Ninaishi na maumivu

Evelyn Salt

JF-Expert Member
Joined
Jan 5, 2012
Posts
77,117
Reaction score
165,385
Sikujua kama kuna siku itakuja kuja niishi na maumivu kwa kiasi hiki. Mipango ya Mungu ni Migumu sana sijui hata kwanini kaamua hili.

Mi namuita mtoto wangu, (mtoto wa kaka, kaka ninaemfata kuzaliwa) alifariki july 2025, hakika Mungu kaamua kunipa maumivu.....

Binti yangu huyu alianza kuumwa mwaka jana october, siku ya nyerere day aliamka na uvimbe usoni mama akajua labda kapigana tu na mdogo ake kama kawaida fujo za watoto, siku ya pili uvimbe ukazidi ya tatu uvimbe ni mkubwa hadi umepush jicho nje, wakaenda hospital. Majibu akaaambiwa hawana uhakika ila ni dalili ya cancer (walimficha tu ila walijua ukweli) binti yangu kaanza matibabu na akakaa sawa. Ikawa aje ocean road kuja kuanza chemotherapy.

22 june nikamfanyia booking ya sgr aje kwa ajili ya matibabu, hiyo siku nikaenda kumpokea anatembea mwenyewe anaongea na simu kuwajulisha siblings kuwa kafika nlifurahi kumuona. Tukaanza utaratibu wa hospital, kujisajiri nk.

27 June ilikua birthday yake akitimiza miaka 6 japo ni siku tumetoka hospital ila tuliamua akate keki tule...

Ijumaa birthday, jpili hali yake ilibadilika akaanza kutapika usiku jtatu tukaenda muhimbili emergency....tumemuuguza july 16 akafariki mwanangu.

NIMESHINDWA KUPONA 😭😭😭
Pumzika kwa amani mwanangu, Mungu nilimuomba sana anihurumie kwa ajili yako ikashindikana. Nina maumivu sana.

Inaniuma nimempokea anatembea lakini nikapeleka nyumbani kwetu Jeneza 😭😭 Mungu nitamlilia sana
 
Pole sana. Mungu akupe nguvu ya kuhimili machungu haya
 
poleeee jaman Mungu akutie nguvu
 
Pole sana dada
 
Pole sana mkuu, binadamu hujafa hujaubika. Pole sana mkuu
 
Pole sanaa cc
 

Pole Eve. Pole sana Baby
 
Pole sana Mungu akutie nguvu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…