Ninalaani vikali kukamatwa kwa Lema! CHADEMA msipochora mstari...

Ninalaani vikali kukamatwa kwa Lema! CHADEMA msipochora mstari...

busara itawale maamuzi! ushauri kwa serekali mkuu wa mkoa ahamishwe!

wapi ndugu wanakohitaji viongozi mapunguani! Ni bora apelekwe ikulu akasaidiane na akina ighondu wanaofanya biashara ya meno ya binadamu sababu kila anayetekwa lazima meno yapelee.
 
Mimi bado najiuliza... Hivi serikali inadhani kwa kumkamata Lema itakuwa imemkomoa au kuwakomoa wanachadema au chadema yenyewe? Does it have any positive impact to the government at all?
Itabadilisha maamuzi ya wananchi kwenye sanduku la kura 2015?
Sometimes viongozi wa serikali wanasababisha skendo zisizo na maana... Au ndio wanataka kuhamisha attention ya wananchi kwenye bajeti ya maji iliyobumba huko bungeni?


CCM na makada wake baada ya kushindwa kuishinikiza tume ya uchaguzi isiitishe uchaguzi Arusha sasa imekuja na mbinu ya kuwachokoza watu wa Arusha wafanye fujo ili wapate sababu ya kuitaka tume isimamishe uchaguzi Arusha. Wamegundua Lema hapa Arusha anaheshimika hivyo kumbambikia kesi itawachokoza watu wa Arusha.
 
Magesa akope busara kwa Gama wa kilimanjaro ambaye pamoja na kuwa kada aliyekubuhu na kuwa karibu na J.K ameweza kuwa kiongozi kati ya watu waliogawanyika kiitikadi na hata halmashauri ya mjini inayoongozwa na upinzani. Hata miaka 9 ya u-D.C alifanya vizuri kwa kutumia busara na kutambua yupo kwenye mfumo wa vyama vingi

Au Rais ateue r.c mtu mzima mwenye hekima kama alivyokuwa Shirima ambaye hana malengo ya kuwatayarisha wakazi kuchagua chama tawala uchaguzi ujao na kumzuia mbunge wa upinzani kutekeleza wajibu wake
 
Well said, lakini nadhani kuna muda nchi itatumbukia vitani. Si vizuri kuchochea na sishauri kuchochea kuinitiate action from public, lakini hata mapinduzi na uasi kwenye nchi kama RWANDA ulianza hivihivi kwa uonevu na udhalimu wa watu wanaodhani wao wana mamlaka ya kutawala na kufurahia keki ya taifa kuliko wengine. Utulivu ulianza kurejea lakini sasa naona taratibu uvumilivu unapotea. Kuna haja ya kutafuta mwafaka wa kisiasa na kitaifa kwa ujumla dhidi ya matukio ya hivi karibuni.

Resolution ni ngumu ikiwa negative side wanaona kutawala ni haki ya msingi,lakini tukiwa kondoo na kupokea kila dalili au ishara ya uovu taifa litaendelea kudhalilishwa.Ifike wakati CDM kama alivyotamka MMM wachukue hatua sitahiki hakuna vita visivyo na mwenyewe
 
Mungu na ampe jicho la rohoni rahisi huyu aone aliowateua wanachofanya!!
 
lema kwa sasa yupo ndani, nasikia amekamatwa usiku wa kuamkia leo hii
 
Nilishasema kuwa kuna watu aina kama ya mkuu wa mkoa wa ARusha they are still alive bcoz is illegal to kill them!. Ngoja watumie hiyo defence ipo siku itakuwa kinyume chake. Hapa ndipo ninapokataa, haki ya kuishi si kila mtu anayo. Ili iweje?.
 
Magesa akope busara kwa Gama wa kilimanjaro ambaye pamoja na kuwa kada aliyekubuhu na kuwa karibu na J.K ameweza kuwa kiongozi kati ya watu waliogawanyika kiitikadi na hata halmashauri ya mjini inayoongozwa na upinzani. Hata miaka 9 ya u-D.C alifanya vizuri kwa kutumia busara na kutambua yupo kwenye mfumo wa vyama vingi

Au Rais ateue r.c mtu mzima mwenye hekima kama alivyokuwa Shirima ambaye hana malengo ya kuwatayarisha wakazi kuchagua chama tawala uchaguzi ujao na kumzuia mbunge wa upinzani kutekeleza wajibu wake

shirima alikua ni kiongozi mwenye kujua nin maana ya vyama vingi..aliweka busara mbele...aliipenda amani ya Arusha..kwake ilikua Arusha kwanza,CCM baadae,bt ths ghost Mulongo hata historia yake alyofanya huko nyuma ni kinyaa!
 
