Ninalaani vikali kukamatwa kwa Lema! CHADEMA msipochora mstari...

Ninalaani vikali kukamatwa kwa Lema! CHADEMA msipochora mstari...

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined
Mar 10, 2006
Posts
34,250
Reaction score
44,579
Sijui nitumie lugha gani kuelezea hisia zangu juu ya kile kinachoendelea nchini na hasa matumizi ya Jeshi la Polisi dhidi ya raia. Lakini siyo tu matumizi lakini hasa jinsi jeshi hili limekuwa likitumia nguvu kubwa sana kwa ajili ya vitu vidogo na hata visivyo na msingi. Kukamatwa kwa Lema na hasa namna alivyokamatwa ni dalili ya matumizi mabaya ya madaraka ya polisi (abuse of power). Kwamba, kwa vile polisi wana uwezo wa kupekua na kukamata basi wanaweza kufanya hivyo popote, kwa yeyote na kwa lolote wakijua kabisa kuwa hakuna wa kuwakemea.

Jeshi la Polisi kama lilikuwa linamtaka Lema vibaya namna hiyo lingeweza kabisa kutumia njia za kawaida za kisheria ikiwemo kumpa wito wa kufika makao makuu ya Polisi wakimueleza anahitajika kwa nini na kama angekataa basi kupata kibali cha mahakama kumuendea na kumkamata na kama kutoa warranti ya kipolisi basi jambo hilo lingefanyika bila kuonesha hisia kuwa Lema analengwa bila ya sababu (targetted for no apparent reason) isipokuwa tu kwa vile ni Lema na ameonesha msimamo wake wa kutokuwapigia magoti watawala. Ni Uhuru huu wa Lema unawatisha watawala zaidi kuliko kitu kingine chochote.

Mwendelezo wa vitendo vya aina hii dhidi ya wabunge wa CDM ni jambo la kukataliwa, kulaaniwa na kupingwa na kila mpenda demokrasia na anayeamini katika haki za raia (civil rights). Kwa miaka sasa tangu baada ya uchaguzi mkuu wa 2010 tumeona vyombo vya dola vikitumika kiunyanyasaji dhidi ya viongozi na wanachama wa CDM; kuanzia Arusha hadi Mbeya, Mwanza hadi Ruvuma, Dar hadi Kigoma. Ni vitendo vyenye lengo la kuwatisha na kuwakatisha tamaa viongozi na wanachama wa CDM lakini zaidi ni vitendo vyenye lengo la kufifisha na kudunisha mageuzi yanayokuja.

Uongozi wa CDM unapaswa kuchora mstari - ambao naamini watashangaa kuwa umeshavukwa - wa kuhakikisha vitendo hivi vinakoma. Kuendelea kulalamika na kudai serikali na dola inawaonea hakutoshi tena (rejea "Karipio Kali). Nimewahi kuandika huko nyuma kuwa kama CDM hawatatuma ujumbe kuwa the balance of political power in the country has shifted - in CHADEMA'S favor - basi wajue wataendelea kunyanyaswa, kudhalilishwa, kuonewa na kubambikiziwa kesi na tuhuma za kila aina. Wanahitaji kuamua kama wataendelea kufanyiwa hivi au watume ujumbe kuwa "enough is enough".

Wasipofanya hivi - na nimewahi kulisema hili pia - watajiandaa kulia na kusikitika na wasipoangalia kujikuta wanazika viongozi na wanachama wao kwani watawala hawaogopi maneno makali ya majukwaani, au vitisho vya matamko. CDM wafikirie namna moja itakayotuma ujumbe dhahiri, wa makusudi na usio na shaka wala utata kuwa mabadiliko ya nchi yanakuja na hakuna lolote ambalo CCM au serikali yake wanaweza kufanya kuzuia. NI mafuriko ya mabadiliko ambayo mkondo wake unatiririka kwa nguvu zote na CCM ama wapishe vinginevyo watasombwa. Jaribio la kuchimba mifereji na kuweka udongo njiani litafeli kwani mafuriko haya hayatakoma.

Ni kwa sababu hiyo ninalaani vikali, na kupinga kitendo cha jeshi la POlisi kutumia nguvu ya chombo hicho kumkamata Lema - Mbunge wa ARusha na raia wa Jamhuri ya Muungano ambaye amekataa kufanya kile ambacho watu wengine ni rahisi kukifanya - kupiga magoti mbele ya madhabahu ya CCM na kutoa sadaka za sifa za uongo.

MMM (BGM)
 
Tatizo lako unatumia taarifa za JF kuhukumu mambo usiyoyajua kwa undani...
 
Wengine tunasubiri tusikie amekamatwa kwa kosa gani.
Huyu ni Lema bwana!inawezekana kosa lake halihusiani na vurugu zilizotokea kule chuoni.
 
Naona imefikia sasa nchi tumeweka sheria pembeni na watawala wameamua kutumia akili ndogo kutawala akili kubwa, sasa kila mtu anajifnyia lililo chini ya uwezo wake mkuu wa wilaya anafanya analotaka, mkuu wa mkoa na anafanya analotaka mkuu wa nchi anasema hajashindwa kuongoza. yaani mambo ni vululu vululu.

Tusipochukua hatua tutajilaumu kuliko tunavyolaumiana sasa.
 
MMM be blessed for your high moral values. You've have already made my day Sir. CHADEMA muda ndio huu na lazima mfanye kitu kwa kauli na matendo ieleweke kwa hawa wahuni wa CCM.
 
