Katika mchakato wa kupata Rais wa JMT, katiba inaelekeza kuwa ni lazima kuwe na mgombea mwenza ambaye Rais akishinda uchaguzi then mgombea mwenza huyo anakuwa Makamu wa Rais.
Nikiri kuwa sikuwahi kuchukua cheo cha Makamu wa Rais kwa uzito mkubwa. Mara nyingi niliona kuwa makamu wa Rais ni takwa la kikatiba tu kwa kuwa mara nyingi niliona kazi nyingi zikifanywa na Rais na Waziri Mkuu akisaidiwa na Mawaziri. Nilikuwa nikimwona Makamu wa Rais kama mtu wa kutembea na mikasi tu kwenye koti kukata utepe wa kuzindua hiki na kile.
Kifo cha Hayati JPM imenionesha kwa vitendo umuhimi wa kuwa na makamu wa Rais anayeweza kufanya kazi za Rais. Kumbe mgombea mwenza sio cheo cha kimasihara.
Nimejikuta nawaza mgombea mwenza wa Tundu Lissu, ndg. Salim Mwalimu. Nikawaza kama Tundu Lissu angeshinda urais na likatokea kwamba ilivyokuwa kwa JPM? Pamoja na ukweli kuwa namuheshimu sana Ndg. Salim Mwalimu lakini sidhani kama ana haiba ya kuwa Rais wetu.
Kimsingi hatoshi kuwa Rais wa nchi hii ukimlinganisha na Rais wake ambaye angekuwa Tundu Lissu. Sasa ni afadhali sana hata huyo Salim Mwalimu. Nimewaza wagombea wenza wengine kama yule wa mzee wa ubwabwa.
Tafadhali vyama viwe serious wanapotafuta mgombea mwenza.