Ninaishi na maumivu

Ninaishi na maumivu

Sikujua kama kuna siku itakuja kuja niishi na maumivu kwa kiasi hiki. Mipango ya Mungu ni Migumu sana sijui hata kwanini kaamua hili.

Mi namuita mtoto wangu, (mtoto wa kaka, kaka ninaemfata kuzaliwa) alifariki july 2025, hakika Mungu kaamua kunipa maumivu.....

Binti yangu huyu alianza kuumwa mwaka jana october, siku ya nyerere day aliamka na uvimbe usoni mama akajua labda kapigana tu na mdogo ake kama kawaida fujo za watoto, siku ya pili uvimbe ukazidi ya tatu uvimbe ni mkubwa hadi umepush jicho nje, wakaenda hospital. Majibu akaaambiwa hawana uhakika ila ni dalili ya cancer (walimficha tu ila walijua ukweli) binti yangu kaanza matibabu na akakaa sawa. Ikawa aje ocean road kuja kuanza chemotherapy.

22 june nikamfanyia booking ya sgr aje kwa ajili ya matibabu, hiyo siku nikaenda kumpokea anatembea mwenyewe anaongea na simu kuwajulisha siblings kuwa kafika nlifurahi kumuona. Tukaanza utaratibu wa hospital, kujisajiri nk.

27 June ilikua birthday yake akitimiza miaka 6 japo ni siku tumetoka hospital ila tuliamua akate keki tule...View attachment 3466019

Ijumaa birthday, jpili hali yake ilibadilika akaanza kutapika usiku jtatu tukaenda muhimbili emergency....tumemuuguza july 16 akafariki mwanangu.

NIMESHINDWA KUPONA 😭😭😭
Pumzika kwa amani mwanangu, Mungu nilimuomba sana anihurumie kwa ajili yako ikashindikana. Nina maumivu sana.
Stay BOLD, Living is temporary, death is permanent.
 
Pole sana, Mwenyezi Mungu awafanyie wepesi kukubaliana na hili, kuondokewa kunauma sana ila kuondokewa na mtoto naona kunauma zaidi,
 
Pole sana mkuu.

You will never heal 100% and this show how much you loved that kid.

Lakini kushare kwako hapa, ni hatua muhimu katika kupunguza maumivu.

Poor kid she didn't got a chance to fight this deadly disease.

My her soul rest in eternal peace.
 
Back
Top Bottom