Nina wakati mgumu; kisa kibuti....

Kipenzi Chao

Member
Oct 12, 2010
99
4
Jamani nimekuwa na my wife, ambaye tumekuwa tukiishi vizuri sana, japo kama ilivyo kawaida katika maisha tumekuwa tukipishana hapa na pale na baadaye tunarudi vema kabisa.... Lakini kikubwa zaidi ni kwamba nimekuwa na nyumba ndogo ambaye my wife hakuwahi kuijua...! Juzi nyumba hii ndogo imenipiga kibuti kikali sana, kitu kilichonipelekea kuumia sana moyoni hadi my wife anashtukia siko sawa....! Sasa nahitaji kupewa faraja juu ya kibuti hiki na wakati mgumu inayonikabili sasa....! Nafahamu fika kuwa ni vigumu mtu kunifariji bila kufahamu vema tatizo linalonikabili....! Sasa nauliza; je hali hii ngumu nimshirikishe my wife, au niitafutie nyumba hii ndogo naye msaidizi?
 
Acha UCHAFU huo...

Acha ZINAA.....

Acha NYUMBA ndogo....

MSHIRIKISHE MUNGU KWENYE MENGI YA MAAMUZI YAKO
 
...hapana, siwezi kukusaidia kumla nyama maiti,
Mungu hapendi.
 
Jamani nimekuwa na my wife, ambaye tumekuwa tukiishi vizuri sana, japo kama ilivyo kawaida katika maisha tumekuwa tukipishana hapa na pale na baadaye tunarudi vema kabisa.... Lakini kikubwa zaidi ni kwamba nimekuwa na nyumba ndogo ambaye my wife hakuwahi kuijua...! Juzi nyumba hii ndogo imenipiga kibuti kikali sana, kitu kilichonipelekea kuumia sana moyoni hadi my wife anashtukia siko sawa....! Sasa nahitaji kupewa faraja juu ya kibuti hiki na wakati mgumu inayonikabili sasa....! Nafahamu fika kuwa ni vigumu mtu kunifariji bila kufahamu vema tatizo linalonikabili....! Sasa nauliza; je hali hii ngumu nimshirikishe my wife, au niitafutie nyumba hii ndogo naye msaidizi?

Uliolea nini wakati bado hujaamua acha dharau kwa wanawake. mwache binti wa watu na ujinga wako!
Na hapo unataka kujionyesha kuwa wewe ni mchafu wa wachafu, tulia na mkeo..
 
kaka angalia sana.maana kitakachofata ni wife kugundua mwenendo wako.na akigundua nae atakupa kibuti kitakatifu.nadhani baada ya hapo ndio utajinyonga kabisa.we kama vipi poteza tu.kama unapiga lager, ongeza kipimo kidogo ili usiwaze hayo mambo.kama ni mtu wa tizi then ongeza kupiga tizi.lakini kutafuta nyumba ndogo kisa umepigwa kibuti na nyumba ndogo itakula kwako
 
mxiiiiiiiiiiiiiiii bila haya unataka tushiriki nawe DHAMBI, ushindwe
na afadhali kakupiga kibuti..sasa wewe kama mwanaume kweli unajiamini mwambie my wife wako uone kazi
umeharibu siku yangu tu mxii
 
Jamani nimekuwa na my wife, ambaye tumekuwa tukiishi vizuri sana, japo kama ilivyo kawaida katika maisha tumekuwa tukipishana hapa na pale na baadaye tunarudi vema kabisa.... Lakini kikubwa zaidi ni kwamba nimekuwa na nyumba ndogo ambaye my wife hakuwahi kuijua...! Juzi nyumba hii ndogo imenipiga kibuti kikali sana, kitu kilichonipelekea kuumia sana moyoni hadi my wife anashtukia siko sawa....! Sasa nahitaji kupewa faraja juu ya kibuti hiki na wakati mgumu inayonikabili sasa....! Nafahamu fika kuwa ni vigumu mtu kunifariji bila kufahamu vema tatizo linalonikabili....! Sasa nauliza; je hali hii ngumu nimshirikishe my wife, au niitafutie nyumba hii ndogo naye msaidizi?

mchuma janga aaahha lzm alitafune na wakwao kwa kwel we jamaa ni mchafu ka namjua mkeo ningemwambia
 
shetani anachukua maujuzi kwa wanaadam siku hizi kwahiyo hakuna cha kushangaza :rip:
 
Acha tabia mbaya mkuu
jirekebishe kuwa na heshima usifikiri unayoyafanya ni sifa ipo siku utajuta
haipendezi kuleta mada hapa ya kipuuzi halafu unataka watu kuchangia upuuzi wako
 
Umepanda aibu na fedheha, na utavuna very soon ulichokipanda,yaani unasononeka kisa nyumba ndogo,hufai kuitwa mume wala baba.
 
Back
Top Bottom