Ninalaani vikali kukamatwa kwa Lema! CHADEMA msipochora mstari...

Ninalaani vikali kukamatwa kwa Lema! CHADEMA msipochora mstari...

Arusha.
Mbungewa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema amedai kupokea ujumbe wa vitisho kwasimu kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo.
Akizungumzana waandishi wa habari mjini hapa jana, Lema alidai kuwa ujumbe huo umeandikwakupitia simu ambayo namba 0752960276 na unaosomeka: Umeruka kihunzi chakwanza, nitakuonesha kuwa mimi ni serikali, ulikojificha nitakupata na nitakupakesi ninayotaka mimi.
Alisemabaada ya kupata ujumbe huo, alimjibu kuwa nimekupata nimekuelewa nipo tayarikwa lolote.
Hata hivyo, Mulongoamekana kumtumia Lema ujumbe huo... Nimepata hizi taarifa wewe ni kama mtu wanane kuniuliza. Sijatuma huo ujumbe na siwezi kuwa na mawazo ya kumtumia ujumbehuo kwani kama ningetaka kumkamata tangu jana pale Chuo cha Uhasibuningemkamata................................
Source: Mwananchi

My take:

Haya majibu ya Mkuu wa Mkoa yanaonyesha ni jinsi gani watawala wetu wa CCM walivyolewa madaraka.

OMG, hivi ni lini Mungu atatukomboa kutoka kwa wakoloni wetu hawa???

usishangae mkuu wangu,kwa mtu ambaye amewahi kutana na kufanya mazungumzo na mulongo lazima ajiulize ktk tanzania ya sasa mtu mjinga kama yule ameteuliwaje kuwa mkuu wa mkoa nyeti kama arusha! jamaa mshamba na anapenda kujisifu mambo ya kijinga.
 
Tatizo siasa inaingilia mpaka mambo mengine ambayo hata hayahusiani
Vijana wanatapatapa na hawajui hatma yao...Serikali chini ya wizara husika ichukue maamuzi ya busara vijana warudi chuoni na wasihusishe siasa kwani inaonekana kuna chuki kati ya RC na MB
 
Inasikitisha kwakweli maana ishu ilikuwa ni busara itumike sio nguvu
 
KUKAMATWA KWA LEMA: MKUU WA MKOA ARUSHA ALISTAHILI KUZOMEWA
Nimefuatilia kwa karibu suala la kuzomewa kwa mkuu wa mkoa wa Arusha na kitendo cha “kuvamiwa” kwa mheshimiwa Lema na kisha kuwekwa ndani. Nimetazama pia video inayoonyesha jinsi mheshimiwa Lema alivyofanya juhudi kubwa sana za kutuliza hasira za wanachuo wa Uhasibu waliokuwa wakijiandaa kuandamana kwenda kwa mkuu wa mkoa.
Nimemtazama pia mkuu wa mkoa (kwenye video) jinsi alivyoingia pale chuoni na kutoka, kisha kuongea na wanachuo. Kwa mtazamo wa haraka haraka, huyu mtu hana sifa ya kuwa kiongozi wa watu.
Kwanza, alivyoingia na kuondoka kwa kisingizio cha kukosa kipazasauti na “kukerwa” na kelele (sio zomeazomea) za wanachuo (wenye uchungu na majonzi) ni ushahidi wa wazi kuwa amelewa madaraka. Yeye alitarajia nini kutoka kwa watu wenye ghadhabu? Alitarajia kupigiwa makofi na kuimbiwa nyimbo na utukufu? Kama ilivyo kawaida ya viongozi wetu.
Pili, ikafuata zomeazomea. Kuzomea ni dalili kuwa wanachuo hakuridhika na maongezi yake. Na kwa fikra zake za “kizamani”, akadhani watanzania wa sasa ni wale wa “kale” wanaoabudu viongozi hata kama ni “mbumbumbu”. Kwa hiyo matarajio yake ya kubudiwa yakazikwa papo kwa papo. Yeye hakupaswa kuogopa wala kushangaa kuzomewa. Lakini kwa kukosa kwake busara kaligeuza suala dogo kuwa kubwa sana. Si kwa manufaa ya wanachuo wala taifa, ila kwa manufaa ya “utukufu” aliouzoea.
Tatu, anatumia neno “serikali” kuonyesha kuwa yeye yuko juu ya kila kitu. Ati anawaamia wanachuo kuwa wameiita “serikali”, na kisha baadaye anatumia neon hilo kwenye ujumbe ambao Lema anasema alimtumia: “…nitakuonesha kuwa mimi ni serikali…” Kwa mtazamo wake serikali ni wale walioko madarakani. Na kwa kwa mtazamo huo huo wa “kikale”, serikali lazima iabudiwe kama Mungu-mtu. Pengine ni kwa kuwa inashikilia vyombo vya dola ambavyo tunshuhudia vikiamrishwa kutekeleza matakwa ya hao wanaojiita “serikali”.
Haikubaliki, na wala haikutarajiwa, kuwa kuzomewa kwa mkuu wa mkoa (aliyeshindwa kuongea na wanachuo) kukawa chanzo cha kuvunjika kwa amani Arusha. Nasema hivyo kwa sababu sioni kosa lolote alilofanya Lema lenye kuhidhinisha “uvamizi” nyumbani kwake. Kwa kuwa huyu ni mwakilishi wa wananchi, sitegemei amani iwapo wananchi wa Arusha wanainuka kumtetea mbunge wao.
Kwa hakika, hata Lema asingekuwa shupavu na mvumilivu, hata yeye angeghadhibika kwa kuwa kelele za wanachuo ziliendelea akiwa anaongea. Kwa kuwa yeye ni kiongozi wa watu (sio mtawala) alifanya juhudi kuwatuliza ili walau wapete ujumbe wake wa amani. Hakuwa na kipazasauti na wala hakusema wanachuo hawana nidhamu ati kwa kuwa wanapiga kelele!!! Hapo ndipo tunapotofautisha ya “kiongozi” na “mtawala”. Mtawala anakuja na askari wake na kiburi cha kuwa analindwa na hapaswi kupata misukosuko! Kwake yeye misukosuko ya kawaida (kama kuzomewa) ni kuvunjiwa heshina na kudhalilishwa hadhi yake ya “utukufu”.
Isitoshe, nguvu iliyotumiwa na polisi pale chuoni (kurusha mabomu ya machozi) ilikuwa kubwa kupita kiasi. Pengine hiyo ndiyo tafsiri ya neno “serikali” analotumia mkuu wa mkoa kuonyesha mabavu yake kwa raia wanaodai haki. Hata hivyo hatumshangai kwa kuwa anaendelea kuuonesha umma wa watanzania jinsi “serikali” yao ilivyo. Ndivyo ilivyo na itaendelea kuwa hivyo hadi hapo watanzania watakapogundua kuwa wao ndio hasa “serikali halisi”.
Hizi ndizo dalili za kuanguka kwa “serikali”. Hata Africa Kusini, wakati wa kudai haki dhidi ya ubaguzi wa rangi “serikali” zilikandamiza raia na hata kuwaua. Lakini ukandamizaji siku zote haushindi nguvu ya watu kudai haki. Waafrika Kusini waliishinda “serikali”. Tuliyaona hayo Yugoslavia, Libya, Misri, na kwingineko. Tujiandae kuyaona pia Tanzania.
 
Aisee huu kweli ni uonezi wa wazi kabisa nimeona video lakini haya yanamwisho kabisa. Ngojeni tusubiri.
 
We are paying the price ya kupeleka wezi magari bungeni
 
:frusty:duuh too bad for our next generation,wakweli huwa hawana nafasi kabisa nchi maskini..selfish kills us.
 
Viongozi wetu kila siku wanapiga kelele lakini naamini madaraka yanawadanganya mnasahau maana ya amani tenda haki amani itakuwepo . Serikali imeoza kuanzia ikuru mpaka kwa balozi .watu tuna hasira sema tumenyamaza
 
We are paying the price ya kupeleka wezi magari bungeni

sasa la wezi wa magari linahusiana na nini kukamatwa kwa lema. huku kukiwa wazi kunaonekana kuwa ni kuonewa tu huko kwa vile Mulongo ana polisi na fiotina tu.
 
hata cc tunaujua umafia umafia wetu ni kwenye sanduku la kura cc mambo yetu ni chini ya jamvi lakini kura lazima zitoshe 2015
 
Mkuu Mzee Mwanakijiji, kwanza pole kwa kuumia nafsi katika kuyashuhudia haya. Nimekusoma in between the lines, nakushauri urejee nyumbani Tanzania, uwashauri hicho cha kufanya ili kuutuma ujumbe wa "enough is enough".

Nimekushauri kwanza urejee, ndipo uwashauri, ili usimamie utekelezaji wa hiyo "enough is enough", vinginevyo ningekushauri, uwashauri wewe ukiwa huko huko, nikakikumbuka kisa cha "Kinjekitile"

Kwani ukweli unajali umbali na ushauri unadai mahali? sihitaji kurudi nyumbani kutoa ushauri kama vile wewe huitaji kuja hapa Marekani kunipa ushauri wa kurudi nyumbani...
 
Tatizo lako unatumia taarifa za JF kuhukumu mambo usiyoyajua kwa undani...

dada ZeMarcopolo upo??nilikuwa sijakuona kwenye anga zangu kwa muda....hebu ukachukue ujira kisha uanze kufikiria kwa ubongo na sio kwa masaburi kama ufanyavyo wewe...kakojoe ulale
 
Last edited by a moderator:

Similar Discussions

Back
Top Bottom