Nina tatizo kidogo na mnyama twiga

Nina tatizo kidogo na mnyama twiga

View attachment 431909

Alama ni kitu muhimu kwenye jambo lolote hasa kwa upande wa mafanikio na ustawi wa kitu, hii hujumuisha hata rangi, wanyama na alama nyinginezo. Kuna baadhi ya nchi kutokana na imani zao kali kwenye mambo ya giza hawaanzishi kitu bila kuwaona wataalam ili wawashauri alama na rangi za kutumia.

Twiga ni mnyama wa kuvutia sana, mvuto wake ukinogeshwa na urefu wake na rangi zake, ni mnyama mpole mkimya na mstaarabu sana lakini pia mvivu labda kutokana na umbile lake.

Najaribu kutengeneza roho ya mafanikio kwa kutumia nembo ya mnyama twiga naona kiza, kwa hulka za twiga ni vigumu sana kustawi kibiashara ukimtumia( wale wakosoaji wangu wanivumilie huu ni mtazamo binafsi).

Tulikuwa na shirika letu la ndege, kwa heshima ya maliasili zetu tukaamua kutumia nembo ya twiga kama utambulisho! Shirika hili halijawahi kusimama na kustawi kabisa. Limeendelea kusuasua huku likifa na kufufuka.

Tuna bank ya Twiga Bancorp(wanatumia jina na nembo ya twiga) pamoja na kuanzishwa kwa mbwembwe na kunia mafanikio lakini hivi karibuni imetangazwa mufilisi. Tunaambiwa iko vizuri tatizo ni mtaji!!!!mmh ngumu hii.

Pamoja na kwamba ustawi wa biashara hutegemea mengi lakini nembo na rangi vina umuhimu mkubwa kwenye ulimwengu usioonekana. Naiombea Twiga Bankorp bank na shirika letu la ndege lenye ndege mpya mbili (bombardier) viweze kusimama kustawi na kusonga mbele.

Umeshaanza kutumwa na mabeberu?
Naona kama si mzarendo tena
 
Kwa mtazamo wako nashauri tutumia alama ya kobe [emoji217] kwenye shirika letu la ndege, huyu mnyama kiroho anamaana zaidi kuliko twiga
Ref: kitabu cha "way of the turtle [emoji217] "

Sent using Jamii Forums mobile app
 
.
tapatalk_1553970522930.jpeg


Jr[emoji769]
 
1060202

Mavitu kama haya Mshana Jr ndiyo tuweke sio?Daah nimecheka saana...Twigaaa
 

Attachments

  • 1554130380872.png
    1554130380872.png
    21.4 KB · Views: 24
Back
Top Bottom