Mkuu kwanza ningependa nikufahamishe bila kumung'unya maneno, mimi sio mwanachama wa CHADEMA ila ninaamini mabadiliko kwa sasa yatapatikana kwa kupitia mwamvuli wa CHADEMA.
Pili kuhusu mfumo kristo ni matunda ya JK alipoona maji yako shingoni turufu yake ya pekee ilikuwa ni kuwadanganya waislamu kwamba Dr Slaa ametumwa na kanisa katoliki kugombea urais kwahiyo yeye JK anapigwa vita kwa uislamu wake wake, lakini cha kushangaza hao masheikh walishindwa kumuhoji mbona Nyerere alikuwa mkatoliki na Mkapa ni Mkatoliki na waliongoza nchi hii hii? na amesahau ni maaskofu hao hao wakatoliki ndio walitusadikisha kwamba Kikwete ni chaguo la mungu na hatukusikia kwamba CCM inafungamanishwa na kanisa, huu ni unafki.
Kuhusu misaada ya kutoka ulaya ninavyofahamu mimi, kanisa katoliki halipokei misaada ila kanisa ndio linapeleka pesa Vatican, na kuhusu swala la shule za mashirika ya dini kuwa ghali hili nakubaliana na wewe na nalipinga swala hili kwa nguvu zangu zote. huu ni ufisadi na haukubali kamwe.
Kuhusu swala la madrasat hakuna anaedharau ila kejeri zinakuja kwa sababu masheikh ubwabwa wanaohubiri chuki kila kukicha dhidi ya wasio waislamu ndio source ya kejeri hizi. huwezi kumuita binadamu mwenzako KAFIR eti kwa kisingio sio mwislamu mwenzako.
Nakupa changamoto sikiliza Redio Tumaini na Wapo Redio, halafu sikiliza Redio Imaan utapata jibu ambalo halihitaji mkalimani.
Wow! ama kweli mimi nina ugonjwa wa kusahau... Hivi JK aliyazungumza haya lini na katika mkutano gani?..Halafu mkuu wangu kuwa na kadi ya Chadema pekee haiwezi kukufanya wewe uwe mwanaChadema isipokuwa kuwa na tumaini la kiimani na itikadi na sera za chama ndio nguvu kubwa ya chama na Wanachadema. Hiyo kadi ni sawa na kuwa na Passport tu haiwezi kuondoa ukweli kama wewe ni Mtanzania.
Halafu mkuu wangu bado hujayajibu maswali yangu hasa kuhusiana na mfumo kristo ni mfumo gani huo? maanake nijuavyo hao waislaam wanaolalamika na mfumo kristu wanailalamikia CCM na JK akiwa kiongozi wao. Hapa kidogo inanitatiza zaidi kuelewa unachojaribu kujenga na hasa kumhusisha JK na Uislaam...Kisha ninakuhakikishia kwamba JK ameyafanya mengi kusaidia makanisa (wakristu) kuliko hao Waislaam na Uislaam wenyewe tofauti na Mwalimu Nyerere ambaye alivunja mkataba na kanisa katoliki mwaka 1967 kwa kutaifisha mali zao..Kisha hao hao Waislaam wasomi wa madrasa alipoingia Mwinyi aliwarudishia wakristu mali zao ktk mkataba wa MoU.. Huyu Muislaam asiyekuwa na Elimu dunia ndiye aliyerudisha mahusiano ya Tanzania na Israel na ndiye pia aliyetuwezesha kuwa na vyama vingi (kuzaliwa kwa Chadema) pamoja na kuchukua mfumo mpya wa kiuchumi kutoka Ujamaa kuingia Utandawazi...Lakini pamoja na kuyafanya yote hayo sijakusikia ukisifia elimu ya madrasa au ndio ktk Ugaidi wa waislaam..
Hizo redio za Masheikh Ubwabwa zinapata nguvu kwa sababu Chadema tumeshindwa kujibu maswali mengi yanayowahusu...Wewe si msomi wa elimu dunia?...kwa nini unarudisha matusi ikiwa mambo mengi yanayozungumzwa na hizi redio ni kuhusu dini na yalikuwepo toka enzi za mwalimu wakifanya mihadhara pale uwanja wa Mnazi mmoja na hatukufika huku iuweje msomi wewe ushindwe kutetea elimu yako unapoitwa kafir kwani kafir maana yake nini msomi?.
Wakristu pia wana mihadhara na mahubiri ya dini ambayo pengine wewe huyasikii. Waislaam wameitwa dini ya shetani, Katukanwa Mtume wao kwa matusi yote unayoweza kufikiria lakini hata siku moja hutamsikia Muislaam akimtukana wala kumdharau Yesu ambaye ndiye DINI na sii waumini wenye kutenda madhambi kila siku na biblia mkononi. Sijui wewe unaishi dunia gani lakini hizi dini zote zipo kughiribu watu waikubaliane na imani yao against dini nyingine na imeanza toka enzi za mitume..
Mkuu wangu nawaombeni sana, na nimeliweka swali hili makusudi kama Mwanakijiji alivyoweza kuwauliza wanaCCM kuhusu Urafiki wake na Uislaam..Na kwa jazba wanna CCM walikuja na kutafsiri hoja nzima wanavyotaka wao ili mradi kudhihirisha chuki zao kwa Chadema na hakika naipatapata picha kwamba haya sii maswala ya CCM na Chadema bali yamefikia ktk UDINI na kwa bahati mbaya chama CCM na Chadema vinatumiwa vibaya na watu kueneza Udini..
Na amini maneno yangu sii wengine isipokuwa viongozi wa dini zetu, waliokufundisha kuwachukia Waislaam kwa sababu ni magaidi na yeyote aliye Muislaam hana elimu dunia... Haaa!Haaa! makubwa haya kama kweli elimu dunia yenyewe ndio hii basi hizo shule sintokwenda hata kwa bakora kwa sababu zinafundisha elimu ya chuki na Ubinafsi..Elimu ya Udini tuloletewa na wazungu kumchukia mpinzani wako ili mradi upate nguvu ya kugawanya na kutawala..
Nitamalizia tu kusema Nyote hapa, wanaCCM na wanaChadema tumeingia mkenge vibaya sana na hizi siasa za chuki. Kufikiria kwamba CCM ni chama cha Waislaam kwa sababu ya JK na Chadema ni chama cha Wakristu kwa sababu ya Dr.Slaa au cha wachagga kwa sababu ya Mbowe...Huu ni Ujinga mkuu wangu hakuna elimu dunia yeyote inayofundisha elimu dunia kwa ufinyu huu.
Na mkuu wangu mnakiweka chama ktk nafasi mbaya sana kuelekea uchaguzi wa mwaka 2015 hasa ikitokea kwamba CUF, NCCR, TLP na vyama vingine vikiungana kwani swala hili lipo mbioni linasukwa na kuna vigogo toka CCM watajiunga huko ili mradi kuiangusha Chadema..Quote my word!
Na sijui kwa elimu yenu ya dunia mliyajua haya....Karagabaho!