Usidanganye watu arusha wameshachoka na lema

Hata kama umechoka na Lema, basi si umwache amalizie kipindi chake? Tambua kwamba asilimia kubwa ya wanaArusha ambao ni vijana na akina mama wako upande wa Lema maana wakiamua kufanya lolote dhidi ya serikali, Arusha haitakalika. Ni kwa busara hii watu wanachangia mawazo tufanyaje Arusha isitibuliwe. Nataka hili lijulikane wazi kuwa maadui wa Lema ni maadui wa WanaArusha. Lolote baya au zuri watakalofanya kwa Lema, wanawafanyia WanaArusha. Nawataka waelewe pia jambo lolote zuri hupongezwa na jambo lolote baya hulaaniwa. Kulaaniwa huko hufanywa kwa kupaza sauti na kukumea au kuchukua hatua ya kukomesha jambo hilo kwa kutumia nguvu. Ieleweke kuwa nguvu ya wananchi ni kubwa kuliko nguvu ya dola. Ninawataka viongozi wa Serikali watumie busara kuepusha wananchi kuamka dhidi ya serikali kwa vitendo wanavyomtendea mbunge wao.
 
Pamoja na maoni mazuri mkuu, endapo CDM wakikaa 'kimya' katika hili, polisi wataendelea kutuonea. Mi nashauri walianzishe... liwalo na liwe...
 
Hata kama umechoka na Lema, basi si umwache amalizie kipindi chake? Tambua kwamba asilimia kubwa ya wanaArusha ambao ni vijana na akina mama wako upande wa Lema maana wakiamua kufanya lolote dhidi ya serikali, Arusha haitakalika. Ni kwa busara hii watu wanachangia mawazo tufanyaje Arusha isitibuliwe. Nataka hili lijulikane wazi kuwa maadui wa Lema ni maadui wa WanaArusha. Lolote baya au zuri watakalofanya kwa Lema, wanawafanyia WanaArusha. Nawataka waelewe pia jambo lolote zuri hupongezwa na jambo lolote baya hulaaniwa. Kulaaniwa huko hufanywa kwa kupaza sauti na kukumea au kuchukua hatua ya kukomesha jambo hilo kwa kutumia nguvu. Ieleweke kuwa nguvu ya wananchi ni kubwa kuliko nguvu ya dola. Ninawataka viongozi wa Serikali watumie busara kuepusha wananchi kuamka dhidi ya serikali kwa vitendo wanavyomtendea mbunge wao.

Serikali haina tena mpango wa kutumia busara. CCM imeshapanic, na dawa yao ni kulianzisha tu...
 
Busara itumike tu,ccm rudishini imani kwa wana arusha kwa kumtoa kafara mkuu wa mkoa otherwise hata udiwani mnaweza msiambulie hata kiti kimoja
 
Tatizo lako unatumia taarifa za JF kuhukumu mambo usiyoyajua kwa undani...

tatizo lako, na wewe bado upo JF kukusaidia kupata posho na familia yako. ila huu udhalimu unaofanyika ipo siku utakwisha tu, maana mnachochoe wenyewe kwa siasa zenu chafu.
 
Ubinafsi wao, watawala serikalini na CCM kwa ujumla, umewafanya wasahau hata historia ipoje juu ya tawala kama hizi; na, hawakumbuki tena kuwa uonevu wao wa waziwazi unawafanya wananchi wapate ufahamu mkubwa zaidi na hamasa kubwa zaidi ya mabadiriko. Ufahamu wao umefunikwa na kiwango cha juu sana cha ubinafsi, hata hawawezi tena- licha ya kuona hali halisi- kukubali kuwa wananchi wa leo siyo wale wa juzi. Kama CCM wanahisi kuwa wapo katika mstari sahihi katika kushughulikia mustakabali wa taifa letu, Tanzania, basi na waendelee tu; ila, wajue kuwa mwisho wa siku watajilaumu kwanini hawakuikabidhii nchi kwa wenye nayo, wananchi, kwa amani.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom