Nina swali kwa WanaChadema

Hili swali ungelunganisha kwenye thread ambayo umeona comment inayosupport allegation zako.

Otherwise fafanua maana hata wanachadema wana tofauti kimadaraka kimajukumu. Kauli ya Mnyika au Nape ziapewa uzito uliko kauli ya Mtazamaji au Mkandara.


BTN
Mimi sio Mwanachadema but ni mtaka mabadiliko
 
Baadhi inaweza ikaamaanisha watu2...naamini mamilioni yaliyobaki ni wale nilimo mie tunaotetea itikadi ya Cdm na si itikadi za udini,wasubiri hao2 watakujibu.
 
Vijana wa kiislam waacheni mgogoro wao UVCCM Arusha
Imamu azungumzia mgogoro wa UVCCM Arusha

Mkuu Mkandara
Ebu ona mambo ya mtu wa Madrasa huyu hapa chini, huenda ikakusaidia kuelewa sababu inayowaangusha watu wa jinsi hii:
Imamu wa Msikiti Mkuu wa Ijumaa Mkoa wa Arusha, ametoa tamko kuhusu mgogoro unaofukuta ndani ya Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), mkoani hapa na amewaasa vijana wa Kiislamu wanaojihusisha katika mgogoro huo kujitoa.
Aidha, amewaasa Watanzania kwa ujumla kutokubali kutumiwa na chama cho chote ili kuleta vurugu nchini.
Imamu huyo, Muhammad Said Hambal, alisema hayo kufuatia mgogoro uliopo ndani ya UVCCM ambao umedhihirisha kuwepo kwa makundi mawili yanayotumiwa na baadhi ya mafisadi.
Alisema kuna baadhi ya watu aliowaita kuwa ni mafisadi wanawatumia vijana kuleta vurugu kwa malengo wanayoyajua wao na akaonya kuwa hali hiyo ikielendelea inaweza kuleta machafuko makubwa katika jamii.
“Ndani ya CCM kuna vijana wanaonyesha mpasuko wa wazi…nawaasa vijana wote wa Kiislamu kuacha, wajitoe katika vurugu hizo mkoani hapa,” alisema.
Imamu Hambal alisema vijana hao wanafahamika na akaahidi kwenda kuwaona kila mmoja binafsi kuwaasa wajiondoe katika mgogoro huo.
Alisema hivi karibuni kumekuwa na madai yanayotolewa na baadhi ya vijana ndani ya umoja huo wakitishia kuchoma moto jengo la makao makuu ya CCM mkoa.
“Ofisi ya CCM ni mali umma, sasa ikichomwa moto wataleta madhara…sisi hatutaki madhara, na ndio maana tunakemea vurugu zozote,” alisema.
Alisema wamepata madhara makubwa katika maandamano yaliyoandaliwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), yaliyofanyika mapema Januari mwaka huu ambapo watu watatu waliuawa na polisi kwa risasi.
“Tumepata madhara makubwa katika maandamano yale ya Chadema, hilo ni funzo na tusingependa mambo haya yatokee tena, wengi walioathitika ni Waislamu,” alisema na kuongeza, “waathirika wa mabomu walikuwa wa hapa mjini kati ambao pia mali zao ziliharibiwa na nyingine kuibwa.”
Akizungumzia hatua ambazo watazichukua iwapo watakaidi, Imamu Hambal, alisema wataenda kuwaona wazazi wao na kama itashindikana wataacha.
Hata hivyo, alionyesha matumaini kuwa vijana hao hawatakaidi tamko lake pale aliposema, “kila muumini anatakiwa kuwatii viongozi wake na kama hawatatii sisi tutawaacha.”
Alisema CCM ni chama kikubwa na kama kuna kasoro basi wakae chini na kuzitafutia ufumbuzi badala ya kukaa kimya na kuwapa faida mafisadi kuwatumia vijana kwa lengo la kuleta vurugu.

 
Kwa nini baadhi yenu mnapenda sana kudharau Madrasa au elimu ya Waislaam kwa ujumla?

Mimi sio Mwanachadema na sio chama chochote, ila nimpenda mabadiliko. As far as your thread is concerned, they say "No research, no right to speak". I am not well clear on how you reached your conclusion. Probably you need to tell us, how was that research conducted, including the unit of analysis, sample size and sampling technigues. Was is stratified to make sure that both stratas within CHADEMA in terms of belief taken care? Did you you test the hypothesis also in other parties like CCM, NCCR Mageuzi, CUF, TLP, non part allied, etc such that you also have the feelings how the members perceive Madrasa education and related education, and why do they feel so that you differentiate them from CHADEMA? Again, did you trace the historical situation to understand how has it been the situation before. Remember that, multiparty system and so did CHADEMA came in for the first time in 1992. Now did you trace back to see how was the situation before? I think to have a good conclusion go through the advices I have aired down. It is my personal advice.
 
Na mimi pia napenda mabadiliko na CDM but am not a member, I have no qualms with Madrasa, my best friend's kids wanaattend and they are well behaved

Nafikiri kuna baadhi ya watu wanatumia hilo neno kama kejeli ili watu watukanane etc...

Remember not many discuss or view Madrasa lowly
 
Jibu nitakalokupa litakudissapoint sana! Ngoja tuache tu. Kumbuka si Kila Kila anayedharau Madrasa ni mwanaCDM
 
Mimi sio Mwanachadema na sio chama chochote, ila nimpenda mabadiliko. As far as your thread is concerned, they say "No research, no right to speak". I am not well clear on how you reached your conclusion. Probably you need to tell us, how was that research conducted, including the unit of analysis, sample size and sampling technigues. Was is stratified to make sure that both stratas within CHADEMA in terms of belief taken care? Did you you test the hypothesis also in other parties like CCM, NCCR Mageuzi, CUF, TLP, non part allied, etc such that you also have the feelings how the members perceive Madrasa education and related education, and why do they feel so that you differentiate them from CHADEMA? Again, did you trace the historical situation to understand how has it been the situation before. Remember that, multiparty system and so did CHADEMA came in for the first time in 1992. Now did you trace back to see how was the situation before? I think to have a good conclusion go through the advices I have aired down. It is my personal advice.

Research gani wewe? acha porojo. kila siku hilo neno naliona humu kama ninavyona neno m.kwere na wala hakuna anayebugudhiwa nalo.
 
Hakuna cha madrasa wala nini? Watu wamezoea kukashifu tu waislam. Hebu someni maneno haya yaliandikwa na Mbunge fulani ambaye hajasoma madrasa. (Huyu ni mbunge).

"Haya wa pili wewe. Kamanda hata hivyo si ulipanga kujitoa? Sasa kelele za nini? Jamani nafasi ilikuwa moja na msingeweza kupata wote. Mbona mnatulaumu wengine? Matusi ya nini? Kwani nani kawaambia muondoke? Bado tunawahitaji sana kwenye chama. Na bora hata mlivyoenguliwa kwenye kinyanganyiro tungkuwaje na kiongozi aliyechakachua umri? Unasahau kuwa umezaliwa 1978?ila unajifanya mtoto? Huoni aibu hata taaluma yako umechakachua, mara ooh natibu......wakati wewe ni.....
Hata hivyo uchaguzi umekusaidia umefahamika kidogo na siku hizi hata JF unaijua. Msalimie Saakumi wa Serengeti. Bado yupo au ameshaondoka?
Bravo Heche. Piga kazi Kamanda."
Yapo mengine ambayo MODS waliyatoa last year, ningeyaweka ila sihitaji ban. Sasa na huyu kasoma madrasa? Tuheshimu dini za watu.
 
Kwa nini baadhi yenu mnapenda sana kudharau Madrasa au elimu ya Waislaam kwa ujumla?
Itakuchukua muda kuelewa Mkandara, watu walishaelewa siku nyingi saana. Na ndio maana jitihada ufanyazo za kuhakikisha JF inakuwa balanced hazifanikiwi. Tumeshafika point of no return, sasa next stage hatujajua itakuwaje? Maana impact yake ni kwenye vyama. Na hii hali ipo JF kuliko hata mtaani. Mitaani watu wanaheshimiana na wanajua karibu kila mtu ana nduguye aliyopo upande mwengine kwahiyo heshma inaendelea kuwepo. Yaani strategy ya divide and rule hapa imefanikiwa saana.
 
Kwa nini baadhi yenu mnapenda sana kudharau Madrasa au elimu ya Waislaam kwa ujumla?

