Vodacom Tanzania: Kwanini mnataka kunisitishia huduma ya kukopa M-PAWA halafu tena mnaniuliza kama ninahitaji mkopo?

Infantry Soldier

JF-Expert Member
Feb 18, 2012
6,984
2,000
Shikamooni wakubwa zangu wote wa hapa jamiiforums. Mimi mdogo wenu (Last Born) Infantry Soldier nipo mzima kabisa wa afya. Thanks to God the Almighty.

Sio kila muda tunapaswa kusoma na kujadili makala zinazohusiana na masuala ya Cold War, jeshi na ujasusi wa KGB. Leo ngoja tujadili kidogo changamoto za maisha katika jamii tunamoishi.

Eti ndugu zangu Vodacom Tanzania;

Kwanini mnataka kunisitishia huduma ya kukopa M-PAWA alafu tena mnaniuliza kama ninahitaji mkopo?

Screenshot_20200809-132208.png

Hii message iliingia kwenye simu yangu nikiwa ninakunywa chai. Hauwezi kuamini nilicheka mpaka nikataka kuangusha kikombe cha chai chini.

MFANO KIDOGO
==========
Just imagine Aisha alikopa pesa kutoka kwa Abdallah kiasi cha 200,000 na kuahidi kulipa pesa hiyo ndani ya kipindi cha mwezi mmoja. Baada ya mwezi mmoja kufika, Aisha alifanikiwa kulipa kiasi cha 90,000 tu na kubakiza deni la 110,000 kwa maana alifikwa na changamoto kadhaa zilizopelekea yeye kushindwa kumaliza deni lake.

Baada ya miezi mitatu baade Abdallah akaamua kwenda kutoa taarifa Police kwamba Aisha amegoma kulipa sehemu ya deni iliyosalia. Baada ya Aisha, Abdallah na afisa wa Police kukaa meza moja ya mazungumzo wakakubaliana kwamba Aisha ajitahidi alipe walau kiasi cha 5,000 kila week ili aweze kumaliza deni lile kidogo kidogo na endapo atashindwa kufanya vile basi hatua kali za kisheria zitafuata.

Sasa punde baada ya mazungumzo yale kuisha na kila mmoja kurejea nyumbani, Aisha anapokea tena ujumbe wa SMS kutoka kwa Abdallah na kumuuliza kama anahitaji tena kukopa pesa. Wewe unafikiri Aisha na yule askari Police (kama akipewa taarifa hii) watamfikiriaje huyu Abdallah? Is he Okay upstairs?

Pia Soma
=====
Kiingereza kibovu cha Staff wa Vodacom. M-Pawa confirmation message

Hatimaye Vodacom Tanzania wametekeleza "constructive idea" yangu niliyoandika humu JF. They were, at least, supposed to acknowledge my intellect
 
Infantry Soldier

JF-Expert Member
Feb 18, 2012
6,984
2,000
Hizo ni algorithms baba ndo zinatuma ujumbe wala sio watu wa kweli

Ni kwamba ni programs ndo zinatuma hizo jumbe kulingana na mtu alivo define parameters mbali mbali
Kwani hizo algorithms haziwezi kutengenezwa kisha zikatofautisha wateja wadaiwa na wale wasiodaiwa?
 
Naantombe Mushi

JF-Expert Member
Oct 16, 2015
3,300
2,000
Kwani hizo algorithms haziwezi kutengenezwa kisha zikatofautisha wateja wadaiwa na wale wasiodaiwa?
Hapo ni utaalamu wa programming.

Mfano wa kitu kama hichi

x = wadaiwa wote

Send message to X

So hapo ikiwa mtu hudaiwi huwezi pata hiyo message maana sio mlengwa. Ni makosa ya udhaifu wa kutengeneza programs.

Nimeongea sio kwamba nahusika, actually nime assume, ila ni kweli kwamba sio watu ndo wanatuma hizo message
 
American 2021

JF-Expert Member
Jun 11, 2020
539
500
Shikamooni wakubwa zangu wote wa hapa jamiiforums. Mimi mdogo wenu (Last Born) Infantry Soldier nipo mzima kabisa wa afya. Thanks to God the Almighty.

Sio kila muda tunapaswa kusoma na kujadili makala zinazohusiana na masuala ya Cold War, jeshi na ujasusi wa KGB. Leo ngoja tujadili kidogo changamoto za maisha katika jamii tunamoishi.

Eti ndugu zangu Vodacom Tanzania;

Kwanini mnataka kunisitishia huduma ya kukopa M-PAWA alafu tena mnaniuliza kama ninahitaji mkopo?

MFANO
===
Just imagine Aisha alikopa pesa kutoka kwa Abdallah kiasi cha 200,000 na kuahidi kulipa pesa hiyo ndani ya kipindi cha mwezi mmoja. Baada ya mwezi mmoja kufika, Aisha alifanikiwa kulipa kiasi cha 90,000 tu na kubakiza deni la 110,000 kwa maana alifikwa na changamoto kadhaa zilizopelekea yeye kushindwa kumaliza deni lake.

Baada ya miezi mitatu baade Abdallah akaamua kwenda kutoa taarifa Police kwamba Aisha amegoma kulipa sehemu ya deni iliyosalia. Baada ya Aisha, Abdallah na afisa wa Police kukaa meza moja ya mazungumzo wakakubaliana kwamba Aisha ajitahidi alipe walau kiasi cha 5,000 kila week ili aweze kumaliza deni lile kidogo kidogo na endapo atashindwa kufanya vile basi hatua kali za kisheria zitafuata.

Sasa punde baada ya mazungumzo yale kuisha na kila mmoja kurejea nyumbani, Aisha anapokea tena ujumbe wa SMS kutoka kwa Abdallah na kumuuliza kama anahitaji tena kukopa pesa. Wewe unafikiri Aisha na yule askari Police (kama akipewa taarifa hii) watamfikiriaje huyu Abdallah? Is he Okay upstairs?

Pia Soma
=====
Kiingereza kibovu cha Staff wa Vodacom. M-Pawa confirmation message

Hatimaye Vodacom Tanzania wametekeleza "constructive idea" yangu niliyoandika humu JF. They were, at least, supposed to acknowledge my intellect
Kijana ninakuona unajaribu kuwakosoa kwa faida yao wenyewe ila wanakuchukia.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom