Ninalaani vikali kukamatwa kwa Lema! CHADEMA msipochora mstari...

Ninalaani vikali kukamatwa kwa Lema! CHADEMA msipochora mstari...

Naamini kikwete atakuwa anafurahia sana haya mambo yanayoendelea nchini......dhaifu mkubwa na ufisadi wake
 
Kwa sasa badhi ya mitaa imeanza kupoa ila ccm kamwe hawezi shinda tena Arusha kamwe tunaapa
 
Mtu akiamua kujiangamiza huwezi kumuokoa, tusipoteze wakati, Lema ni msiba mkubwa sana kwa chadema na Arusha, Ana hatia na hafai hata kidogo, utetezi wenu hautamsaadia, niko Arusha na wananchi wengi hawamtaki, watu wanaogopa tuu fuju za wahuni wanaoshangilia mambo ya fujo na kuharibu mali za watu, na hao ndio wanaomuunga mkono lema, kwa manufa yao ya kupora mali za watu na kuteketeza wachoweza kubeba. Watu wengi wa Arusha wameshoshwa na Mambo Ya LEMA. na pia huyu bw atakuwa Mbunge wa term moja tuu.
 
Aisee nipo mbali natamani niwe hapo Arusha niungane na makamanda kuupinga huu udhalimu anafanyiwa mbunge wa Arusha.
 
umeambiwa wewe ni mshabiki wa mpira usiyejua hata kupiga mpira tu,hujui sheria zote za mpira wa miguu umekalili rangi ya jezi za timu unayo ishangilia .shame on you ingia uwanjani uone game
 
Maneno yenye hekima kutoka kwa mtu anayeonekana kuwa na hekima kutokana na kiwango chake cha elimu na uzoefu wa maisha na uongozi.mashaka yangu ni kama huko polisi kuna watu wenye vichwa kama wewe na sie wa jf hapa watakuelewa.ila kama ndo walewale akina Kamuhanda..mh!no way,tuendelee kuimba nao tu, u never know bwana!
 
Tatizo kubwa la serikali ya magamba ni kuishi kwao kwenye giza nene lenye dhana potofu ya kuwa CHADEMA ni chama tu. Wasichofahamu ni kuwa CHADEMA imeshavuka mpaka na si chama tena, bali ni itikadi, ni mfumo wa maisha ya kila siku, ni kilio cha wanyonge, ni nguvu ya umma. CHADEMA ni vuguvugu la ukombozi wa mtanzania aliyechoshwa na 'ukoloni' wa hawa watanzania wachache walioko madarakani wanaojiona bora kuliko watanzania wengine. Kukua kwa CHADEMA ni matokeo ya kukosa imani na serikali iliyoko madarakani inayoongozwa na vibaraka wachache wanaojilimbikizia mali kupitia jasho la wananchi walalahoi.

Matendo yanayofanywa leo hii na serikali ya ccm hayana tofauti na matendo yaliyokuwa yanafanywa na serikali ya makaburu huko Afrika ya Kusini wakati wananchi walikuwa wanazuiwa hata kuandamana kudai kilicho chao. Serikali ya makaburu ilikuwa haina simile kwa mtu yeyote yule aliyediriki kupaza sauti kuzungumza hadharani kuhusu maovu yao. Watu wengi walisingiziwa kesi, walifungwa na kuuawa. Kwa watakaopenda kurudi nyuma kwenye historia kulikuwa na mauaji ya 'Sharpeville' wakati askari wa makaburu walipofyatua risasi na kuwaua wanafunzi waliokuwa wanaandamana.

Lakini kama walivyofika mahali makaburu wakashindwa, pamoja na nguvu yote hiyo ya dola, na pesa, na kushikilia nguzo zote kuu za uchumi, Mandela alitoka gerezani na akashika utawala wa Afrika ya Kusini. Kwa mtu wa kawaida angeweza kusoma na kuelewa ya kuwa hii ni ishara mbaya kwa ccm, inaashiria mwisho wake. Lakini sikio la kufa halisikii dawa. Ni kama Nuhu alipowaambia watu wake ya kuwa gharika inakuja wakamcheka alipokuwa anajenga safina, viongozi wa ccm wakumbuke ya kuwa gharika ilifika. Watamshika leo Lema, watabambikiza kesi, watafanya kila njia, lakini mawingu yanatanda na wafahamu wazi gharika iko karibu!