Hili swali, halijatulia.
Unawajuaje kuwa ni wanachadema?
Au ina maana mtu yeyote atakaye kashifu uislam/elimu ya waislam hapa JF basi lazima tu atakuwa mwanachadema? Hapa napinga.

Kwa upande mwingine, malumbano ya kidini yanapotokea, wanakuwepo pia wanaokashifu ukristo/ukatoliki...
Je itakuwa haki ku-assume kuwa wanaofanya hivyo ni WanaCCM/CUF? It'll be a wrong assumption too.
 
Kwanza natanguliza pole kwa jinsi inavyoelekea limekuguswa na baadhi ya michango inayogusa madrasa.
Pili ni ushauri tu kuwa wenye maoni hayo si lazima wawe wanachadema.
Tatu wewe mwenyewe chunguza mwelekeo wa michango hiyo ni ya kujihami au ya kuchokoza?

Kama baadhi yetu tujionavyo nafsini tena mbele ya Mwenyezi Mungu hili suala ulilolizungumzia kweli lipo na kuna chanzo. Rahisi tu fikiria ukishabikia CDM mtu anakujibu mkatoliki (yaani mkristo) inauma sana; kwa sababu kwa bahati mbaya unaweza ukawa si mkristo lakini dhumuni la mwandishi wa aina hii ni matusi na dharau hata kebehi inayodhalilisha.

Chunguza tawala zilizopita za Mwinyi na sasa JK bila kukuficha zimeleta uislamisation kwenye serikali kwa makususdi na kuumiza na kuathiri baadhi ya maisha ya watu. Si ajabu wengine tukikumbuka tunaropoka kwa frustration hiyo. Lakini ebu jiulize JK anapohutubia udini kwa lengo la kushambulia watu wenye dini tofauti na yake, halafu mtu huyo huyo hana show case ya kujivunia ila visingizio kwa wapinzani wenye dini tofauti na yake. HII NI MBAYA NA INAKWENDA MBALI KUPITA UNAVYO ULIZA KIUPOTOFU.

Cha kufanya

Turudi kwenye katiba yetu na utamaduni wetu ambao dini ni suala la mtu binafsi maana yake utakapolitaja hadharani kama ni nyezo au hoja ya kubaguana madhara yake yanakwenda mbali kama unavyouliza kuwaingiza waliopo na wasiokuwepo. Ingewezekana wote wote tukalichukulia kuwa ni hatari kama kumtongoza baba/mama mkwe (yaani kuvunjiana heshima na madhara yake) tulipe mipaka mawazoni mwetu na midomoni mwetu. Kwa pamoja tudumishe kuona hakuna tofauti ya dini kwenye suala la harakati za maendeleo ya kiuchumi na kijamii.

Kweli linauma SANA labda kwa sasa kila mmoja wetu ajichunguze na achukue hatua binafsi
 
Kwa nini baadhi yenu mnapenda sana kudharau Madrasa au elimu ya Waislaam kwa ujumla?

Nafikiri swali lako umeliunda vibaya kwa ku-single out wanaChadema tu; ni watu wengi wenye elimu ya juu wanatabia kudharau wale wenye elimu ya chini. Kwa hiyo wengi wa wanaodharau watu waliofikia elimu ya madrasa tu (yaani ile elimu ya awali ya dini ambayo hufundisha watoto kusoma na kuilewa quran) ni wale walio na elimu ya kuanzia darasa la kumi na mbili na kuendelea, siyo wana CHADEMA tu. Kwa kufanya hivyo siyo kuwa wanadharau elimu ya madrasa bali ni kwa sababu wanachukulia kuwa hiyo ni ngazi tu ya kufikia elimu ya juu zaidi. Ni kama leo hii watu wanavyowadharau kielimu wabunge walioshia darasa la saba, lakini siyo kuwa elimu ya darasa la saba ni ya kudharualiwa bali ni ngazi mojawapo ya kupitia kendelea na elimu zaidi.

Hata hivyo kuna watu wasiojua viwango vya elimu za dini ambao hudharau elimu yote ya dini siyo ya kiislamu tu. Kwa mfano mtu anaweza kusoma kutokea madrasa akaendelea na elimu ya juu ya dini hadi akapata shahada mbalimbali za dini ya kiislam. Mtu mwenye elimu ya namna hiyo siyo wa kudharauliwa kielimu.
 
Back
Top Bottom