Nina tatizo kidogo na mnyama twiga

Nina tatizo kidogo na mnyama twiga

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
374,710
Reaction score
868,049
1478756277443.jpg


Alama ni kitu muhimu kwenye jambo lolote hasa kwa upande wa mafanikio na ustawi wa kitu, hii hujumuisha hata rangi, wanyama na alama nyinginezo. Kuna baadhi ya nchi kutokana na imani zao kali kwenye mambo ya giza hawaanzishi kitu bila kuwaona wataalam ili wawashauri alama na rangi za kutumia.

Twiga ni mnyama wa kuvutia sana, mvuto wake ukinogeshwa na urefu wake na rangi zake, ni mnyama mpole mkimya na mstaarabu sana lakini pia mvivu labda kutokana na umbile lake.

Najaribu kutengeneza roho ya mafanikio kwa kutumia nembo ya mnyama twiga naona kiza, kwa hulka za twiga ni vigumu sana kustawi kibiashara ukimtumia( wale wakosoaji wangu wanivumilie huu ni mtazamo binafsi).

Tulikuwa na shirika letu la ndege, kwa heshima ya maliasili zetu tukaamua kutumia nembo ya twiga kama utambulisho! Shirika hili halijawahi kusimama na kustawi kabisa. Limeendelea kusuasua huku likifa na kufufuka.

Tuna bank ya Twiga Bancorp(wanatumia jina na nembo ya twiga) pamoja na kuanzishwa kwa mbwembwe na kunia mafanikio lakini hivi karibuni imetangazwa mufilisi. Tunaambiwa iko vizuri tatizo ni mtaji!!!!mmh ngumu hii.

Pamoja na kwamba ustawi wa biashara hutegemea mengi lakini nembo na rangi vina umuhimu mkubwa kwenye ulimwengu usioonekana. Naiombea Twiga Bankorp bank na shirika letu la ndege lenye ndege mpya mbili (bombardier) viweze kusimama kustawi na kusonga mbele.
 
Tumifano twako tuko loko sana kuthibitisha ukakasi wako juu ya mnyama twiga, kuboronga kwa Tz katika hizo sekta ulizozitaja bado haiwi sababu za ujumla za kumkosesha credit kiumbe huyu.
I love Twiga [emoji8]
 
Tumifano twako tuko loko sana kuthibitisha ukakasi wako juu ya mnyama twiga, kuboronga kwa Tz katika hizo sekta ulizozitaja bado haiwi sababu za ujumla za kumkosesha credit kiumbe huyu.
I love Twiga [emoji8]
Nakubaliana nawe kwa mtazamo wako kwakuwa kuna kampuni kama Twiga cement inafanya vizuri sana na ndio maana nikasema ustawi wa biashara hutegemea mambo japo nayo saivi mmh mengi
1478758199331.jpg
 
Mshana buana, kuna watu walituaminisha eti bora twiga anayeruka kuliko twiga aliyesimama kama ngongoti. Wakalipa pesa nyingi nembo ya Airtz ikabadilishwa. Sasa wewe umeitumia picha yao kuonyesha uvivu wa twiga.
 
Back
Top Bottom