Sauti ya wanyonge haitazimwa kamwe!
 
Mzee Mwanakijiji,Kimsingi mimi nakuunga mkono kabisa kwa bandiko lako,hasa kuhusu kutafuta suluhu endelevu na si kuendelea kuwaambia wananchi juu ya uonevu wa serikali,afterall hata wao wanajua wazi kuwa Maccm na Serikali yao imebaki kutumia vyombo vya dola kufifisha mabadiliko yajayo,hasa ukizingatia yameanza kushika kasi.
Kimsingi hatua iliyobaki kwa CHADEMA ni kuwaongoza watanzania wapinga udhalimu,wapinga uonevu,na wapenda mabadiliko kwenye suluhu endelevu ambayo kwangu mimi naona ni kuiambia serikali ya CCM kuwa hapa sasa mwisho.lakini haiwezekani kufikia huko kwa maneno bila vitendo,hatuwezi kufikisha ujumbe kwa watawala.Na ili ujumbe ufike ni lazima dhamira yetu ya moyoni isiwe ni ya kutanguliwa na tamaa ya madaraka,bali itanguliwe na moyo safi wa kizalendo,wa kulipenda taifa,moyo wenye upendo kwa wanadamu wenzio na hivyo kuwa jasiri hata kufikisha ujumbe kwa ku-sucrifice maisha,kukubali kufungwa na hata kupata ulemavu ukipigania haki.CCM kamwe hawatatoka madarakani kwa kuwapigia tarumbeta,na kadri kasi ya mabadiliko inavyoogezeka ndio na wao wanapanga mkakati wa kudhoofisha kasi hiyo.
Ni jukumu la viongozi wa CDM kuwaongoza watu kwenye kupeleka ujumbe wa kukataa unyama unaoendelea kwa kutumia kile kilichotangazwa kuwa mwaka huu kwa CDM ni mwaka wa nguvu ya umma.tuuongoze umma kukataa mbinu dhalimu za kufifisha kasi ya mabadiliko.
 
Hivi ule wimbo wa kipindi kile 'Chinja kaburu matata chinja' mwalimu alikuwa anachochea fujo?
Kama ni J. K. Nyerere alituletea hako kawimbo na hakakuwa na tatizo kwanini tusikadumishe kwa kukaimba na kukifanyia kazi kila wakati kwa kuweka jina la muhusika pale 'chinja Mulongo matata chinja. Na kuifanyia kazi nyimbo hii kwamba Mulongo achinjwe kama tulivyowachinja makaburiFredrick de Clark na akina Peter Botha
 
MMM be blessed for your high moral values. You've have already made my day Sir. CHADEMA muda ndio huu na lazima mfanye kitu kwa kauli na matendo ieleweke kwa hawa wahuni wa CCM.

Pamoja na mapendekezo mazuri ya MMK na kuungwa mkono. Je "kitu kwa kauli na matendo" ni kitu kipi? Kama ni kauli za majukwaani CDM wametoa sana na kuungwa na wananchi. Kama ni maandamano ya amani, hilo nalo usiseme mpaka wanaitwa chama cha maandamano! Hatua zilizobaki ambazo zikichukuliwa, itakuwa ni mwanzo wa kuvunjika amani ya nchi labda na umwagaji damu. Hilo mimi siliungi mkono katu. Mwanakijiji huenda anatumia falsafa ambayo ipo juu ya uelewa wangu kwa vile anasisitiza hatua zichukuliwe zaidi ya hizi zinazochukuliwa na CDM. Hatua hizo ni zipi? Mimi ninadhani katika mapambano yoyote ya kudai haki, silaha kuu kupita zote ni KUTOKUKATA TAMAA. Katika vita hivi, majeruhi ni lazima wapatikane lakini tusilegeze kamba. A LUTA CONTINUA.
 
Usidanganye watu arusha wameshachoka na lema

Hivi wewe nguchiro umetumwa na nani? Hivi gamba kama wewe umpende Lema kivipi na roho zenu za kishetani zinazofukuta? Gamba na CDM wapi na wapi? Wanaompenda ni wananchi wa kawaida waliochoka na maisha magumu, sio mnaokula keki ya taifa kama wewe! Nyambaf
 
mzee mwanakijiji amesema kila kitu,sina cha kuongeza,mpira urudi kwa mbowe,slaa,zitto,lissu na wanachadema wote.
 
