Rekebisha kichwa cha makala yako kiwe Swali kwa wasio waislam.
Kwa msaada kwa wale wasio ijua madrasat toa ufafanuzi, ukieleze elimu hiyo inalenga nini kwa wanaoisoma na faida wanazopata.
Kuelekeza swali kwa kundi moja la siasa inazidi kuchochea udini bila sababu.
Mkuu wangu siwezi kubadilisha kichwa cha makala hii kwa sababu naelewa nilichokiandika na sababu zake.
Udini nchini unatokana na siasa hizi chafu za majitaka. Tanzania hatuna Udini isipokuwa kwa kupitia SIASA za vyama na nimeandika haya makusudi baada ya kutambua kwamba CCM walicheza lugha ya Udini kana vile kuwaambia Waislaam kwamba Chadema kinampinga JK kwa sababu ni Muislaam na kwa bahati mbaya BAADHI ya waislaam walivutiwa na hoja hii kutokana na sababu ndogo sana - Dr.Slaa ni mkristu na alikuwa Padre hivyo kuna hatari ya Waislaam kubaguliwa..
Ndipo wakaanza kuhoji uwezo wa Dr.Slaa kabla ya uchaguzi na hakika walikuwa na haki ya kufanya hivyo kwa sababu hakuna mtu anayeweza kumchagua kiongozi wake pasipo kujua vizuri dhamira zake nje ya misingi ya kiutawala, na ndio maana wenzetu hufuatilia marais wao hadi chumbani. CCM walianza ku launch personal attack kwa Dr.Slaa, Chadema na Ukristu wakiwatumia viongozi wa dini na kwa uhakika zipo report za UWT zinazothibitisha jinsi viongozi wa dini walivyoweza kutumiwa kwa FEDHA kuanzisha Udini nchini kupitia mfereji huu wa Siasa za majitaka.
Binafsi sikuona tatizo kubwa zaidi ya kukemea udini tu, lakini athari za matumizi ya misikiti na makania ulifika kiwango kibaya sana cha kuanza kuwatenganisha wananchi wenyewe kwa makundi ya dini. Swala hili halikuwa siasa tena isipokuwa BAADHI Waislaam waliamini Chadema ni chama cha Wakristu na kwa bahati mbaya pia BAADHI ya WanaChadema waliamini kwamba Chadema ni mahala pao bila kujua terms zilizotumika kisiasa. Ikawa kana kwamba Chadema ni chama cha waliokoka na CCM ni chama cha Mafisadi kupitia nadharia ya kiimani ya dini na sio kisiasa tena...
Na ndio maana Mzee Mwanakijiji alipoweka mada ile ya kuhoji Urafiki baina ya CCM na Waislaam umeanza lini, waislaam walikuja juu pasipo kuelewa kwamba kila walivyoshambulia Chadema ndivyo ilivyoonyesha imani yao ya dini kisiasa.. Nikiwa na maana ukiwapinga Chadema ktk hoja ya CCM basi bila shaka unawapa support CCM..Lakini haikuishia hapo kwani hata wale waliokuwa wakibeza urafiki wa CCM na Waislaam nao pia walikuwa ktk mashambulizi ya Waislaam, CCM na Ufisadi wake kuwa kundi moja badala ya kuweka swali la Mwanakijiji kama lilivyo ili Waislaam wapate kujiuliza kwa nini wamevutiwa na kanyanga la CCM kuwatenganisha Waislaam na Wakristu kisiasa...
Vivyo hivyo mimi nimekuja toka upande wa pili baada ya kuwasoma sana wanaChadema wakirusha madogo kwa Waislaam as if CCM ni ya waislaam na hakika kuonyesha chuki yao dhidi ya Waislaam bila kufahamu kwamba sisi wote hapa ni
VICTIMS..Na hakika mada hii imedhirisha wazi kwamba sisi wenyewe tumekuwa influences kiasi gani na Udini uliopazwa. Na hakika wapo wakristu na waislaam ambao wameshindwa kutambua kwamba hizi ni siasa za majitaka na hakuna chama kinachoweza kumtumikia bwana mmoja ama upande mmoja isipokuwa tumejazwa ujinga..
Halafu basi hao wote walijaa ujinga huu wanajiita wasomi ili hali wamefunikwa na kiza kikubwa cha kuna mbali. Mkuu wangu, mimi nimepata habari za mbinu zinazojengwa kukiangusha chama Chadema nje ya nguvu ya CCM... Nakama tusipojiweka vema Chadema itakuwa hadithi coming 2015, kwani udini ukishindikana kuivunja Chadema, bado CCM wana plan C, D, E na F ambayo wewe na mimi hatutaifurahia hata kidogo..CCM leo hii hawashughulikina ujenzi wa Taifa tena isipokuwa ni jinsi gani wataweza kuivunja nguvu Chadema na hakika watu wengi hapa JF on both sides wanaisaidia sana CCM kisiasa hali wananchi wakiendelea kulia na maisha magumu..