Well said, lakini nadhani kuna muda nchi itatumbukia vitani. Si vizuri kuchochea na sishauri kuchochea kuinitiate action from public, lakini hata mapinduzi na uasi kwenye nchi kama RWANDA ulianza hivihivi kwa uonevu na udhalimu wa watu wanaodhani wao wana mamlaka ya kutawala na kufurahia keki ya taifa kuliko wengine. Utulivu ulianza kurejea lakini sasa naona taratibu uvumilivu unapotea. Kuna haja ya kutafuta mwafaka wa kisiasa na kitaifa kwa ujumla dhidi ya matukio ya hivi karibuni.
 
Mimi bado najiuliza... Hivi serikali inadhani kwa kumkamata Lema itakuwa imemkomoa au kuwakomoa wanachadema au chadema yenyewe? Does it have any positive impact to the government at all?
Itabadilisha maamuzi ya wananchi kwenye sanduku la kura 2015?
Sometimes viongozi wa serikali wanasababisha skendo zisizo na maana... Au ndio wanataka kuhamisha attention ya wananchi kwenye bajeti ya maji iliyobumba huko bungeni?
 
Tatizo lako unatumia taarifa za JF kuhukumu mambo usiyoyajua kwa undani...

ZeMarcopolo ww unajua nn? Ongea facts ili tulinganishe anayejua na kuhukumu ujinga ni MMM au ww ZeMarcopolo? Aliyehukumu bila kujua ni ww uliyeandika Ugolo pasi na hoja. Hicho kitendo cha Polisi kilichofanyika kwa G.Lema na kwingineko chini ya polisi ni cha kulaani kwa nguvu zote sasa ww unaleta Ugamba hapa.

Matukio hayo yametokea sehemu nyingi sana niliwahi kutoa taarifa Uhuni Uliofanywa na polisi Kijiji cha Kwaga Kasulu mkoani Kigoma polisi bila kufuata kanuni waliwavamia watu kuanzia saa sita-Saa tisa usiku ikiwa ni kuvamia, kupiga na kukamata Viongozi wa CDM jimbo la Kasulu vijijini na Viongozi wa serikali halimashauri kijiji cha Kwaga kupitia CDM na yeyeote ambaye kwake kuna bendera ya CDM.

Mpaka sasa ni mwezi na nusu sasa bado wako Mahabusu kwa uonevu huohuo ulifanyika Kwa Lema.Hivyo Wewe ZeMarcopolo nashindwa kukuelewa kama mwili wako Unavuja damu maana hata kama ww ni Gamba ifikie hatua tuwe tunaguswa na uhalifu huo unaofanywa na polisi sio kila kimoja tu ww kukejeli tena bahati mbaya bila hoja.
 
Duh! acha kukurupuka!!!! Umeangalia video zilizowekwa hapa na kuona popote pale ambapo Lema alitoa kauli yoyote ya kustahili kukamatwa!!? Mkuki kwa nguruwe kwa binadamu mchungu. Unaudhi sana kwa kauli zako fyongo. Una uwezo mkubwa sana wa kuchanganua mambo lakini umeamua kujivika umazwezwe na kukurupuka kila mara ili kutetea maovu nchini.

Tatizo lako unatumia taarifa za JF kuhukumu mambo usiyoyajua kwa undani...
 
Dictatorship.

No respect for the rule of law.

tatizo kuwa na vichaa kama law enforcement..wapelekwe Somalia
 
Chilosisi sijui kalala? make na huyu jamaa akiona tu post zinazoegemea upande wa CDM lazima akimbilie huko kupost ujinga wake. Bado sijaelewa hawa watu Nape anawalipaje, kwa kuwa wa kwanza kupinga kitu kinachoegemea upande wa CDM au kupinga tu? kama kupost mapema Chilosisi atakuwa anachukua fungu kubwa.
 
Kuna vitu vinatia hasira! Yaani ccm ndo isahau kabisa jimbo la arusha. Cant believe they can stoop this low!
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Bu Asante sana MM kwa bandiko lako la kututia moyo wapambanaji naona CCM wanakula adhabu yao wenyewe itakayowatesa kwa karne nyingi kuanzia 2015.

CHADEMA wanapaswa kuujibu uhuni huu wa serikali kwa busara kwani kwa hali iliyopo ni serikali kutafuta visingizio ili ichukue hatua wanazoimba kina Mwigulu na Wassira kila siku yaani za kukifuta chama. Hilo likifanyika CCM itaonja ladha ya hasira za wananchi na kutopata nafasi ya kujutia kosa lao milele!

Haiingii akilini hata kidogo kwamba serikali inaweza kutumia Polisi kumnyanyasa mwakilishi wa wananchi; lakini kipimo hiki hiki kinachowekwa na CCM leo ndiyo kiwe hiki hiki cha mgao wao baada ya 2015.
A luta continua!!
 
Hakika na haki itatendeka dhidi ya huu udhalimu
 
Wanatafuta kila namna ya kumwaga damu ili wapate sababu ya kauli zao kwamba CDM ni chama kinachotaka kuleta umwagaji damu nchini. Wanajua fika Arusha hawana chao labda ndio sababu hawajali, lakini wanachokosea ni kwamba maovu wanayoyatenda Arusha yanawagusa Watanzania wote kila kona ya nchi yetu na hivyo kuzidi kuongeza umaarufu wa CDM.

Kuna vitu vinatia hasira! Yaani ccm ndo isahau kabisa jimbo la arusha. Cant believe they can stoop this low!
 
Back
Top Bottom