bila kujua idadi halisi ya wateja waliolala wakimchukulia mfanyabiashara kuwa ni mdanganyifu.

Ninaishauri eneo hili Serikali iliangalia ili kuweka flat rate hasa maeneo ya mjini na kusiwe na makadirio inayoleta harufu ya rushwa.

(3) Gharama ya kupima watumishi wanaofanya kwenye mahoteli, guest houses, bars nk. Nashauri eneo hili lifutwe na Serikali. Upimaji uwe ni bure kwa watumishi wanaofanya kazi katika maeneo hayo.
 
Back
Top Bottom