Wanatumia hizo dawa nao ni binadamu,ila nilipanga nilifanye 2040,nimeghairi nalifanya 2030
KILA LAKHERI MKUU.
Mimi pia nilitamani kufanya hivyo kama ambavyo wewe una wiwa kufanya kwa mtoto wako.
Mimi niliplan kufanya hivyo mwaka 2025 kwa condition kwa Samia asipogombea basi mimi nitakuwq miongoni mwa wagombea watakaoomba ridhaa ya chama cha mapinduzi (CCM) ili kuongoza dola.
Kwa bahati mbaya sana Mama alikomaa.
Kwa kawaida huwa sikati tamaa kirahisi. Na ndio maana mwaka 2022 Marehemu Job Ndugai alipoachia ngazi ya Uspika (Baada ya kufanyiwa figisu) Mimi nilikuwa miongoni mwa watu 71 waliochukua form (ukirejea kwenye ile list basi nipo top 5).
Kama Roho mtakatifu ataniongoza vema, basi nakuhakikishia safari hii 2030 mimi nitachuana (sio kwa ubaya) na huyo kijana wako ili kupata nafasi ya kuleta haki na kukomesha ufisadi, na kisha kuwaletea watanzania maendeleo hasa watu wa maisha ya kati (middle income) na wale wa maisha ya chini ambao ni wengi (low income earners - inclunding peasants 70% of them).
Kimsingi nakerekwa sana na hali ya sasa na hasa huu utamadumani wa watu kutaka madaraka kwa ajili ya kujinufaisha wao na familia zao.
Kwa sasa naendelea kupambana na maisha yangu huku nikifuatilia kwa ukaribu duru za siasa kuelekea 2030.
NB: 2027 naanza kwa kugombea cheo kikubwa cha kisiasa ndani ya CCM kwa ngazi ya Taifa ili nianze kuchungulia jikoni kwa urahisi na kuweza kutengeneza mazingira ya kuaminiwa ndani ya chama.
Kiukweli ikitokea siku nimeingia IKULU naamini watanzania wote hata kwa kizazi kijacho hawatakuja kunisahau kwa jinsi nitakavyo ipambania nchi yangu na kuiletea maendeleo kwa kipindi cha muda mfupi wa uongozi wangu.
Mwambie huyo mwanao asikate tamaa ila asiwe mbinafsi ajitoe kwa ajili ya nchi yake na sio kwa ajili ya tumbo lake na faida ya familia yake.
KILA LA KHERI KAKA MKUBWA.