Ninadaiwa Tala, Branch na M-pawa. Nisipowalipa watanifanya nini?

Tangia lile sakata lililosababisha mpaka bosi wa voda akamatwe, sakata ambalo tala nao walihusika, hawajatoa tena mikopo.

Nadhani BoT watakua wamewapiga pini la kimya kimya, au walivyotaitiwa wakati wa lile sakata ikabidi watumie hadi mtaji kuwanasua mabosi wao kutoka lockup.

Mie mwenyewe nimeomba mkopo tangia mwezi uliopita na bado sijapata.

Wanadai wanachunguza maombi yangu wakati huko nyuma mikopo ilikua inatoka dakika hiyo hiyo na hata siku moja sijawahi kuchelewa kulipa mkopo.
 
Hawa wana kesi, hawatoi mikopo. washenzi sana badala ya kusema ukweli, wanawapa matumaini watu kumbe biashara imekufa
 
Vipi Mkuu, ufikirii hawa jamaa kutumia details zako siku za mbeleni kwa kukuzushia SAKATA...!!

Maana nao watatafuta pa kuponea...
Tangia lile sakata lililosababisha mpaka bosi wa voda akamatwe, sakata ambalo tala nao walihusika, hawajatoa tena mikopo. Nadhani BoT watakua wamewapiga pini la kimya kimya, au walivyotaitiwa wakati wa lile sakata ikabidi watumie hadi mtaji kuwanasua mabosi wao kutoka lockup. Mie mwenyewe nimeomba mkopo tangia mwezi uliopita na bado sijapata. Wanadai wanachunguza maombi yangu wakati huko nyuma mikopo ilikua inatoka dakika hiyo hiyo..na hata siku moja sijawahi kuchelewa kulipa mkopo.
 
Vipi Mkuu, ufikirii hawa jamaa kutumia details zako siku za mbeleni kwa kukuzushia SAKATA...!!

Maana nao watatafuta pa kuponea...
Naomba wajaribu. Siku hiyo ndio nitakua nimepiga bingo...maana nitawaburuza mahakamani nidai fidia ya 1Bn. Uzuri sijawahi chelewa hata siku moja kuwalipa hela yao..so hawana kisingizio.
 
Hio hapo, shenzi hawaa! Nawashauri tu wadaiwa sugu msilipe mikopo hio
Screenshot_20190518-171902~2.jpeg
 
Kweli kabisa Mkuu..!
We wachunie tu, kwani Makampuni mangapi yanafungwa kwa kujitangaza kufilisika...!
Mimi wananidai 390,000 ila nimeogopa kulipa maana nahisi nitakuwa nkmeshaitoa kafara hiyo pesa sinto ipata tena
 
Habari wana jamvi wenzangu, hivi karibuni kumeibuka wakopeshaji wengi wa mitandaoni, wakiwemo hawa marafiki pendwa wa TALA.

Lakini kinyume na matarajio yao kume kuwa na wimbi kubwa la wakopeshwaji ambao wana yakimbia madeni yao au hata kubadili simu kabisa.

Sasa kitu cha kushangaza mimi mwenyewe nimejikuta nikiwa muhanga wa jambo hilo na hasa baaada ya kupata taarifa nyeti kutoka kwenye jukwaa humu kwamba jamaa wana kwepa kodi ya serikali, hivyo nikaona kumbe hawa jamaa sio waaminifu ngoja na mimi nijaribu kukwepa deni lao ili wajaribu kuangalia ni kwa kiasi gani serikali inaumia kwa kitendo chao hicho cha kukwepa kodi pia.

Lakini pamoja na yote wame kuwa wakinitumia sms kwamba tutakufuata hapo ulipo kama usipo lipa hela yetu leo, kitu ambacho hawajakifanya kila itwayo leo, je nikweli wana ubavu wa kunifuata mpaka home au kwa kazi?

Mlowahi kufuatwa tupeni mbinu na namna bora ya kukabiliana na maswali yao kama wanavyo sema kwamba watakuja na madalali wa yono.
 
Ujumbe wao kwangu suku ya leo.

''Unajua kabisa umekiuka masharti ya mkopo wa TALA kwa kukaa muda mrefu bila kulipa lakini bado hukamilishi mkopo huu, hii ni kama unafikiri kuna siku tutaacha kukudai,ukweli ni kwamba tutaendelea kukupa taarifa kila siku huku hatua nyingine zikiendelea kuhakikisha tunakufuatilia kiundani, miamala yako, mawasiliano yako, na kuhakikisha unapatikana haijalishi ni lini, hakikisha unalipa leo deni lako la TALA kabla hatujakufikia kwani hatutakuwa na huruma''
 
Ujumbe wao kwangu suku ya leo.

''Unajua kabisa umekiuka masharti ya mkopo wa TALA kwa kukaa muda mrefu bila kulipa lakini bado hukamilishi mkopo huu, hii ni kama unafikiri kuna siku tutaacha kukudai,ukweli ni kwamba tutaendelea kukupa taarifa kila siku huku hatua nyingine zikiendelea kuhakikisha tunakufuatilia kiundani, miamala yako, mawasiliano yako, na kuhakikisha unapatikana haijalishi ni lini, hakikisha unalipa leo deni lako la TALA kabla hatujakufikia kwani hatutakuwa na huruma''
Usipo leo kesho tena wata kwambia leo
 
Tala hawakopeshi tena nadhani changamoto ya wasio rejesha imekuwa kubwa.. On other hand wakopaji wabaya ndio adui wa wakopaji waaminifu. Vimkopo hivyo vinasaidiaga sana, sasa unakuta kuna baadhi ya watu wakiona njia hizi rahisi za kukopesheka japo vijisent basi wao wanakimbia na madeni hayo kama vile wanawakomoa wakopeshaji... Akili matope kabisa, matokeo yake wakopeshaji wanafilisika au wanaacha kukopesha.... Wapo watu wansokopa vizuri na kurejesha vizuri.. Wameathiriwa na huu mtindo wa wadaiwa sugu.
 
Back
Top Bottom