Nina 'supp', naweza kuajiriwa?

Nina 'supp', naweza kuajiriwa?

Asalam wakuu!

Nimemaliza chuo mwaka jana na nimesomea degree ya ualimu chuo kikuu cha UDOM tatizo langu ni kwamba nimeshikwa kozi moja ambayo natakiwa niirudie kuisoma semister ya pili pamoja na hawa mwaka wa tatu, kuhusu fomu zakuchagua halmashauri/wilaya za kwenda kufanyia kazi tulishajaza tangu mwaka jana, swali langu ni je kuna uwezekano wa kutochaguliwa mwaka huu kwa sababu a hicho "kimeo" changu?

Mwenye uzoefu na hii naomba anijuze.
kuajiriwa ni muhimu..ila hakikisha una i clear kwanza hiyo supp...
 
Katumbue ilo jipu la kimeo.. wewe bado mwanafunzi hata vyeti hutopata na uliosomaga nao
 
kuhusu ninavyojua,unapangiwa kituo kama kawaida ila halmashauiri wanakwambia mpaka uende uclear ndo unaingizwa kwenye payroll ila ajira yako inakuwepo kama kawa mpaka hapo unapochomoa kimeo,
 
Kwa siku za nyuma walikuwa waajiri halafu unakwenda kumalizia,ila kwa sasa hutapangiwa kituo na hata kama utapangiwa itakuwa ngumu kuajiriwa kwa sababu watakagua vyeti na hawata kubali uajiriwe wakati elimu ya chuo kikuu huja fuzu
 
Utapangiwa but nafasi yako itabaki km ilivyo kule utakako pangiwa mpk upeleke cheti au transcript
 
"supp ni somo kama yalivyo masomo mengine;Hivyo inatakiwa muongeze juhudi ya kulisoma ili mlifaulu vizuri" {PHILIPO M, 2013} a.k.a Kilaza wa vilaza tz.
 
Ajira utapata kama kawaida., mimi Dada yangu alimaliza UDSM alikuwa na carry akapangiwa kazi kama kawaida.! Mambo ya cheti au transcript yalisumbua kidogo kwa Afisa Utumishi lakini alieleweka na hakuwahi kusumbuliwa kuhusu mshahara mpaka transcript ilipotoka akaipeleka
 
Zamani Hiyo. Kwa sasa Cary over mpaka uclear

Sent from my itel_it1701 using JamiiForums mobile app
 
Ndalichako Empire


Only Division 1 & 2 ya 4m6
Ndo unaenda University
Division 3 diploma

Ajira kwa walimu

Arts subjects ni kuanzia GPA 3. 0

Science subjects ni kuanzia GPA 2. 8 lazima uwe na C mathematics f4

Walimu wa cheti wote lazima wawe wana D moja ya mathematics na D ya English ndipo masomo mengine yatatazamwa


Vigezo vya kusoma uwalimu ngazi ya cheti lazima uwe na daraja la 4 points 26 lakini lazima uwe na D mbili ya maths na english

Nawatakia Evaluations njema

Ask urself utachomoka?

Hapa JoB tu!

Sent from my itel_it1701 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom