Nina swali kwa WanaChadema

Nina swali kwa WanaChadema

Research gani wewe? acha porojo. kila siku hilo neno naliona humu kama ninavyona neno m.kwere na wala hakuna anayebugudhiwa nalo.

nimefanya tafakuri nikagundua wewe kilaza bila hata chembe ya wasiwasi,yaani na maelezo yote hayo hauelewi,we hutufai! Kasema umuhimu wa kutrace historical background ya hicho kinachosemwa,pia hali ilikuaje kabla na baada ya multiparty system, pia research techique iliyotumika,sample size nje na ndani ya kinacho lalamikiwa,kwa kuzingatia social stratification,mwisho kama ulitest hypothesis yako kama alivosema.sawa wewe mwenzetu vp? Au research siku hiz mwiko,ni kujisemeasemea tu porojo.badilika muda ndio huu.
 
sababu mnakihusisha Chadema na ukristo jambo ambalo si sahihi kabisa. hasa pale Mkulu anapopiga propaganda za kitoto eti kuna udini!!
mara oooh siju Dr Slaa ni Padre, mara oooh sijui chama cha wachaga hiki chama ni universal hakina dini wala kabila!
 
Si vyema kusema wanachadema wanadharau madrasa, ni vizuri ungetueleza kwa ushahidi kidogo, lakini pia unatakiwa kujua kuwa CHADEMA ni chama chenye wanachama wa aina zote yaania wakristo na waislam si chama cha kidini.

Tatizo linaweza kujitokeza na kuonesha kuwa baadhi ya watu wapo kinyume na imani fulani kutokana na viongozi wa dini kuingilia mambo ya kisiasa na kudakia hoja wasizozifaham. Ni kawaida kuwasikia viongozi wa vyama mbalimbali hapa nchini wakishambulia kwa maneno viongozi wa kidini kutokana na tabia yao ya kuingilia mambo ya kisiasa.

Si kweli kwamba CHADEMA inachukia uislam jaribu kufanya utafiti kwa makini isije kuwa kuna watu wanatengeneza na kueneza habari hii kwa manufaa binafsi au kwa maslahi ya chama fulani jambo ambalo kimsingi halina maslahi kwa taifa letu.
 
Ziko madrasa nyingi mf Za somali,afghanstan nigeria,waulize wenye madrasa mbona ujumbe wao haupokelewi vizuri sababu ndo wenye message ya kinachofundishwa madras ,so usiwasingizie Cdm matatizo ya madrasa !
 
nimefanya tafakuri nikagundua wewe kilaza bila hata chembe ya wasiwasi,yaani na maelezo yote hayo hauelewi,we hutufai! Kasema umuhimu wa kutrace historical background ya hicho kinachosemwa,pia hali ilikuaje kabla na baada ya multiparty system, pia research techique iliyotumika,sample size nje na ndani ya kinacho lalamikiwa,kwa kuzingatia social stratification,mwisho kama ulitest hypothesis yako kama alivosema.sawa wewe mwenzetu vp? Au research siku hiz mwiko,ni kujisemeasemea tu porojo.badilika muda ndio huu.

Hayo ndo maneno yenu, kama si mtu wa madrasa basi ni kilaza
 
Kuongezea bob walio wengi JF hawana hata kadi za CDM! Swali lako kuelekezwa CDM naona unalenga kwenye udini zaidi. Hapa JF nadhani mimi nimelitumia sana hili madrasa al sul kwa wale wenye chuki zidi ya ukristo....mfano angalia gazeti la An-nuur na ile radio ya Moro! Post zenye kumwita padre, wakatoliki, wakristu, kafir, na chochote Kama hicho kwa Dr Slaa na wapenzi wa CDM najua wawafahamu niwaambiao wazee wa hiyo madrasa bila kudharau wenye michango yenye akili JF bila kuweka kashfa
 
Hii thred haina manufaa kwa wa tz. Ni muendelezo wa kutugawa kwa dini zetu. wengi wanachangi kishabiki na kwa kuropokwa bila kuwa na ushahidi hata chembe. Tafuteni topiki zenye manufaa kwa wote bila kubagua dini zao kam hauna kaa kimya.
 
Kuongezea bob walio wengi JF hawana hata kadi za CDM! Swali lako kuelekezwa CDM naona unalenga kwenye udini zaidi. Hapa JF nadhani mimi nimelitumia sana hili madrasa al sul kwa wale wenye chuki zidi ya ukristo....mfano angalia gazeti la An-nuur na ile radio ya Moro! Post zenye kumwita padre, wakatoliki, wakristu, kafir, na chochote Kama hicho kwa Dr Slaa na wapenzi wa CDM najua wawafahamu niwaambiao wazee wa hiyo madrasa bila kudharau wenye michango yenye akili JF bila kuweka kashfa

Ha ha ha
Usijitetee, jibu swali
 
Teh teh teh, kwani hilo gazeti na radio ndio madrasa? kama ni hivyo nitakubali ndiyo

Hapa umerudi kundini.... An-nuur gazeti na ile radio ni full Madrasa al sul....halina ubishi hilo
 
Kwanza nitaanza na kuwashukuru nyote mlionipa majibu ingawaje wengi wenu hamkutaka kukubali ukweli kwa sababu mnazozifahamu. Kwa mfano wapo watu wasiokuwa wanachama wa Chadema wamejibu kupinga hali wakidai wao sii wanachama wa Chadema kwa hiyo swali haliwahusu..na majibu mengine toka wanachama yamejieleza wazi kwa kejeri hata ktk mada hii acha hizo nyingine ambazo nimezifanyia uchunguzi kabla sijaandika kuuliza swali hili. Na majibu mengine nimeyawekea alama ya likes kuonyesha tu jinsi watu walivyokuwa na fikra finyu wakati muda wote wamekuwa watetezi wakubwa wa Chadema.

Pili, sii swala la watu wengine nje ya Chadema wanaona vipi elimu ya madrasa isipokuwa mimi nauliza pale panaponihusu kwa sababu najua sana dharau ya wakristu ktk elimu ya waislaam na hasa madrasa kwa sababu sii imani yao ya dini. Hivyo hata Muislaama anaweza kabisa kuidharau elimu ya biblia na hata kuwabeza watu kama dr.Slaa na udaktari wake..lakini yote haya ukiyatazama kwa umakini utakuta dharau hizi zimeingia sehemu mbaya sana ya kuunda makundi ya UDINI..

Na wapo wanaotaka kujenga hoja kwamba wanachadema hujibu haya kama kujibu mapigo lakini unajibu mapigo kwa imani ipi? sii ya dini sasa iweje leo azungumzwe dr.Slaa liwe swala la Wakristu wote? iweje mtu azungumzie JK iwe swala la Waislaam wote!. hapa ndipo naposhindwa kuelewa na hasa imetokea kwamba mapungufu ya baadhi ya watu imekuwa hoja ya Waislaam na elimu zao...

Kama kweli wana Chadema mnafikiria mnaweza kupata ushindi mwaka 2015 kwa lugha hizi, fikirieni UPYA! na haijalishi siasa za Nape NNauye na Uchagga kwa sababu tuna makabila 120 hivyo hawezi kujenga hoja against ukabila nje ya uongozi wa chama na hakuna hata sehemu moja kawadharau Wachagga au kukashifu Uchagga isipokuwa tuhuma za ku practice ya Ukabila, jambo ambalo naliona sana toka upande wa Chadema wakikashifu Uislaam na madrasa..halafu hamuwezi kunambia Nape anayasema haya kwa sababu yeye ni Muislaam na kasoma madrasa hivyo ndio maana akili zake ziko mnavyojua wenyewe.. Hata anayeshambuliwa sii Nape bali Uislaam na sababu sizielewi!

Na hakika huwezi kujua madrasa na uwezo wake ikiwa wewe ni mkristu isipokuwa chuki na dharau inayotokana na ujinga wa kutoelimika. Binafsi sii kwamba sioni mapungufu mengi ktk elimu ya Kikristu tena naweza kujaza kurasa na kurasa lakini haihusu kwani hii ni elimu ya kiimani. Ni muumini tu wa dini hiyo ndiye anajua uzito wa mafunzo hayo hata kama hayana ukweli kwangu.

Kisha hata huyo Sheikh wa Arusha, sioni wapi kazungumza vibaya zaidi ya kuwa kingozi wa dini kuwakanya waumini wake wasijiingize ktk malumbano ya kisiasa na kuelta madhara kwa wananchi. Ni maneno yapi yanayodhihirisha elimu yake kuwa ni ya madrasa ikiwa maneno haya haya huzungumzwa na wachungaji wa kikristu na sijasikia mtu akisema ni elimu ya aina gani...

Kwa hiyo wakuu zangu, kwanza niseme tu sikupndelea sana mada hii kuhamishiwa huku kwa sababu ni swala la kisiasa na nawauliza WanaChadema (chama cha kisiasa) hoja ambayo wanashindwa kuijibu isipokuwa kuendelea kutukana na wengine kukosoa swali langu wakati wamelielewa vizuri na majibu wanayo..Na hakika CCM wanafanikiwa kwa kiasi kikubwa sana kuwaweka Chadema ktk kona na hakika mnacheza ngoma yao ya Udini kama walivyotarajia wakati wao CCM pia na huyo Nape wanacheza ngoma yenu ya Ufisadi.. Mwisho wa siku the big looser atakuwa CHADEMA kwani UDINI ni hatari kuliko hizi habari za UFISADI kwa sababu Ufisadi hauna dini wala imani na hakika kila mtu anataka kutajirika ktk nchi hii ambayo sisi wote tunabeba misalaba yetu..

Waislaam wamewakosea nini WanaChadema ikiwa kweli hamchezi ngoma ya CCM?
 
Mkuu hii inahusiana vipi na thread ya swali kwa wanaCDM?
Hizi discussion zilianza taratibu kwa Mkandara kutoa angalizo kule kabla ya kufika hapa tulipofika. Kwa bahati mbaya saana Regia Mtema akiwa mhusika kwa siku ya leo. Tena angalizo lile lilikuwa kwa nia njema kabisa kama ambavyo Mkandara hujitahidi kuepushana misuguano ya kidini hapa jamvini. Lakini kama kawaida MODs leo tena wameihamishia wapi sijui. Mie nilikopi nilijua tu lazima dada yule achemke maana siasa zinamkimbiza. Ninayo na ile ya Kiranga, kwa kuwa wewe Mkuu ni mwenyeji nadhani unaikumbuka saana ile ya uchaguzi.
 
Kuongezea bob walio wengi JF hawana hata kadi za CDM! Swali lako kuelekezwa CDM naona unalenga kwenye udini zaidi. Hapa JF nadhani mimi nimelitumia sana hili madrasa al sul kwa wale wenye chuki zidi ya ukristo....mfano angalia gazeti la An-nuur na ile radio ya Moro! Post zenye kumwita padre, wakatoliki, wakristu, kafir, na chochote Kama hicho kwa Dr Slaa na wapenzi wa CDM najua wawafahamu niwaambiao wazee wa hiyo madrasa bila kudharau wenye michango yenye akili JF bila kuweka kashfa
Mkuu nimekutumia PM isome na labda nishereheshe kidogo tu kwamba CCM na wananchi kwa ujumla wanayo kila haki ya kuhoji uwezo wa Dr.Slaa kuwa rais ikiwa yeye alikuwa ama ni kiongozi wa dini. Na haki hiyo hiyo wanayo raia wote kuhoji mtu yeyote uwezo wake kuongoza ikiwa ana mahusiano makubwa na Taasisi yeyote acha mbali Upadre lakini haina maana wanaitukana dini nzima.

Nina hakika kama angesimama Sheikh yeyote wnaanchi wangekuwa na haki hiyo hiyo ya kuhoji uwezo na mahusiano yake na dini maanake hutaki kusikia Sheikh katuletea Sharia law au siio?. Ni right ya wananchi kujua maswla yeyote yanayomhusu Dr Slaa kama mgombea urais, hivyo tulitakiwa Chadema kujibu maswali yote yanayomhusu Dr.Slaa kwa staha na heshima kuonyesha uwezo na mahusano yake na kanisa kama yanaweza ku influence maamuzi yake na sio kutukana matusi ili hali tunashindwa kujibu wakati majibu mazuri sana na ya kimsingi tunayo.

Hayo magazeti ya Alnoor unaweza kwenda huko na kujibizana nao ama kuna ukumbi wa dini ambao unaweza kujumuika na wenye kupenda malumbano ya dini, licha ya hivyo zipo pia redio na magazeti kibao yanayotukana Uislaam lakini siwezi kuyatumia kama sababu ya kutukana Ukristu. Haya ni mawazo na fikra za watu wenye siasa kali na huwakilisha kundi dogo sana la waumini..
Vinginevyo ni kutukosea wengineo tusoyajua ya CCM ila kujali imani zetu..
 
Hata Mkandara analeta hoja km hizi ??!!
Mkuu wangu usilolijua ni sawa na usiku wa kiza. Nimeuliza nipate kujua maanake Uislaam unashambuliwa kushoto kulia kwa sababu ya JK, CCM sijui Nape. Na sioni mahusiano ya hawa watu na Uislaam au maamuzi yao.
 
Nadhani heading ya hii thread imefanya generalization ambayo siyo fair. JF ina members 38810, I am sure Active members ni kama 20,000. Katika hawa wanaomwaga upupu wa mambo ya kidini kila siku humu toka pande zote hawafiki hata 100 na wanafahamika. Sasa kuita that group ni wanachadema wakati hata inawezekana hawana kadi za hicho chama is completely unfair. Tena wengine kati ya hao wana ID's zaidi ya moja zenye mlengo huo huo. Uzuri wa hizi forums zinatunza statistics, unaweza pia hata kusearch neno madrassa limetumika mara ngapi na limetumiwa na nani.

Siamini kama mwanaCHADEMA, mwanaCCM au mwanaCUF wa maneromango au Nkasi, kanyigo au Mfaranyaki hata Kawe anawakilishwa na hawa religious fanatics wa JF. Kiasi kwamba maoni ya hawamembers wachache wa JF yatishie uhai wa chama fulani.

Niliwahi kulizungumzia suala hili huko nyuma kuhusu hawa religious fanatics, kuna watu walikejeli, walibeza na wengine kuunga mkono. Anywayz such charges bila kujali numbers would have been valid kama say Mbowe, Lissu au Dr. Slaa angekuwa ametoa comment ya namna hiyo.

Tukirudi kwenye hoja na haya ni maoni yangu, madrassa is regarded as elementary schooling katika dini ya kiislam, same as sunday schooling au masuala ya komunio na kipaimara kwa wakristo. Of which wanaosema say Mkandara una elimu ya madrassa, maana probably ni kwamba una elimu ya msingi tena ya kidini of which ingejibiwa na wewe una elimu ya sunday school definetely it would have been pau. Lakini sasa zikishaingia hisia za masuala ya imani mara nying statements and opinions hazichukuliwi kirahisi namna hiyo.

All in all everyone is entitled to their own opinion ila hiyo kujumlishwa na kuita wanachadema nadhani si sahihi.
 
Back
Top Bottom