Busara itumike tu,ccm rudishini imani kwa wana arusha kwa kumtoa kafara mkuu wa mkoa otherwise hata udiwani mnaweza msiambulie hata kiti kimoja

Mkuu hata waki muondoa mkuu wa mkoa- MUONGO; Kwenye sakata la uchaguzi wa madiwani unao tarajiwa kufanyika mwezi wa sita mwaka huu, take it from me hawatapata hata kiti kimoja, Arusha maCCM haya uziki, hata kampeni zao tu itakuwa ni mithili ya Bongo movie.
 
Mtazamo wangu binafsi: Kukamatwa kwa Lema (MB) kama jambazi sugu ni ishara kuwa mamlaka ya sheria ya nchi imeanguka na kupoteza sifa kwa kiasi kikubwa. Haiji akilini mwangu kwa mtu maarufu, aliyechaguliwa na wananchi na kuibwaga CCM mara mbili mahakamani akamatwe kwa mtindo ule. Nilichokitegemea ni kwamba angepewa taarifa ya kuitwa kituoni na kuitikia wito. Haiji akilini mwangu RC anapotamka kuwa hawezi kuhongea na wanafunzi mpaka Mbunge aondoke, hiyo ni "akili ndogo ambayo inaendesha akili kubwa". Kwa busara alitakiwa kutoonyesha tofauti zake dhidi ya Mbunge mbele za wanafunzi. Tukiendekeza siasa za visasi na ubabe nchi hii haitafika popote. Hivi kweli njia zote za kumwita Lema polisi zilishindikana mpaka akamatwe kama jambazi? Hivi kwa kufanya hivyo ni kumharibia Lema au kumpatia sifa na umaarufu asiostahili? Naamini kwa wapiga kura wake ni ushindi mkubwa na kuwafanya wawe karibu zaidi na mbunge wao. Jamani viongozi mlioteuliwa (maRC na maDC) tumieni busara ya hali ya juu kuitumikia serikali. Ukiona yamekushinda mtaarifu aliyekuteua kuwa umechoka na uendelee na kazi zingine. Najua wengi wenu mlishapoteza dira maishani, ndo maana mnatekeleza majukumu ya serikali kwa kukurupuka na hatimaye mnamfanya Rais wetu aonekane dhaifu bila sababu za msingi. Hicho kilichotokea kwa Lema (MB) kiwe fundisho kwa viongozi wanaotaka kuendesha nchi kwa jazba ambazo zinaigharimu kwa kiasi kikubwa serikali yetu

Huku tuendaka sasa ni hatari tupu, hapa naanza kuona kwa mtazamo wangu viongozi wa serikali kuanza kukosa busara. Kuweni na busara na mfanye mambo kwa maslahi ya taifa.

Kumkamata mbunge bila kosa eti kisa wewe ni mkuu wa mkoa ni dhambi kubwa sana na inaweza kuiletea matatizo taifa letu kwa ujumla. Nalaani sana kitendo cha kukamatwa mbunge na polisi eti kwa kuwa mkuu wa mkoa amesema!
 
Hiki ndicho alichokisema Mzee Mwanakijiji. Mbinu za kawaida za Chadema ni hizi mbili tuu maarufu, kuitisha maandamano, na kufanya mkutano wa hadhara na ama kulalamika, ama kuwashitaki kwa wananchi!, sasa kama unazo mbinu nyingine zaidi ya hizi, wasaidie!.
Pasco.

Pasco,

Nimekusoma toka juu ya uzi huu. Mbinu wanazotumia cdm za kidemokrasia ili amani ya tzn idumu. Bado na shauri mbinu hizi zitumike wakati ushaidi unaotosha kuthibitishia umma wa tzn wasio na woga kuchukua hatua mathubuti, of course in support of other nations. Na hili haliko mbali sana, we only need justifiable and beyond reasobable doubts that maganbas are the breakers of tnz' s peace but not cdm kama ambavyo wangependa.
 
Duh! Marahabaa mengine haya ya mwaka! Ccm rekebisheni viongozi wenu wote wazembe! Kama huyu Tata magesa kachoka mwambie apumzike tafuteni mwingine weka mkuu wa mkoa sio lazima eti akiteuliwa ndo afe nao! Tatizo hapa mnataka viongozi mnaowataka nyie ndo watuongoze! Na sio wanaotakiwa na wananchi
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom